Waliyoyafanya wazazi wetu kwenye kutulea na yale tunayoyafanya sisi kwenye kulea watoto wetu

Mi katika malezi najiona kama vile nimezidi ukali, natamani nipunguze, yani kama sielewi elewi....
Natamani kuwa kama mama wenye maneno laini Mtoto ukiongea taratibu aelewe, kijana wangu bila mikwara naona kama hanielewi
 
Kuna wazazi wao ndo wanachangia kuharibu watoto wao kwa malezi ya upendeleo kuna familia moja ina watoto 4watatu ni wa ndoa mmoja ni wa njee wa baba lkn,mama aliwabagua sana hasa yule wa baba alimnyanyasa mno ila wale watatu aliwapenda sana kiasi kwamba hata wakosee hakuweza kuwaonya wamesoma hadi vyuo matokeo yake hawana adabu kwa wazazi yaan wao sasa ndo wenye saut kweny nyumba na mama anaumia lkn ndo bomu lake akilitengeneza kwan wamekuwa hawana adabu hdi kwa ndugu na majirani yule mtoto wa kambo alifukuzwa kwenye familia kajikalia mbali anawaangaliatu wanavyotoana macho so tuwapende watoto wetu lkn tuwafanye watambue nini maana ya heshima
Ndio maana sitaki kabisa kuzaa nje ya ndoa
 
mbaya enh?
acha niidelete mwaya!
Vijana wa leo hawataelewa unachoongea madam, mada nzuri hasa kwa walio na familia/watoto.

Binafsi kuna mambo, lifestyle ya wazazi hasa baba ambayo sitaki kuwapa wanangu, naamini ilikuwa nzuri kwa kipindi kile(wakitulea sisi) lakini leo hii siwezi ku-implement kwa wanangu.

Sitaki watoto waniogope(I used to fear my dad), nataka waweze kukaa na mimi na kunieleza mambo yao,matatizo yao na changamoto zao.

Yapo mambo nitachukua toka kwa wazee na kuyaleta kwa wanangu, lakini lazima niangalie na nyakati tunazoishi.
 
Vijana wa leo hawataelewa unachoongea madam, mada nzuri hasa kwa walio na familia/watoto.

Binafsi kuna mambo, lifestyle ya wazazi hasa baba ambayo sitaki kuwapa wanangu, naamini ilikuwa nzuri kwa kipindi kile(wakitulea sisi) lakini leo hii siwezi ku-implement kwa wanangu.

Sitaki watoto waniogope(I used to fear my dad), nataka waweze kukaa na mimi na kunieleza mambo yao,matatizo yao na changamoto zao.

Yapo mambo nitachukua toka kwa wazee na kuyaleta kwa wanangu, lakini lazima niangalie na nyakati tunazoishi.
Hii ta kuogopa wazazi nakwambia sa hi automatic hawatuogopi tu!!
Kuna siku binti yangu alinijibu "but mum its not fair" akainuka akapiga mguu chini kaondoka!!
ASEEEEEEEEEEEEH!!
dooooooh sauti ya mamangu ya not in my house not when I am alive ilirudi kichwani paaaaap!
Ah NILITANDIKAAAAA!!
 
Mi katika malezi najiona kama vile nimezidi ukali, natamani nipunguze, yani kama sielewi elewi....
Natamani kuwa kama mama wenye maneno laini Mtoto ukiongea taratibu aelewe, kijana wangu bila mikwara naona kama hanielewi
HHAWA MACHALII ASEEE NAHS KAMA WANATUOVERTAKE ,KUWA TU HIVO HIVO
 
Niliwahi kumtuma mtt wa sista yangu aliletee maji akaniambia amechoka...dah imagine nimemzidi 13 yrs ivi ..wakati enzi hizo ukitumwa na mkubwa iwe umechoka hujachoka utaenda tu
KWANZA HATA KUWAZA TU KUWA UNAWEZA KUJIBU MTU HIVO?HIYO GUTS UNAITOOOA WAAAAPI?
lakin siku hizi wanajibu aseeee!!
Mtoto ANASEMa subiri nakuja!
Uuuwih kuna vitu sijui tumejisahau wapi yarabi!
 
Mwaaah Big Sam mwaah. .......

Asante kwa busu mujarabu wanihorojesha ujue..... natabasamu tuu muda wote.

Sijui jioni nikienda pale Rhodizo ntakukuta. ....... nawaza tuu
HAPO RODIZO KWNEYE KONA mniiite hapo mkunguni!
 
Nilichojifunza kwenye umaskini malezi hayaeleweki.
1. Mzazi anakuwa na watoto hasa wa kike zaidi ya miaka 20 wanazaa nyumbani na hawazalishi chochote. Hapa familia inakuwa kubwa na kuelemea watu wachache wanaojishughulisha. Mara nyingi wazazi wanaendekeza hili wanaendelea kulea hadi wajukuu.
Kuishi kwa pamoja si shida ila wenye umri wa kufanya kazi wafanye.

2. Wazazi wadogo kurudi nyumbani baada ya kuchemka. Nyumbani patumike kama sehemu ya kujipanga unakosea na si kwako kwa milele.

3. Watoto waliokua wanafikiri bado wazazi wao wana wajibu wakuwahudumia. Umelelewa tangu day 0 na umekuwa na ndevu bado na pengine umezaa bado unadai uhudumiwe. Wapumzisheni wazee wenu.
LAKINI HALI NI MBYA ZAIDI KWENYE KINYUME CHAKE my dear!!
HALI NI TETE HASA!!
 
Kizazi cha wakina James delicious hiki, kabinti ka form two kanasalimia kaka "mambo" na kijana anasalimia "inakuaje?. Hua siviitikii
 
Ijumaa usichelewe... nna mahela ya bonus toka kwa mkoloni... Amarula bado unatumia?

YeeeeyIjumaa hii ntawahi kutoka mapemaa niwahi eneo la tukio. Amarula ndo kaugonjwa kangu. Hapo hapo umelenga. See you babuuu Big Sam. .... mmuaah.
 
Tujitahidi kuwapa misingi mizuri toka wadogo kujua heshima ni kwa wakubwa wote sio mama na baba tuuu. Sala za familia zinasaidia kushape watoto na kupata hofu ya Mungu toka wakiwa wadogo bila kusahau kuhudhuria pamoja sehemu za ibada. Kuchapa fimbo pale inapobidi tusiache fimbo jamani fimbo zinashape sana. Mimi mama yangu alinichapa sana sana namshukuru mpk leo kwa sbb alinishape sijui ningekuwaje leo hii maana nilikua mtukutu. Watoto wa leo hawachapwi achilia mbali hata kuonywa tuu kwa ukali baadae huja huwa balaa kwa wazazi. Tujitahidi yapo mengi ya kuongelea ila tukijitajidi na kumuweka Mungu mbele atatusaidia màana peke yetu hatuwezi
 
Back
Top Bottom