Waliotangazwa washindi kwenye kilichoitwa uchunguzi mkuu wa 2025, naona ni watu wasio na furaha na wanajihisi kukosa political legitimacy

Waliotangazwa washindi kwenye kilichoitwa uchunguzi mkuu wa 2025, naona ni watu wasio na furaha na wanajihisi kukosa political legitimacy

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,141
Reaction score
162,536
Huu ndio ukweli na hata wao wanaujia, ila tu wameshindwa kupambana na roho za ubinafsi na tamaa ya madaraka.

Yaani kwa sasa hata kumita mtu sijui Mheshimiwa Raisi, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu au sijui waziri fulani, mbunge au diwani fulani, unaona kabisa unakosea na hustahili kumuita hivyo(nafasi inakukatalia kabisa).

Miaka ya nyuma, mtu akishinda uchaguzi, mshindi anajitokeza kushukuru wapiga kura huku wananchi nao wakiwa wamehamasika na kutamba kama wanavyotambiana mashabiki wa Simba na Yanga pale timu moja inaposhinda au kufanya vizuri.

Leo hii hata hamasa ya soka imeshuka na mfano mzuri ni hamasa ya mechi za kimataifa zilizochezwa mwishoni mwa wiki hili ambapo timu kongwe za Simba na Yanga zilishiriki huku hamasa katika michezo hiyo ikiwa chini kabisa.

Ukweli ni kwamba, watawala wamepoteza political legitimacy na wananchi wanajihisi kutawaluwa na watu wasio na uhalali kabisa.

Taifa limepooza huku vifo vilivyotokana na mauji ya kikatili, ndio vikaongeza machungu ya uchaguzi usio wa haki uliozaa balaa lote hili katika nchi yetu .
 
Back
Top Bottom