Walitaka kuniuwa, asema Sheikh Farid

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
DSC09748.JPG


446309610_o.jpg


WASIWASI umetandakuwa huenda kuna watuwanataka kumuuwaSheikh Farid.

Hiyo ni kutokana na kile kilichojiri hivi karibuniambapo watu waliokuwakatika gari walifukuza gariyake na kuipiga risasi, lakinikwa bahati nzuri Sheikhalikuwa hayupo ndani yagari hiyo.

Wakati huo huo, mwanamke mmoja aliyekuwa akishikilia bendera ya Uamsho yenye maandishi Laaila ha ilallah, ameshushiwa kipigo kikali na polisi alipokataa kuachia bendera hiyo.

"Huyo polisi mmoja alikuwa akinilazimisha nimpe bendera, nikamwambia mimi hii siitoi hata kama utaniuwa, basi bora nife nayo mkononi mwangu hii ina Lailahaila llah… sikupi akaendelea kunipiga kwa kile kirungu cha polisi alichokuwa nacho…akanipiga tena nikaanguka chini na akanivuta bendera yangu tukawa tunanyanganyiana." Amesema Bi Riziki akiongeana mwandishi juzi.

Bi Riziki Omar Chande(42) ni mmoja wa wanawake kadhaa waliojitokeza na kueleza jinsi walivyopigwana kudhalilishwa na polisi.

Riziki Omar Chande(42) mkaazi wa Mfenesini anasema kuwa baada ya kusikia kuna mhadhara Donge, yeye alitoka mapema na kwenda kupanda gari kuelekea Donge kama wenzake lakini baada ya kufika Mahonda jeshi la polisi lilisimamisha msafara na kuwataka watu wote warejee mjini.

Hata hivyo anasema kuwa viongozi wa msafarawaliwataka wasiondoke mpaka viongozi wakuu watakapofika.

Ilikuwa ni katika muda huo huo Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake walifika katika eneo la Mahonda na kutaka jeshi la polisi kuacha kuhatarisha amani kutokana na kitendo chaocha kuwazuiya watu waliokuwa wakielekea Donge kuhudhuria mkutano uliokuwa ufanyike katika Msikiti wa Donge.

Hata hivyo badala ya kuwasikiliza na kujadiliana nao, polisi waliwafukuza kwa mabomu ya machozi na ndipo Masheikh haowalipoingia Msikitini.

Taarifa kutoka eneo latukio zinafahamisha kuwa polisi waliwafuata huko huko Msikitini kuwatawanya kwa mabomu ambapo Sheikh Farid na wenzake waliruka ukuta na kukimbia kwa miguu katika pori kutoka Mahonda kuelekea njia ya Mwangapwani.

Huku nyuma, wakidhani Sheikh Farid yupo ndani ya gari alilokuja nalo, watu wasiofahamika walilifukuza gari hilo na kulipiga risasi ambapo lilipinduka na kuharibikia vibaya.

"Sijui kama walitaka kutuuwa au vipi, lakini bahati mimi sikuwemo katika ile gari ingawa wanadhani kwamba ile gari ni yangu, lakini niseme mimi ile gari sio yangu ila nilipewa kwa kutumia kwa ajili ya shughuli za kuendeleza hizi harakati zetu", alisema Sheikh Farid muda mfupi baada ya kurudi katika hekaheka hizo ambapo walifanya mhadhara wao Mbuyuni baada ya kutokufanikiwa kupenya kwenda Donge.

Akielezea juu yakilichomfika Bi Riziki anasema kuwa kwa vile alikuwa kashikilia bendera, ilikuwa rahisi kwake kufuatwa na polisi.

"Mimi nilikuwa nimekamata bendera yangu polisi alipokuja kunichukua akanikamata mkono ananipeleka kituoni alipofika mbele kuna polisi mwenzake akawambia unampeleka kituo kama BiHarusi, mpige virungu,…yule polisi akajibu kwanini tumpige wakati amekubali kutii amri halali?"

"Mwenzake akasema, haiwezekani hao hawana adabu lazima apigwe, yeye ndio akaanza kunipiga huku akinambia nimpe bendera yangu ya Uamsho mimi nikamwambia nipige lakini bedera yangu sikupi ndio akaendelea kunipigana kunipiga", alisema BiRiziki.

"Wakawa wanatuambia maneno ya ovyo kwamba tutakoma, kwa hivyo yule polisi mmoja akawa anaendelea kunipiga alipokuja polisi mwenzake akawambia unampigia nini huyo wakati yeye amekubali umpeleke kituoni ndipo waliponichukua na kunipiga tena".

Riziki ambaye aliumia sehemu ya jicho baada ya kupigwa kibao na jicho lote kupiga wekundu, anasema kilichomshangaza ni kwamba kila kituo cha polisi alipokwenda alikataliwa kupewa barua ya kwenda kupata matibabu.

