Waliyoyafanya wazazi wetu kwenye kutulea na yale tunayoyafanya sisi kwenye kulea watoto wetu

Yawezekana unamchapa lkn kuna wakati unakuwa rafiki yake sana, ndio maana anapata ujasiri wa kukueleza hayo. Hilo ni jambo zuri sana sasa wapaswa kumuelewesha na hata muahidiane kuwa kuna abc's hapaswi kuzifanya na kwanini hapaswi kuzifanya. Muonyeshe kuwa haupendi kumchapa ila anakuudhi ndio maana. Na kwakuwa hofu ya Mungu ushaijenga ndani yake, itumie hiyo zaidi kumuonya kuliko fimbo.
Asante dear.Hapo kwenye urafiki ni rafiki yangu haswa nadhani ndo mana aliniuliza hivo .Mungu azidi tu kutulelea wenetu.Uwe na ucku mwema.
 
Tujitahidi kuwapa misingi mizuri toka wadogo kujua heshima ni kwa wakubwa wote sio mama na baba tuuu. Sala za familia zinasaidia kushape watoto na kupata hofu ya Mungu toka wakiwa wadogo bila kusahau kuhudhuria pamoja sehemu za ibada. Kuchapa fimbo pale inapobidi tusiache fimbo jamani fimbo zinashape sana. Mimi mama yangu alinichapa sana sana namshukuru mpk leo kwa sbb alinishape sijui ningekuwaje leo hii maana nilikua mtukutu. Watoto wa leo hawachapwi achilia mbali hata kuonywa tuu kwa ukali baadae huja huwa balaa kwa wazazi. Tujitahidi yapo mengi ya kuongelea ila tukijitajidi na kumuweka Mungu mbele atatusaidia màana peke yetu hatuwezi
Mi bado nachapa aisee!
 
Japo bado sio mzazi, naamini malezi ya zamani yalikuwa rahisi sana kulinganisha na ya sasa. Wakati nakua, wasi wasi wa wazazi wangu ulikuwa magazeti ya Shigongo na un-monitored TV, siku hizi kuna jinamizi linaitwa INTERNET. A lot of information(positive and negative) zinapatikana kirahisi sana kupitia mitandao, na zinahitaji muongozo wa hali ya juu la sivyo zina-pollute minds za watoto. Solution pekee ni wazazi kuzungumza na kuwa karibu na watoto. Ukidhani kuwa wanao wako salama kwa kuwa hawana simu za kisasa au access ya mitandao, fikiria tena.
umeniwazishaaa!
hako kasentensi ka mwisho!
DAH!
 
Unaanzaje kuidelete wakati hii ni mada inayomeza mada karibia zote za MMU!!
UMEONA ENH!
mambo mengi unaona yanaandikwa hapa ni kweli kuna mahala jamii TUMEACHA KULEA!
nawaza kuhusu baba na mama yangu nilivowatazama kama wazazi bora wenye ndoa bora kabisa!
najiuliza JE WANANGU WANATUTAZAMA HIVYO!
najiweka kwenye kundi maana jamii ni pamoja na mimi!
hili swali tukijiuliza na haya yanayoletwa humu kila uchao!
aseeee KUNA MAHALI KABISA KABISA KUNA JAMBO TUNATAKIWA TUFANYE!
-misingi ya familia imebomoka kwa kiasi kikubwa sana
-kina baba sio kina baba tena,watoto wa kiume hawajikuti kuwa proud na baba zao na wala hawatamani kuwa kama wao!na ndio hao wanaoa na kuwa wababa wa leo
-kina mama sio kina mama tena ,watoto wa kike hawajikuti kuwa proud na mama zao na wala hawatamani kuwa kama wao!
na ndio hao wanaoolewa na kupata watoto sasa
-ndoa zetu kwa kiasi kikukbwa ndizo hizi zinawakilishwa na hizi thread hapa,watoto wetu wanatamanije kuwa na ndoa if at all ndoa ndo hizi nani anaweza kutamani kuwa nazo(though mi sio muumini sana wa akishindwa mtu name nimeshindwa)
lakini wengi wanafall kwneye hii

SO GUYS!
KUNA MENGI YA KUFANYIA KAZI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA!
MENGI SANA KUSEMA UKWELI!
 
Well, ni ukweli usipingika kwamba kinamama mnajitahidi sana katika malezi kuliko sisi kinababa HASA KWA WATOTO WA KIKE.

Kizazi cha zamani, kinababa na watoto wa kiume walikuwa ni marafiki sana, nadhani ni kwa ile dhana ya kwamba yeye ndio atakuwa mrithi wa familia, ila siku hzi, watoto wa kike ndo wamekuwa marafiki sana na kinababa kama ilivyo kwa watoto wa kiume na mama zao.

