Walipopoteza unyenyekevu na Taifa likaanza kupoteza maadili na ubinafsi ukaanza kuota mizizi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Zipo picha nyingi za ikulu ile ya awamu ya kwanza. Huwa zinatukumbusha mambo mengi, yakiwemo mazuri na mabaya pia. Ni kumbukumbu zinazotunzwa ili angalau ziwaonyesha watoto na wajukuu ule utamaduni mzima wa uongozi wa awamu ya Mwalimu Nyerere ulikuwa vipi.

Ipo picha ya Mwalimu akiendesha baiskeli ndani ya viwanja vya ikulu, na jua linaonekana kuwa juu yake kwa maana ya picha kuwa imepigwa mchana, na nadhani ilikuwa ni mwishoni mwa wiki, labda Jumamosi au Jumapili.

Ipo picha nyingine anaonekana akiwa anapiga ngoma na pembeni yake amekaa nadhani ni Madaraka akiwa mtoto mdogo na kwa muonekano wake hajafikisha hata miaka mitano. Sura ya Mwalimu imejaa tabasamu akifurahia ule upigaji wa ngoma.

Zipo picha za upandaji wa maua, anaonekana hajali kuona suruali yake ikichafuliwa na udongo uliotoka kuchimbwa ili hilo ua liweze kushindiliwa shimoni. Hakujali kwamba pembeni yake yupo mpiga picha na atakwenda kuisafisha na itakuwa ni kumbukumbu ya miaka mingi ijayo, hakuonekana kujali uwepo wa waandishi wachache wa habari zaidi ya kujikita kwa asilimia mia moja katika upandaji wa huo mti.

Mwalimu hakuwa na huu ukuu wa kutembea na kiti cha ikulu na kwenda nacho misibani au kwenda nacho pale Mlimani chuo kikuu kwenye shughuli ya mjadala kati yake na maprofesa wa chuo kikuu!. Mwalimu Nyerere hakujikweza kwa namna yoyote ile.

Nakumbuka pale St Joseph kanisani namna alivyowekwa katikati wakati wa ukaaji. Kushoto na Kulia wakikaa walinzi wake waliovalia kaunda suti. Kwenye shughuli za kijamii alikalia viti alivyovikuta mahali husika tofauti na namna wapambe wa leo hii wanavyochukulia kule kuchafuka kwa dunia ya sasa kama sababu za kumtenga Mkuu wa Nchi na uhalisia unaomzunguka.

Wanadhani wanamlinda Amiri Jeshi kwa kumbebea kiti popote anapokwenda kumbe ni janja yao ya kutaka aione heshima ya bandia wanayoitengeneza ili waanze kufaidika na cheo chake kupitia upambe unaozaliwa baada ya yeye kiongozi kujiona ni wa tofauti.

Mwalimu Nyerere angeweza kuendekeza haya majivuno mengi yanayoambatana na heshima anayopewa kiongozi wa nchi lakini alihakikisha anabakia ndani kabisa ya moyo wake kuwa ni Julius Kambarage Nyerere. Licha ya kuheshimiwa na marais wote wa mataifa ya Afrika, licha ya kuheshimiwa na kuogopwa na wakuu wa mataifa ya Ulaya na Amerika ya Kaskazini aliporudi nyumbani hakutaka kujikweza na kuwakoga jamaa zake mbalimbali.

Marais watatu wa mwisho wa Tanzania ya leo, wamenasa katika mtego wa kuthaminiwa na kuonyesha kwamba wao ni wa tofauti na wote wanaowazunguka. Ndio maana umezaliwa upambe usio na aibu hata kidogo.

Yamezaliwa mambo ya kutaja majina yote ya Mheshimiwa Rais, mambo ya kumsifia mkuu wa nchi hata ndani ya ukumbi wa bunge mahali penye kumruhusu mbunge kutumia haki yake ya kidemokrasia.

Nadhani kama Taifa hatujaenda mbali sana katika kufanya hili kosa la kiuendeshaji, bado tunayo nafasi ya Marais wetu kukumbuka kuwa wao ni sehemu ya kila siku ya maisha yetu sisi, kwamba wamechaguliwa tu kuwa mahali pale lakini ule usisi tulionao na wao wataishi mpaka watakufa nao.
 
Mwalimu alikuwa mzalendo, mwalimu na baba. Muumini wa nguvu ya hoja siyo hoja ya nguvu. Huwezi kuwabomolea wqtu nyumba zao na kuwaacha wengine ati kwasababu walikuchagua!
 
Mwalimu alikuwa mzalendo, mwalimu na baba. Muumini wa nguvu ya hoja siyo hoja ya nguvu. Huwezi kuwabomolea wqtu nyumba zao na kuwaacha wengine ati kwasababu walikuchagua!
Mwalimu angejengea hoja maamuzi yake mpaka yangeeleweka miongoni mwa hao waliobomolewa nyumba zao.

Alikuwa na kipaji cha maneno yenye mantiki tena yenye kueleweka kwa msikilizaji bila ya kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.
 
Mwalimu angejengea hoja maamuzi yake mpaka yangeeleweka miongoni mwa hao waliobomolewa nyumba zao.

Alikuwa na kipaji cha maneno yenye mantiki tena yenye kueleweka kwa msikilizaji bila ya kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.
Yule anayeitwa shujaa angewatisha watu kwamba yye hatishwi. Yaani watu waliokupigia kura leo unawatisha kwa kiburi jeuri ya dola? Ati unapigana vita ya kiuchumi? Ndo utuwekee wqbunge wa chama kimoja? Sasa hiyo vita nani kashinda??
 
Back
Top Bottom