"Tunafanywa kama sio raia wa nchi hii tulipokwenda kituo walikataa kutupa barua wakati wanajua hatuwezi kutibiwa kama tumeumia mpaka tupate barua ya polisi, tulipotoka Mahonda tukaja mjini tulikwenda Kituo cha Polisi Mkunazini wakakataa kutupa kibali tukenda Malindi pia wakatwambia nyinyi nendeni tu hukohuko hospitali wambieni madaktari kuwa mmepigwa na polisi …hawakutupa."

Bi Riziki ambaye aliumia mkono na jicho anasema hata walipokwenda hospitali walikataliwa kupewa tiba hadi watakapokwenda na barua ya polisi.

Naye Hafsa Mohammed Mahfoudh (19) mkaazi wa Kinuni, Magogoni anasema katika zahma hizo watu wengi walikimbilia Msikitini na ndipo walipoona Polisi wakiingia Msikitini na kuwapiga wanawake na wanaume na kuwatoa nje huku wakitaka wanawake wote wavuliwe mashungi yao.

"Walikuwa wakisema maneno mabaya mabaya huku wakituvuta mashungi yetu wakitwambia tokeni hapa Waislamu, Waislamu, Waislamu nini, wanafiki wakubwa, na kuna askari wa kike alinivuta sana shungi na kunipiga sana kwa....

Inaendelea
 
Jama hii ya kutaka kum (sacination) Sheh Farid itakuwa ni mipango ya Usalama wa Taifa wakishirikiana na vigogo ndani ya Serekali zote mbili ya Muungano(Bara) na ya Zanzibar kwa wale wenye kupinga Serekali ya umoja wa kitaifa na kupinga Uamsho kwa kisingizio cha kupinga Muungano.

Hili liko wazi na lina mkono wao nazani Wazanzibar list za watu hawa tunazijuwa ninani na nani na tunazo.

Hawa ni wale wenye kutumia mabavu na nguvu ya Dola vibaya , lakini ikiwa wanataka kuvuruga amani ya nchi na utulivu uliopo hivi sasa Zanzibar basi wajuwe chombo kikizama na wao wamo wala hawatoki.

Hawa hawajafahamu kuwa dunia ya leo sio ile ya jana , ufanye utakavyo uachiwe tu, tutatumia nguvu yetu ya people power juu ya wamaya hawa.

Mungu ibariki Zanzibar na viongozi wetu wote wa Uamsho.
 
Baada ya Boko haram kuingizwa kama genge la magaidi, UAMSHO mtafwata hivi punde.
 
Ndivyo itakavyokuwa; ni lazima watokee mashahidi kwanza ili harakati zizidi kupata uhalali na kuwa more violent. Atauuawa mtu huko Zanzibar ili wana harakati wapate shujaa wa kuzunguka nyuma yake. Thats how it works!

You dissapoint me!
Do you really think they "missed"him?
 
Wandugu ndio maana mnaambiwa mwende shule kwanza!! Hebu tazama hata habari yenyewe ilivyokaa. Duu!!
 
Hio picha ya izo vitobo vya bullets ni edit! Na inaonekana hasa kama editing!! Khatari kweli
 
Hayo matundu ya risasi tunadanganyana, angalia kwa makini utagundua kuwa hayo matundu yanafanana muundo na size pamoja na mchoro uliyoyazunguka,
sheihk farid anataka kutafuta mori wa vijana kwa spinning.
Laila ha ilah


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Lol, nimependa hicho kidhungu cha kum-sacination. Umenikumbusha shosti wangu mzenj!

Usalama wa taifa unarusha risasi kama mpira wa nage? Hata kama maalim hakuwepo, which can't happen manake mission haifanywi kwa kubahatisha; aliekuwepo angeipata khabari yake!
Jama hii ya kutaka kum (sacination) Sheh Farid itakuwa ni mipango ya Usalama wa Taifa wakishirikiana na vigogo ndani ya Serekali zote mbili ya Muungano(Bara) na ya Zanzibar kwa wale wenye kupinga Serekali ya umoja wa kitaifa na kupinga Uamsho kwa kisingizio cha kupinga Muungano.

Hili liko wazi na lina mkono wao nazani Wazanzibar list za watu hawa tunazijuwa ninani na nani na tunazo.

Hawa ni wale wenye kutumia mabavu na nguvu ya Dola vibaya , lakini ikiwa wanataka kuvuruga amani ya nchi na utulivu uliopo hivi sasa Zanzibar basi wajuwe chombo kikizama na wao wamo wala hawatoki.

Hawa hawajafahamu kuwa dunia ya leo sio ile ya jana , ufanye utakavyo uachiwe tu, tutatumia nguvu yetu ya people power juu ya wamaya hawa.

Mungu ibariki Zanzibar na viongozi wetu wote wa Uamsho.
 
Back
Top Bottom