Unyenyekevu ni somo la maisha ya RIP Ali Hassan Mwinyi

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Nilimsika Padre mmoja jumapili tatu zilizopita akihubiri juu ya suala zima la wito, yalikuwa ni mahubiri ya kina ambapo aliamua kufundisha kuhusu wito na michakato yake maishani.

Padre yule alielezea kuwa adui wa ajira nyingi za watu mbalimbali ni ukosefu wa sifa ya unyenyekevu katika maisha yao ya kikazi. Huo huwa ni mwanzo wa kuanguka kwao kutoka katika nafasi za juu na kupotea kabisa.

Nikaoanisha namna Hayati Mwinyi alivyojaliwa unyenyekevu kiasi cha kukubali kujiuzulu cheo chake na miaka kadhaa baadae maisha yakampandisha mpaka akafikia hatua ya cheo cha juu kabisa.

Pengine asingeutanguliza unyenyekevu wakati ule akiwa waziri wa mambo ya ndani asingekuja kupata cheo cha urais, alitengeneza sifa ambayo ilikuja kuwavutia waliomfikiria kuwa anafaa kuwa rais.

Alichukulia ni sehemu ya kazi kwa kutimiza wajibu wake kwa kujiuzulu na wakati huo huo akawa ameiweka wazi nguvu yake nyingi ya kutothamini madaraka mpaka kufikia hatua ya kuutanguliza ubinafsi wake.

Kwamba watu wa usalama wa Taifa walikuwa wakigawa vipigo hovyo tu kwa wananchi wasio na hatia huko kanda ya ziwa mkoa wa Shinyanga ilikuwa ni habari iliyotosha kabisa kuwa sababu ya Waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo kumwandikia barua bosi wake na akajiuzulu cheo hicho.

Hakutaka kuhalalisha uonevu huo kwa kutafuta sababu za kuendelea kushikilia nafasi hiyo ya uwaziri. Ni mara nyingi tu mawaziri wanajifanya hawaoni uovu mwingi unaotokea katika wizara zao ukifanywa na watu walio chini yao.

Unakuwa ni wakati wa mtihani wa kimwili na kiroho unaozikumba nafsi zao na wao wanaona ni heri waitetee ajira yao kumbe kwa kufanya hivyo wanajinyima fursa nyingine nyingi zinazowasubiri siku za mbeleni.

Somo ni moja tu na lina ujumbe wa kudumu kwa maisha ya wote wanaoshikilia vyeo mbalimbali vya kiserikali, unyenyekevu ni kitu muhimu sana. Ni hatua mojawapo inayokwenda pamoja na wito anaoitiwa mtu kwenye maisha yake ya kikazi.

Kukubali kukosa unyenyekevu na kuongozwa na kiburi pamoja na jeuri za aina nyingi ni sawa na kuufungua mlango wa kuanza kuteremka ngazi za kimaisha na kupotea kabisa. Kiburi kimekuwa ni anguko la wengi wenye mamlaka wanaodhani wameshafika hapo walipo.

Miaka 98 ni mingi sana imepungua miwili tu afikishe karne nzima, amenikumbusha namna Baba yake Mfalme Charles wa Uingereza alivyoaga dunia akiwa amebakisha miezi michache tu afikishe karne nzima.

Inawezekana Mzee Mwinyi aliwakwaza wengi wakati wa uhai wake lakini sifa ile ile ya unyenyekevu ilitunyima sisi wananchi aliotuongoza ile nafasi ya kuwafahamu ni kina nani, hakuwa na sababu ya kuutangazia dunia ugomvi wake na wote aliokwazana nao.

Nitamkumbuka Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa unyenyekevu wake, mara nyingi akiwa ni mwingi wa methali na nahau zilizowaacha hoi wasikilizaji huku wakiulizana hapo amemaanisha nini alipotumia maneno hayo!.

Aliwahi kusema suala lenu nitalitilia UPONDO, watu waliokuwa wakimsikiliza wakabaki wamedua wasielewe maana ya upondo ni nini. Upondo ni umuhimu maana yake suala lenu nitalipa umuhimu katika kutafuta suluhisho lake.

Huyo ni hayati Ali Hassan Mwinyi aliyetangulia mbele za haki akiwa amekula chumvi nyingi na mpaka uzeeni mwake alisoma bila ya kuvaa miwani akiwa kasimama mbele ya hadhira.

Mungu na amlaze mahali pema peponi.
 
Unyeyekevu wa hayati Ali Hassan Mwinyi ulikuwa wa kipekee! Apumzike kwa amani.
 
Nikaoanisha namna Hayati Mwinyi alivyojaliwa unyenyekevu kiasi cha kukubali kujiuzulu cheo chake na miaka kadhaa baadae maisha yakampandisha mpaka akafikia hatua ya cheo cha juu kabisa.
Usimpe mwinyi sifa ambazo hakuwanazo.

Aliambiwa na Nyerere aandike barua ya kujiuzulu. The only choice he had was either to resign or be fired which would have had even worse consequences.

Kawawa aliutema uwaziri mkuu kutokana na kashfa ile.

Pascal Mayala anayafahamu vyema haya kwakuwa yalimgusa baba yake.
 
Kila mtu ana vyanzo vyake vya taarifa.
 
Unyenyekevu wa kuuza loliondo na kutaka Magu atawale milele ili tu mambo ya wanawe yanyooke!
Magi alistahili ile heshima aliyopewa na RIP Mwinyi, walishindwa marais wanne wa JMT yeye akawa na ujasiri na uthubutu, ukiondoa udhaifu wa kibinadamu wa hapa na pale nchi ilimstahili sana mbabe JPM hakucheka na kima hata kidogo.
 
Loliondo mpaka leo tumeifanyia kipi cha maana?, na pengine kwa kumilikiwa na waarabu wameweza kuitangaza mara tatu zaidi ya ambavyo ingekaa bure tu.

Anayekwenda huko kwenye mbuga zisizo za asili za uarabuni anapata taarifa kwamba wanyama wametoka Tanzania, hivyo anafunga safari kuja hapa. Sijui kama tunaweza kuona kwa jicho hilo au ni akili zile zile za kichoyo zinazotusumbua.
 
Unyenyekevu wa kuuza Loliondo yetu?
Loliondo bila ya kuuzwa kwa mwarabu sisi wenyewe tumeiongezea tija ipi?. Hulka zile zile za kichoyo na za kimaskini za kusema sisi ni matajiri wakati ni utajiri unaoweza kupatikana ikiwa bado haujapatikana na haijulikani lini na kwa namna gani utakuja upatikane!.
 
Back
Top Bottom