Walitaka kuniuwa, asema Sheikh Farid

Asante kwa kuliona hilo.

ni kweli kabisa,angalia matundu mawili ya juu yanafanana ramani yake,na mawili ya chini yanafanana pia,wanafoji watafute sympathy,na mwandishi angekuwa mkweli angewahoji na polisi wasemee tukio hilo
 
Sheikh ameonyesha picha ambapo vioo vya gari lake vina matobo ya risasi. Huu ni uongo wa hali ya juu. Amejishushia sana hadhi!!! Pole sana Sheikh (Kiongozi wa dini) Picha yenyewe ni feki na ameicopy kutoka kwenye internet!

446309610_o.jpg


Hebu tazama hapa!
http://img.auctiva.com/imgdata/1/4/7/1/6/7/6/webimg/446309610_o.jpg
 
Hii hata mimi ninadout, hebu angalia yale matundu ya risasi ule mchoro wa nje, yote manne yanafanana.:sad:
 
Nina mashaka sana na ukweli wa hii habari. Hawa jamaa zetu ni mabigwa sana wa kuunda habari ili waonekane wanaonewa na Serikali ya Muungano.

Sidhani kama wangekuwa na nia ya kumuua wangeshindwa. Yeye ni nani hata ashindikane kuuwawa? Hakuna hata mtu mmoja mwenye nia ya kuutoa uhai wake.

Hiyo gari wala haina uhusiano wowote na yeye. Kama atakufa ni kwa mapenzi ya MUNGU na si Serikali wala kikundi chochote. Asitake kujiona ni mjanja au ajifananishe na Osoma Bin Laden.
 
Shule kitu gani mkuu, wenzio tunaanza Chuo at the age of five! chezea sie weye!
Chuo chenyewe ni hicho cha kudanganya umma kwa picha feki za internet? Sasa Iwapo Sheikh anasema uongo namna hii tumwamini nani? Mnataka kuleta fujo zisizokuwa na maana. Iwapo umesoma Chuo hebu copy link ya hiyo picha na kisha u-google ili uone uongo wa Sheikh wako!!!!
 
Can you believe it? Halafu eti wanathubutu kujiita UAMUSHO...UAMUSHO, my foot! Ni kama kipofu kumwongoza kipofu! When will these guys ever wise up!

Hiyo picha iliyoletwa inauhusiano upi na Uamsho?
 
Hii hata mimi ninadout, hebu angalia yale matundu ya risasi ule mchoro wa nje, yote manne yanafanana.:sad:
Kama unataka gonga pia hapo kwenye maandishi ya blue...

Fake Bullet Holes And Damage Stickers Make The Perfect Illusion ...

bikeaddicts.net/.../img.auctiva....
30+ items – fake bullet holes and damage stickers make the perfect illusion ...
Item:6512419 Fake Bullet Holes - Who Shot My Truck???? : For Sale at
seller s description fake bullet holes set of 4318x261
 
abdulahsaf ungeweza kuziwekea maelezo angalau machache tu picha hizi (hasa hiyo ya chini) ungesaidia mjadala huu uende vizuri na hasa kuipa credibility habari yenyewe. Je huyo 'mwarabu' hapo juu ndiye Sheikh Farid?

Na je hiyo picha ya chini ni kioo cha gari lilopigwa risasi (ambalo ilidhaniwa Sheikh Farid yumo ndani yake)?
 
Hiyo picha Sheikh Farid kasema wapi kuwa ni ya gari yake?

Katika taarifa nzima hatukutajiwa kuwa Sheikh Farid alimuonyesha muandishi wa makala gari wala kumpatia picha ya ku"sindikizia" taarifa zake.

Hakuna uhusiano baina ya picha iliyowekwa kwenye makala na alichokisema yeye......
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hiyo picha Sheikh Farid kasema wapi kuwa ni ya gari yake?

Katika taarifa nzima hatukutajiwa kuwa Sheikh Farid alimuonyesha muandishi wa makala gari wala kumpatia picha ya ku"sindikizia" taarifa zake.

Hakuna uhusiano baina ya picha iliyowekwa kwenye makala na alichokisema yeye......

DSC09748.JPG


Kwa nini Sheikh anasema uongo na kudhamiria kuleta machafuko?


Hebu tazama hapa:


WASIWASI umetandakuwa huenda kuna watuwanataka kumuuwaSheikh Farid.

Hiyo ni kutokana na kile kilichojiri hivi karibuniambapo watu waliokuwakatika gari walifukuza gariyake na kuipiga risasi, lakinikwa bahati nzuri Sheikhalikuwa hayupo ndani yagari hiyo.

Wakati huo huo, mwanamke mmoja aliyekuwa akishikilia bendera ya Uamsho yenye maandishi Laaila ha ilallah, ameshushiwa kipigo kikali na polisi alipokataa kuachia bendera hiyo.

"Huyo polisi mmoja alikuwa akinilazimisha nimpe bendera, nikamwambia mimi hii siitoi hata kama utaniuwa, basi bora nife nayo mkononi mwangu hii ina Lailahaila llah… sikupi akaendelea kunipiga kwa kile kirungu cha polisi alichokuwa nacho…akanipiga tena nikaanguka chini na akanivuta bendera yangu tukawa tunanyanganyiana." Amesema Bi Riziki akiongeana mwandishi juzi.