Binafsi huwa nafurahi sana wife anapomletea kibesi na kumchapa kidogo binti yangu pale anapozingua. Na kiukweli namshukuru Mungu dogo yuko poa.

Tabia moja ambayo siipendi, labda ni kwa sababu mama yangu mwalimu hakunizoesha au vipi, ni TABIA YA KULILIA NGUO ZA SIKUKUU kila inapofika sikukuu yoyote.

Nilichomfundisha ni kwamba nitakununnulia nguo siku yoyote nikiwa na hela, na huwa namletea mara nyingi sana. Ila asitegemee nimletee nguo ya christmas wala easter.

Ninachoamini mimi ni kwamba, ikifika sikukuu, halafu huna hela na umeshamzoesha mtoto hayo mambo, unaweza hata ukaenda kukopa, ili tu umfurahishe. Unaingia kwny madeni yasiyo na msingi. Na ukishamzoesha hvy, daaah..!!! Inabidi ujipange.
 
Mbinu zinatofautiana kuendana na nyakati, sasa hivi tuko kwenye digital era, tofauti na enzi zetu tukiwa watoto, basi tutumie hekima na busara kuendana na wakati (Ngoma ya Msondo ngoma inahusika).. hata kipindi Nyerere anaongoza uongozi aliufanya kuendana na mazingira ya kipindi kile.. Chuma kinatema cheche sasa kuendana na mazingira ya kipindi hiki.. so tuchukue yale mazuri ya kipindi kile tunayoona bado ni relevant, tuchanganye na mazuri ya sasa tuweze kuwashape watoto ifaavyo
 
Sasa watoto wa leo ni balaaa... nimeshashuhudia kamtu kanachungulia koridoni kama kuna mtu kisha kanatoka bafuni uchiiii kanakimbilia chumbani ... ukliuliza kanasema hakukuwa na mtu... nyumba ya familia! jamaniiii
Ha ha ha hii watoto wengi hufanya nadhani ni stage ya ukuaji tu....ha ha ha
 
UMEONA ENH!
mambo mengi unaona yanaandikwa hapa ni kweli kuna mahala jamii TUMEACHA KULEA!
nawaza kuhusu baba na mama yangu nilivowatazama kama wazazi bora wenye ndoa bora kabisa!
najiuliza JE WANANGU WANATUTAZAMA HIVYO!
najiweka kwenye kundi maana jamii ni pamoja na mimi!
hili swali tukijiuliza na haya yanayoletwa humu kila uchao!
aseeee KUNA MAHALI KABISA KABISA KUNA JAMBO TUNATAKIWA TUFANYE!
-misingi ya familia imebomoka kwa kiasi kikubwa sana
-kina baba sio kina baba tena,watoto wa kiume hawajikuti kuwa proud na baba zao na wala hawatamani kuwa kama wao!na ndio hao wanaoa na kuwa wababa wa leo
-kina mama sio kina mama tena ,watoto wa kike hawajikuti kuwa proud na mama zao na wala hawatamani kuwa kama wao!
na ndio hao wanaoolewa na kupata watoto sasa
-ndoa zetu kwa kiasi kikukbwa ndizo hizi zinawakilishwa na hizi thread hapa,watoto wetu wanatamanije kuwa na ndoa if at all ndoa ndo hizi nani anaweza kutamani kuwa nazo(though mi sio muumini sana wa akishindwa mtu name nimeshindwa)
lakini wengi wanafall kwneye hii

SO GUYS!
KUNA MENGI YA KUFANYIA KAZI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA!
MENGI SANA KUSEMA UKWELI!
Kuna ombwe kubwa sana katika malezi nyakati hizi, Mungu atusaidie kwakweli.
 
Leo sisi ni wazazi wa watoto wetu lakini jana tulikuwa watoto wa wazazi wetu.
TUTAFAKARI JANA YETU NA LEO YAO!
KIPI UNAONA WAZAZI WAKO WALIFANYA KWAKO LAKINI WEWE HUFANYI KWA WANAO AU WANAO HAWAFANYI KWAKO!

INAKUATHIRI KWENYE MALEZI /MAKUZI YA WANAO
INAKUSAIDIA KWENYE MAALEZI/MAKUZI YA WANAO

mamangu alikuwa ana msemo "NOT IN MY HOUSE NOT WHEN I AM ALIVE"
ILITUSHAPE FLAN HIVI!
INATURUDIA MPK UKUBWANI SASA KIASI KUNA VITU NAJIKUTA KABISA SIWEZI KUFANYA SAUTI YAKE INALETA MWANGWI HIVI!
lakini sijawahi waambia wanangu kauli hii!
sina sababu yoyote ya kimsingi but naona kama ilibidi niwe nawaambia!

