Waliotumbuliwa wadai wana siri nzito

Waliotumbuliwa wadai wana siri nzito

Mahakama zetu zishaingiliwa wala wasiende huko watafute alternative means
 
Si wana mitaji ya kutosha? Waende wakajiajiri bwana, mbona mwenzao Rutengwe ameshajiajiri wala hatumsikii kulialia tena?
 
View attachment 454059

Wasema wataiburuza serikali makamani.

Wadai serikali inawaonea na wapo na siri nzito na wako tayari kuzitoa mahakamani.
mimi nashangaa sana hawa wateule wa Rais. mimi nilidhani suala la Ombeni Sefue lilikuwa ni somo tosha kwao?

kweli wacha tu Watanzania tutukanwe matusi yote tunayoweza kutukanwa...dah!
 
Sheria zinamtaja raisi ni zaidi ya mwajiri, Zinamtaja yeye kama mamlaka ya juu zaidi ya kinidhamu kwenye utumishi soma section 35(1) ya public services regulation wa umma kwa hiyo sheria imempa uwezo wa kutumbua anavyojisikia yeye,Lakini pia wateule wake wakitumbuliwa na mamlaka zingine za kinidhamu wanaweza ku appeal kwake na akawarejesha kazini S.60() public services regulation.
I can bet, ni wachache sana hata miongoni mwa waliotumbuliwa wanalijua hilo. Mtu akiteuliwa akapewa mkataba, anaangalia palipoandikwa kiasi cha mshahara, sehemu ya kuandika jina na kuweka sahihi, basi. Sehemu zingine si muhimu hadi limtokee (La kutumbuliwa kwa mfano).
 
Mkuu fikiria kidogo. Wangezitolea wapi hizo siri.. Assume umefukuzwa na HUNA mamlaka ya kukaa ofisini wala kuita Mwandishi habari.. Anyway back to the topic hata WAkilalamika bado rais kisheria inafafanua yeye ndio mwajiri.. Hawatafanikiwa

Mfanao.
Akienda mahakamani akasema nimefukuzwa baada ya kukataa kumtafutia ulaji Ndugu wa alieniteua na akatoa ushahidi imara wenye vilelezo kama vi-memo huoni kuna tatizo.
 
Walivyokuwa wanaiba na kujenga maghorofa nani alikuwa anawapandisha hadhi siwalikuwa wanatudharau na kututukana.
 
Hapo ni kwamba anapotengua kwa matakwa yake,hapo hakuna shida. Shida INA kuja pale anapokuharibia public image ya kukwamnia labda wewe mwezi, ulikosea, au sababu yoyote inayokushushia hadhi mbele ya jamii. Unayohaki ya kwenda mahakamani kuweka historian sawa
Hiyo public image ndo kitu gani bana mbele ya mali ya umma hawa siyo wa kutetea hata kidogo.
 
ahha ahaha, walikuwa wanatwambia vijana mkajiajili
Hahaa tena wao wanamitaji tayari. Waje kujiajiri tu. Hawa ndio walikuwa wanasema vijana wanafanya nini mjini huko vijijini mapori kibao wakalime, waje mtaani tukalime wote.
 
wafa maji hawaishi kutapatapa...................................................mpaka wanakufa........
 
Tatzo la viongoz wetu wengi hawana akili kutokana na kuwa kwenye system ivo cc tuliopo nje ya system wanatuona hatuna msaada wowote ule kwao but baada ya kutumbuliwa ndio wanataka kumwaga hizo sili hazarani je kpnd wapo kwny ssytm walikuwa wap?
 
Common sense: wengi walitenguliwa nafasi zao kwa kudhalilishwa, hivyo kuondoa dhana ya kuw Ni nafasi za kuteuliwa tu, hawana haki ya kushtaki.
Waliambiw Wezi, kama wana ushahidi kuthibitisha hawakua na Doa, lazima waliowasema namkuwafhalilisha waende mahakamani tu.
Kama angewaondoa kwenye nafasi zao bila tuhuma,hapo panaweza pasiwe na kesi.
 
Hii tabia ya chuki kwa watumishi wa umma inatoka wapi!!

Watu tumekuwa ma vampire tunapenda sana damu (balaa ziwapate ndugu zetu)!!

Tumekuwa kama yale majini ya ajali!! Isipotokea ajali yanakuwa na kiu balaa!! Ikitolea ajali ikaua yanafanya sherehe!!

Nani kasema kila bosi wa taasisi ya uma ni mwizi!!!
Wizi ni tabia haijalishi cheo.

