Waliowahi kuacha kazi naomba ushauri

Waliowahi kuacha kazi naomba ushauri

lee jack

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
1,082
Reaction score
1,915
Habari ndugu zangu naomba msaada wa mawazo.

Hivi karibuni nimepata kazi mkoa fulani kazi yenyewe ni kua nadeal na wagen tourist.

Tatizo langu ni kua kuanzia nireport kazini wafanyakazi wenzangu hawanipendi wananisema vibaya chini Kwa chini maneno mengine wanamwambia boss.

Jambo lingine ni kua nikifanya kosa linakuzwa linakua kubwa unnecessary yaani Sina hata miezi sita lakini kazi imekuwa chungu kwangu.

Uamuzi ninaotaka kuchukua ni kuresign.

Msaada ndugu zangu.
 
Habar ndugu zangu naomba msaada wa mawazo
Hivi karibuni nimepata kazi mkoa fulani kazi yenyewe ni kua nadeal na wagen tourist
Tatizo langu ni kua kuanzia nireport kazini wafanyakazi wenzangu hawanipendi wananisema vibaya chini Kwa chini maneno mengine wanamwambia boss.
Jambo lingine ni kua nikifanya kosa linakuzwa linakua kubwa unnecessary yaani Sina hata miezi sita lakini kazi imekua chungu kwangu
Uamuzi ninaotaka kuchukua ni kuresign
Msaada ndugu zangu
Kwanini wakuseme,una tabia mbaya au wanakuonea wivu?

Unataka kuacha kazi kwakuwa watu wanakusema?

Nina wasiwasi na Emotional intelligence yako!!

Kwa ufupi ni kwamba Mtu hakimbii matatizo anapambana nayo.
 
Mimi ni ke
Kazi ya muhindi
Kabla nilikua nafanya kazi tours

Pole sana, Bocy Muhindi ni mwepesi kupokea Majungu sana, bila hata kutafuta ukweli.

Kama inakulipa sana sana, vumilia kwa malengo, ila Kama inakuzalilisha utu wako, achana nayo.

Majungu na fitina vinamalizwa na ukimya, kuchapa kazi zako vizuri na utulivu, na kutokuwa na makundi.

Kama lalamiko lako ni majungu tu na kuchongewa kwa bosy, hakuna uzalilishaji, be strong, stay, boresha character zako.

Wewe mwenyewe, maana unajua una saving kiasi gani, utaishije baada ya kazi, na mambo mengine unajua zaidi.

Usitafute ujasiri wa kuacha kazi toka kwa watu, waulize tu wa kushauri, ila ujasiri wa kuacha kazi hakikisha ni wakwako, na umeshawishika upo tayari ku face challenges.
 
Nimefanya kazi sehemu yenye fitina na majungu kwa muda wa miaka miwili na nikaondoka baada ya kupata kazi sehemu nyingine

Kitu cha msingi jikite zaidi kwenye job description yako usiende nje ya hapo,wahi kwa wakati toka kazini kwa wakati.

Fanya kazi yako vizuri,hakuna boss atataka kufukuza mfanyakazi mzuri.
Usiongee sana,usiingilie mambo yaliyo nje ya kazi yako.

Ukifanya hivyo hakuna neno wala ugombanishi utakaokusumbua
 
Kama una Tabia mbaya acha hiyo Tabia mbaya USIACHE kazi,
Maswala ya kusemwa yapo Sana , na yapo kokote
We endelea hapo hapo kati ya wafanyakazi huwez kukuta wote wanakusema Kuna m1 kati ya 30 atakua na roho nzuri huyo ongea vzr ,
Atakupa mazuri yako na mabaya yako
Mimi nahisi ana tabia ambazo sio nzuri na hapendi kubadilika,mtu hawezi kuacha kazi kisa kusemwa vibaya,never!
 
JF msimseme sana huyu kijana. Atakimbilia Facebook kusema JF wananinanga, nataka kufunga account yangu.

Anyway, kuna msemo maarufu usemao 'Kwenye riziki hapakosi fitina'. Hata uende wapi, utakutana tu na maneno ya Walimwengu. Utatoka hapo kwa Kanji, utaenda kwa Wabongo nako dawa ni ile ile.

Vumilia mpendwa, kama kuna upuuzi unaufanya uache. Usipende pia kuipa nguvu hasi ikutawale ndani ya nafsi yako.

Acha kazi baada ya kupata majukumu mengine. Kila la kheri.
 
Kazi nzuri ni ile uliojiajiri; hizi zingine huwa ni mateso tu, sema watu wanavumilia kwa sababu hawana mbadala.
Fanya kazi yako kitaaluma, jikite kwenye kuongeza mapato kwenye kampuni; fanya tathmini tangu umeajiriwa hapo, kuna mchango gani wa kiuchumi/mapato umeiwezesha kampuni.
Hakuna tajiri anayeweza kumfukuzisha kazi 'potential worker', kwa kusikiliza maneno ya waswahili.
Debe tupu huwa haliachi kutika, wacha waseme we piga kazi, kazi yako ndio ikutangaze.​
 
Dah. Pole sana. Mie nilikaa mkoa fulani miezi saba nikakimbia mwenyewe.
maneno yalikuwa mengi. Mara ooh, sijui nawataka wafanyakazi, wakati kichwani kwangu apo nawaza matofali tu. Mshahara utoke niingie site. Hiyo hoja ya kuwataka wafanyakazi wala haikuwepo kichwani kwangu. Kichwani kwangu mie nilikuwa nawaza matofali tu 😀😀😀
Niliwaachia brand, wakakaa nayo miezi mitatu tu brand ikafa. Wakanyang'anywa maana niliowaachia walishindwa kuiendesha.
Cha muhimu, weka pamba masikioni. Usiache kazi. Subiri mpaka ufukuzwe.
Cha kufanya switch into 'quiet quiting' mode.
Kama huelewi, google kuhusu 'quiet quiting'...
 
Umechafuliwa nyota yako mkuu. Kwa ufupi una kimavi. Unaweza kusafisha kea njia moja kati ya mbili;

1. Kwenda kwa mganga mwenye uwezo mkubwa

2. Kuongoka na kumkubali Yesu Kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako( njia hii ni nzuri na ni ya uhakika zaidi).
 
Back
Top Bottom