Walitaka kuchinja, lakini....!

Walitaka kuchinja, lakini....!

kabanga

Platinum Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
37,649
Reaction score
19,042
hapa kila mtu anataka ajiokoe...

bull.gif
 
Ukitaka kumchinja ng'ombe halafu akafanikiwa kukurupuka basi wote mliokuwa hapo mtafute pa kwenda hasa yule aliyeshika kisu.
 
Huyo wampeleke Geita wanakogombania kuchinja, najaribu kuwazia jinsi ya kumlaza ili kutafuta uelekeo wa ...
 
Mkeshaji ushawahi kukumbana na hii adhma nini maanake unavyoongea kwa hisia na msisitizo,poleeeeeee kama ulikutana na hicho kivumbi maanake najaribu kupiga picha ila sipati picha ulivyokuwa unaupangua upepo,Haaaahaaaaahaaaaa[joking}
Ukitaka kumchinja ng'ombe halafu akafanikiwa kukurupuka basi wote mliokuwa hapo mtafute pa kwenda hasa yule aliyeshika kisu.
 
Last edited by a moderator:
Mkeshaji ushawahi kukumbana na hii adhma nini maanake unavyoongea kwa hisia na msisitizo,poleeeeeee kama ulikutana na hicho kivumbi maanake najaribu kupiga picha ila sipati picha ulivyokuwa unaupangua upepo,Haaaahaaaaahaaaaa[joking}
Nawashangaa watu wanavyogombea kuchinja. Hawamjui ng'ombe vizuri. Yule ni nyati, tofauti ni kwamba anafugika.
 
Natumai hiyo picha itakuwa imewapa funzo fulani la kuwa na utahadhari na ng'ombe.
Nawashangaa watu wanavyogombea kuchinja. Hawamjui ng'ombe vizuri. Yule ni nyati, tofauti ni kwamba anafugika.
 
Ukitaka kumchinja ng'ombe halafu akafanikiwa kukurupuka basi wote mliokuwa hapo mtafute pa kwenda hasa yule aliyeshika kisu.

Mkeshaji ushawahi kukumbana na hii adhma nini maanake unavyoongea kwa hisia na msisitizo,poleeeeeee kama ulikutana na hicho kivumbi maanake najaribu kupiga picha ila sipati picha ulivyokuwa unaupangua upepo,Haaaahaaaaahaaaaa[joking}

Wakuu msiombe kukutana na dhahama hiyo,kuna siku tuko msibani tunataka kuchinja,basi akakurupuka,ilikuwa mshikemshike almanusra utokee msiba mwingine ndani ya msiba...
 
Haaaaaaahaaaaaaahaaaa nacheka kama vile mazuri naomba tu unisamehe mkuu maanake napiga pichwa kichwani naona watu kibao msibani kila mtu akitafuta njia yake wallahi nashindwa kuhimili kicheko,hata hivo poleni sana mkuu.

Yaani ulivyocheka wewe najikuta na mimi nikicheka nikikumbuka tukio lile,ilikuwa mshikemshike kila mtu akitafuta njia yake hakuna cha wanawake wala wanaume, halafu alikuwa akimwandama jamaa mwenye kisu.Kilichomuokoa jamaa ilikuwa ni kurukia juu ya mpera wa pale kwenye ile nyumba, basi alipomkosa ndio akaanza kuandama kila mtu anayemuona mwisho akatokomea maporini....
 
Daaaaahhhh basi ilikuwa bonge la patashika kuwahi kutokea,sasa mkuu unamaanisha wewe ulikimbia hadi ukawa huna habari kabisa na waifu?Je kama ungeona waifu tu ndo anaandamwa na huyo ngo'mbe ungechukua hatua gani?

Bahati nzuri waifu alikuwa ndani akimfariji mjane, ila ingekuwa waifu ndio kaandamwa wala sijui ingekuwaje maana kumsogelea yule ibilisi ilikuwa ni kubeep kifo....
 
Haaaaaahaaaaahaaaaaa mkuu pole kwa hicho kimbembe ila ingetokea waifu anakimbizwa huo ndio ungekuwa muda wako wa kuproove kuwa unampenda kiasi gani na kama uko tayari kumlinda kwa lolote.Msalimie waifu basi.
Bahati nzuri waifu alikuwa ndani akimfariji mjane, ila ingekuwa waifu ndio kaandamwa wala sijui ingekuwaje maana kumsogelea yule ibilisi ilikuwa ni kubeep kifo....
 
Chezea kitu uhai wewe,kila kiumbe kilicho chini ya jua kila uchao kinaulilia uhai wake usipotee bure.

Ni heri kuwa mlaji wa majani,matunda na mizizi kuliko nyama ya mnyama mwenzako mwenye damu nyekundu kama yetu.
 
Back
Top Bottom