Siri Nzito? hahaha, nacheka kwa dharau tu, yaan mnatishia nyau, hivi mnajua maana ya serikali?
Kwanza mshukuruni JPM tu maana hatoi sababu za kutumbua mbali na ile ya Kitwanga ambayo ilikuwa ni lazima aiseme, na ile ya Board ya TRA, wengine hajasema.
Mkapa kipindi chake alikuwa anasema hivi....
"Rais amemstaafisha *** kwa manufaa ya Umma" hayo manufaa ya Umma nani aliyewahi kuyahoji?
Rais kumteua mtu ni discretion yake, na kumuondoa ni discretion yake, sasa unahoji nini mahakamani? unahoji kutenguliwa kwa nafasi yako au stahiki zako baada ya kutenguliwa?
Kwanza, Rais akiamua kutuma team ikuchunguze toka umeanza kazi katika Taasisi husika hadi unatenguliwa uliyokuwa unayafanya au uliyofanya, na maendeleo yako na kipato chako, na kama kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi au madaraka, ndugu yangu umekwisha, tena kwa hawa Watanzania waliokuwa wanakula cake enzi za JK. utawakamata wengi sana, waambieni watulie tu, wajiajili tu, wadau stahiki zao tu wapewe. ..
Hii ndio Afrika Bwana, kama huamini hii ni Afrika, Nyanyua kichwa chako kwa watawala uone....