Shaffin Simbamwene
JF-Expert Member
- Nov 16, 2008
- 2,156
- 1,521
Mv maendeleo na Canadian sprit zilibamba sana enzi hizo afu bus German Voyage siku mbili ndio unafika.Naliona bweni langu la Jamhuri pale. Niliishi Cell D. Huo uwanja wa basketball upo karibu na town way pale Kwa Mbunge Kanjibai njia ya kuelekea Coast.
Miaka hiyo ilikuwa usafiri wa uhakika kwenda Mtwara ni meli tu. Barabara haikupitika kirahisi.
Mwalimu Mnelamwana alishawahi kunipa adhabu ya kung'oa visiki kule forest kama unaenda chuo Cha ualimu ufundi. Alifanya kurusha jiwe na kusema mwisho wa adhabu yako ni pale na ukimaliza adhabu uje kuripoti. Sikwenda kuripoti maana ilikuwa ni mtego wake kwani ukienda kuripoti huwa anakuja kukagua na kurusha Tena jiwe huku akisema mwisho wa adhabu yako sio hapa bali ni pale (anarusha jiwe upya).
All in all, hapa nilijifunza discipline kwenye maisha. Kwa sasa Mimi ni Civil Engineer.
Namkumbuka sana Mrs Kilimba yule muuguzi alikuwa poa sana.
Mnelamwana yule mhuni zilikuwa hazipandi hadi nahamia Moshi Tech kwa Mpande.
Ekoni wa Ekoni pamoja na Ngari walikuwa poa sana bila kumsahau Mshkaji Kisuu