Sasa hivi haya watu wakisikia kuna waziri kafukuzwa wanashangilia, kuna mkurugenzi kafukuzwa, wanafurahia, kuna afisa kilimo, daktari, mwalimu, hata dereva kafukuzwa wanashangilia!! Bila hata ya kutaka kujua ukweli wa mambo!

Tumekuwa ma vampire tunaombea wenzetu ajali, balaa na hata vifo alafu tunashangilia tunafurahia!

Naomba tukemee hii tabia, hata Mungu hapendi.

Ukisikia mtuhumiwa kahukumiwa kifo usishangilie!! Hujui undani wake!

Dunia hii ina mengi, balaa leo liko kwa mwingine kesho kwako au kwangu!!

Tumche Mungu na Tupendane. Sisi ni ndugu!!!

Upendo ukitawala kwa watu wote viongozi na wananchi baraka zitakuwepo!!
 
Tatzo la viongoz wetu wengi hawana akili kutokana na kuwa kwenye system ivo cc tuliopo nje ya system wanatuona hatuna msaada wowote ule kwao but baada ya kutumbuliwa ndio wanataka kumwaga hizo sili hazarani je kpnd wapo kwny ssytm walikuwa wap?
Ndio hapo udhangae sasa.
 
Mkuu fikiria kidogo. Wangezitolea wapi hizo siri.. Assume umefukuzwa na HUNA mamlaka ya kukaa ofisini wala kuita Mwandishi habari.. Anyway back to the topic hata WAkilalamika bado rais kisheria inafafanua yeye ndio mwajiri.. Hawatafanikiwa

Tatizo TZ hatuko energetic,hatuna munkari sijui kwakua hatuvuti bangi vyakutosha na kunywa visusio ili tuwe na hasira. Yaani mtu anaonewa lkn anatuliaaa hata kusema nimeonewa hawezi,mtu anang'olewa meno kimyaa,kucha kimyaaa,anasingiziwa wizi na ufisadi kimyaaa...dah!! Tunakasirika tukichkuliwa Wake tuu

Falsafa ya Karl Marx bado inadumu. Alipokuwa anasema "workers unite, you have nothing to loose except your unity" alikuwa na maana kubwa. Katika muktadha wa wafanyakazi waliokuwa wanatumikishwa kufanya kazi kwenye viwanda vilivyomilikiwa na mabwenyenye karne ya 19, walikuwa ni watu ambao hawakuwa na kitu chochote cha kumiliki (they had nothing to own). Hawakuwa na ardhi wala kiwanja, hawakuwa na elimu, hawakuwa na ajira. Ili waishi ilibidi ahakikishe kila siku anaingia kufanya kazi kwa bosi. Hata huyo mke hana.

Katika muktadha wa Tanzania ya leo, watu tumekuwa kama wajinga, kama kondoo apelekwaye machinjoni kwa sababu we have something to own. Mtu ana ajira, mwisho wa mwezi anapata salary. Ana shamba, ana nyumba, ana kiwanja, ana familia etc. Akipiga piga kelele, either anaitwa anapewa bahasha au cheo anatulia (rejea akina Polepope, Mwakyembe, na wengine). Wengine ndo hivyo mtu anapotea kimya kimya na hatusemi neno, kwa sababu tunaogopa kupoteza kitu tulicho nacho. Utamwambia mtu tukaandamane, anawaza nikivunjwa mguu, nikifa nani atatunza familia yetu. Na huo ndo uchawi mkubwa kuliko wote (Intimidation)
 
Ndg yangu usiseme hivy
Hiyo public image ndo kitu gani bana mbele ya mali ya umma hawa siyo wa kutetea hata kidogo.
Ndugu yangu usiseme hivyo, ktk maswala ya umma unaweza kusingiziwa kitu hadi ukafukuzwa lkn ukifwta sheria unakuta hakuna sehemu uliyokosea.
Unaweza sema hivyo labda hayajakukuta lkn kwa watu waliyowakuta wanajua.
Binadamu wote si sawa na hatupendani
 
Ndg yangu usiseme hivy

Ndugu yangu usiseme hivyo, ktk maswala ya umma unaweza kusingiziwa kitu hadi ukafukuzwa lkn ukifwta sheria unakuta hakuna sehemu uliyokosea.
Unaweza sema hivyo labda hayajakukuta lkn kwa watu waliyowakuta wanajua.
Binadamu wote si sawa na hatupendani
Sawa lakini ukifuatilia wote waliopigwa chini wamehusika kwa ubadhilifu, kwanza wote ni matajiri wa kupindukia hizo hela wametoa wapi mzee.
 
Back
Top Bottom