Waliotia nia CCM wapo wezi. Wananchi semeni tusiongozwe na mijizi; ilishaiba sana, sasa yatosha

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Ama hakika umri wangu umeenda, ama hakika nimezeeka.

Narajea tena nimezeeka ebo! Kumbe sijazeeka bhana ila vijana wengi wamejitokeza kutia nia na ndio maana kwa ujana tunao lingana wameamua kutia nia.

Vijana wenzangu walio tia nia kupitia CCM wengi tulisoma nao shule ZA msingi, sekondari na vyuo vikuu.

Je, tusiotia nia tupo tayari kuwasema na kuusema ukweli dhidi hao watia nia dhidi ya tabia wetu mwaka huu?

Je, tunajua madhara ya kutowasema waliotia nia ili jamii zetu ziwaajue?

Mfano mimi niliwai kuwa Waziri wa Habari chuo kikuu fulani. Aliyekuwa waziri mkuu katika serikali yetu enzi hizo alipata alishutumiwa kwa kuiba kiasi kikubwa cha fedha hizo enzi hizo hapo chuo kikuu na baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika kweli aliiba na akasimamishwa uongozi, na nijuavyo mimi hata cheti cha chuo kikuu hakukipta kwa wakati kisa wizi.

Leo hii ni mtia nia kupitia Chama cha Mapinduzi; hii ni inshara tosha hata majambazi yanatia nia kugombea uongozi kupitia CCM na Rais hata tuseme ili majambazi hayo yapate fursa ya kutuongoza.

Waliotangaza nia CCM, majambazi ni wengi. Wananchi tuseme jamani.
 
Back
Top Bottom