WELL HEBU LEO TUONGEE KUHUSU WATOTO NA KUSAHAHU BABA NA MAMA ZAO KIDOOOOGO!
ruksa pia hata watoto walio na wazazi wanaona kabisa mi nawish babangu/mamangu angekuwa ananikemea hivi au anasema hivi kwangu labda nisingekuwa hivi(najua tuna teenagers humu)

INAWEZA SAIDIA MTU FULANI MAHALA FULANI!
KARIBU!
We mdada mi nakukubali sana unamawazo mazuri sana kama tu unayazingatia haya unayoandika,ongera sana
 
"HAPANA USIFANYE HIVYO"
mi ninaikumbuka hii kauri ya mamaangu mdogo MWENYEZIMUNGU amrehemu alifanye KABURI lake liwe miongoni mwa VIWANJA vya peponi
ikifika weekend huwa nikipienda kwenda kwake mana ndo kulikuwa na dada zangu na bro wangu wa rika langu ambao tulikuwa tunapatana sana nikikosea lolote halikuwa hanipigi wala aniongeleshi kwa UKARI ananiambia kwa upore tu HAPANA USIFANYE HIVYO
tofauti kwa B mkubwa ukizingua hana time ya kuzungumza na wewe
MIBAO tu ya MGONGO labda ufanikiwe kuchoropoka
sasa hii kauri inanirudia sana hata hivo ukubwani hasa ninapokaribia kufanya jambo ambalo najua kabisa ni makosa
 
Siku hizi hakuna watoto..
utoto umeporwa na TV na Internet na ubize wa wazazi makazini
wamama wanaenda makazini hiki kimebadilisha kitu kikuubwa mno
ukichanganya na smart phone na kadhalika..

unaweza kukuta una binti mdogo wa miaka 9 but role model wake ni Gigi Money
au Faiza wa Sugu..but iko tu moyoni mwake
siku ikija kukulipukia usoni ndo unatamani wazazi wako wangekusaidia kuwalea wanao..
 
Dah
 
WAZAZI WETU WANAIISHI MIOYONI MWETU!!

Sisi tutaishi MIOYONI mwao???

INAFIKIRISHA MNO!!

MUNGU atusaidie Sana!!
 
WAZAZI WETU WANAIISHI MIOYONI MWETU!!

Sisi tutaishi MIOYONI mwao???

INAFIKIRISHA MNO!!

MUNGU atusaidie Sana!!
Ni shida Sana.Wazazi tusikubali tupelekeshwe na huu utandawazi.Yaliyo ndani ya uwezo wetu hebu tuyatimize tulee watoto jinsi iwapasavyo.

Hivi Kwa mfano unakuta unamwachia cm mwanao wa miaka minne aangalie clips mbali mbali bila hata kujua ipi inamfaa na ipi haimfai ukija kuta anayapractice aliyoyaona utamlalamikia nani.Tunayoweza kuyaepuka embu tuyaepuke.Bila kusaau sala na maombi jamani tuwaombee watoto wetu.

Mi huwa na utaratibu wangu kila mwaka baada ya xmass nafunga Kwa sala na maombi hadi mwaka mpya,kuombea wanangu mwaka mpya unavoanza wawe mikononi mwa Mungu.Tufanye Kwa sehemu yetu iliyobaki tumwachie Mungu.Hata mtoto akikua hana wa kumlaumu kwasababu utakua umetimiza wajibu kama mzazi.
 
Mie kuna mengine alikuwa ananiasa mama yangu (R.I.P) lakini sitayaendeleza. Kwa mfano kama siku hiyo tunapika nyama halafu akinikuta nimeokota pande la nyama ninakula bado ikiwa jikoni, kwa kisingizio cha kuonja kuwa imeiva alikuwa ana nichapa huku akitamka maneno haya "MWANAMKE HATAKIWI KULA MBOGA IKIWA JIKONI, KAMA ULITAKA KUONA KAMA IMEIVA UNGENAWA MIKONO HALAFU UCHUKUE KIPANDE KIMOJA UKIBONYEZE TU, BILA KULA" hahahhah hebu imagine kama kweli inawezekana kubonyeza nyama. Japo alikuwa na nia nzuri ya kuzuia uroho
Nimekumiss mpenzi upo kweli?
 
Siku hizi hakuna watoto..
utoto umeporwa na TV na Internet na ubize wa wazazi makazini
wamama wanaenda makazini hiki kimebadilisha kitu kikuubwa mno
ukichanganya na smart phone na kadhalika..

unaweza kukuta una binti mdogo wa miaka 9 but role model wake ni Gigi Money
au Faiza wa Sugu..but iko tu moyoni mwake
siku ikija kukulipukia usoni ndo unatamani wazazi wako wangekusaidia kuwalea wanao..
duh!
unaweza upagawe
 
Back
Top Bottom