Bi Riziki Omar Chande(42) ni mmoja wa wanawake kadhaa waliojitokeza na kueleza jinsi walivyopigwana kudhalilishwa na polisi.

Riziki Omar Chande(42) mkaazi wa Mfenesini anasema kuwa baada ya kusikia kuna mhadhara Donge, yeye alitoka mapema na kwenda kupanda gari kuelekea Donge kama wenzake lakini baada ya kufika Mahonda jeshi la polisi lilisimamisha msafara na kuwataka watu wote warejee mjini.

Hata hivyo anasema kuwa viongozi wa msafarawaliwataka wasiondoke mpaka viongozi wakuu watakapofika.

Ilikuwa ni katika muda huo huo Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake walifika katika eneo la Mahonda na kutaka jeshi la polisi kuacha kuhatarisha amani kutokana na kitendo chaocha kuwazuiya watu waliokuwa wakielekea Donge kuhudhuria mkutano uliokuwa ufanyike katika Msikiti wa Donge.

Hata hivyo badala ya kuwasikiliza na kujadiliana nao, polisi waliwafukuza kwa mabomu ya machozi na ndipo Masheikh haowalipoingia Msikitini.

Taarifa kutoka eneo latukio zinafahamisha kuwa polisi waliwafuata huko huko Msikitini kuwatawanya kwa mabomu ambapo Sheikh Farid na wenzake waliruka ukuta na kukimbia kwa miguu katika pori kutoka Mahonda kuelekea njia ya Mwangapwani.

Huku nyuma, wakidhani Sheikh Farid yupo ndani ya gari alilokuja nalo, watu wasiofahamika walilifukuza gari hilo na kulipiga risasi ambapo lilipinduka na kuharibikia vibaya.

"Sijui kama walitaka kutuuwa au vipi, lakini bahati mimi sikuwemo katika ile gari ingawa wanadhani kwamba ile gari ni yangu, lakini niseme mimi ile gari sio yangu ila nilipewa kwa kutumia kwa ajili ya shughuli za kuendeleza hizi harakati zetu", alisema Sheikh Farid muda mfupi baada ya kurudi katika hekaheka hizo ambapo walifanya mhadhara wao Mbuyuni baada ya kutokufanikiwa kupenya kwenda Donge.

Akielezea juu yakilichomfika Bi Riziki anasema kuwa kwa vile alikuwa kashikilia bendera, ilikuwa rahisi kwake kufuatwa na polisi.

"Mimi nilikuwa nimekamata bendera yangu polisi alipokuja kunichukua akanikamata mkono ananipeleka kituoni alipofika mbele kuna polisi mwenzake akawambia unampeleka kituo kama BiHarusi, mpige virungu,…yule polisi akajibu kwanini tumpige wakati amekubali kutii amri halali?"

"Mwenzake akasema, haiwezekani hao hawana adabu lazima apigwe, yeye ndio akaanza kunipiga huku akinambia nimpe bendera yangu ya Uamsho mimi nikamwambia nipige lakini bedera yangu sikupi ndio akaendelea kunipigana kunipiga", alisema BiRiziki.

"Wakawa wanatuambia maneno ya ovyo kwamba tutakoma, kwa hivyo yule polisi mmoja akawa anaendelea kunipiga alipokuja polisi mwenzake akawambia unampigia nini huyo wakati yeye amekubali umpeleke kituoni ndipo waliponichukua na kunipiga tena".

Riziki ambaye aliumia sehemu ya jicho baada ya kupigwa kibao na jicho lote kupiga wekundu, anasema kilichomshangaza ni kwamba kila kituo cha polisi alipokwenda alikataliwa kupewa barua ya kwenda kupata matibabu.

"Tunafanywa kama sio raia wa nchi hii tulipokwenda kituo walikataa kutupa barua wakati wanajua hatuwezi kutibiwa kama tumeumia mpaka tupate barua ya polisi, tulipotoka Mahonda tukaja mjini tulikwenda Kituo cha Polisi Mkunazini wakakataa kutupa kibali tukenda Malindi pia wakatwambia nyinyi nendeni tu hukohuko hospitali wambieni madaktari kuwa mmepigwa na polisi …hawakutupa."

Bi Riziki ambaye aliumia mkono na jicho anasema hata walipokwenda hospitali walikataliwa kupewa tiba hadi watakapokwenda na barua ya polisi.

Naye Hafsa Mohammed Mahfoudh (19) mkaazi wa Kinuni, Magogoni anasema katika zahma hizo watu wengi walikimbilia Msikitini na ndipo walipoona Polisi wakiingia Msikitini na kuwapiga wanawake na wanaume na kuwatoa nje huku wakitaka wanawake wote wavuliwe mashungi yao.

"Walikuwa wakisema maneno mabaya mabaya huku wakituvuta mashungi yetu wakitwambia tokeni hapa Waislamu, Waislamu, Waislamu nini, wanafiki wakubwa, na kuna askari wa kike alinivuta sana shungi na kunipiga sana kwa....

Inaendelea
 
Back
Top Bottom