Waliosimamishwa UONGOZI na MBOWE, wahamia CCM

Waliosimamishwa UONGOZI na MBOWE, wahamia CCM

Kama nitakuwa sahihi,sijaona viongozi wa CHADEMA waliohamia CCM kwenye habari hii.
 
Katika tukio lingine la hivi karibuni lenye kudhihirisha kasi ya CCM kuibomoa CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime, kimevuna wanachama wapya 800 ambao awali walikuwa ni wanachama na wafuasi wa CHADEMA.

Wanachama hao ambao idadi yao imetimia takriban 800 wamekuwa wakiingia CCM kwa muda wa wiki tatu mfululizo tangu kumalizika kwa ziara ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA katika wilaya ya Tarime, ambapo wanachama zaidi ya 600 walijiunga wiki mbili zilizopita na 256 walijiunga na CCM jumanne iliyopita katika mikutano ya hadhara.

Mikutano hiyo ya hadhara ambayo inaendelea wilayani humo, jumanne ya juzi ilifanyika katika uwanja wa kituo cha Sirari, ukihutubiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Rashid Bogomba, ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa eneo hilo na katika mkutano huo ndipo wanachama wengine 256 waliporudisha kadi za chadema na kujiunga na CCM na kutimiza idadi ya wanachama hao wapya kutoka chadema kutimia zaidi ya 800.

Wanachama hao wamedaiwa kuhamia CCM baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa , Freeman Mbowe kuwasimamisha uongozi viongozi wa CHADEMA wa wilaya hiyo ya tarime, ambao waliamua kuhamia CCM wakifuatwa na wafuasi wao kutoka katika chama hicho.

Source: Uhuru_ukurasa wa 8

Do hawa Wasaghane
Hawana cha kuandika,hivi hao walioondoka ni wakurya kweli au ni watu wa tanga

Kwa akili yako hakuna waliotoka chama kingine au ambao hawakuwa na vyama yaani woote wametoka Chadema? We Farasi kama jina lako hata kama ni mapenzi yako kwa Ccm umezidisha ndugu yangu duh
 
Nafuu wameondoka na bado mtaondoka wengi sana.
Ukisimamishwa uongozi unahamia chama kingine? Kwahiyo wewe farasi unataka kutuambia hawa watu walifuata uongozi CDM wamesimamishwa wakakimbia?
Kawapeni uongozi huko CCM.
 
mbona sababu imewekwa wazi kuwa ni maamuzi ya kukurupuka ya mbowe,, hili la MONEY limetoka wapi mwanawane..?????

Nakumbuka Zitto alisema haamini katika sera ya kuhamahama vyama.

Mimi naamini hawa wanaohama vyama sio waleta mabadiliko ya kweli na usishangae hata kwenye kupiga kura hawa ndo ambao kura zao huwa zinaharibika. Maana anafika pale kwenye form ya kupigia kura ila nafsi na ubongo wake havielewani.
Wacha waende tu maana wengi wao walitokea CCM kama Wassira. Huwezi kuwaamini tena watu wa jinsi hii
 
weka ushahidi vinginevyo itakuwa ni sawa na debe tupu.

Ushahidi ndo huu mkuu, Misukule mtabadili badili ID hadi lini ?

Join Date : 8th April 2013
Posts : 133
Rep Power : 327
Likes Received13
Likes Given5
 
Katika tukio lingine la hivi karibuni lenye kudhihirisha kasi ya CCM kuibomoa CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime, kimevuna wanachama wapya 800 ambao awali walikuwa ni wanachama na wafuasi wa CHADEMA.

Wanachama hao ambao idadi yao imetimia takriban 800 wamekuwa wakiingia CCM kwa muda wa wiki tatu mfululizo tangu kumalizika kwa ziara ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA katika wilaya ya Tarime, ambapo wanachama zaidi ya 600 walijiunga wiki mbili zilizopita na 256 walijiunga na CCM jumanne iliyopita katika mikutano ya hadhara.

Mikutano hiyo ya hadhara ambayo inaendelea wilayani humo, jumanne ya juzi ilifanyika katika uwanja wa kituo cha Sirari, ukihutubiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Rashid Bogomba, ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa eneo hilo na katika mkutano huo ndipo wanachama wengine 256 waliporudisha kadi za chadema na kujiunga na CCM na kutimiza idadi ya wanachama hao wapya kutoka chadema kutimia zaidi ya 800.

Wanachama hao wamedaiwa kuhamia CCM baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa , Freeman Mbowe kuwasimamisha uongozi viongozi wa CHADEMA wa wilaya hiyo ya tarime, ambao waliamua kuhamia CCM wakifuatwa na wafuasi wao kutoka katika chama hicho.

Source: Uhuru_ukurasa wa 8

Chanzo cha habari UHURU. Halafu muandishi wa habari hii Nchemba. Mbona gazeti hili hili halikuandika lile lundo la kadi za CCM alizo kabidhiwa Mwigulu? Ngoja nikajipumzishe kwa RAHA zangu!! Wala sina preasure miye!!
 
Kama kuna chama cha siasa ambacho kwa sasa kimepoteza kabisa muelekeo basi chama hiko ni Chadema.,kimepata mmomonyoko kuanzia uongozi ngazi yake ya juu kabisa ya taifa kisha mmomonyoko huo unaendelea katika ngazi nyingine za mikoa na wilaya.

Bahati mbaya wanachama wa chama hiki hawajielewi, hawazingatii wala hawafikiri sawasawa.,wanafuata uongozi wa ki-imla hawahoji wala hawaulizi.

Chama kinaongozwa na watu wa hovyo, na ni watu wa hovyo tu watakifuata.
 
Uhuru!! Kwani inchi hii inahuru? Sisomagi uchafu na ninaomba wewe ulie leta habari za magazeti ya ajabu ukome,kwani huu sio muda wa propo ganda ni muda wakazi ukome kutuletea magazeti ya choo.naogopa bani ila ukome kutusomesha magazeti yasio na uchungu na yanayo tokea inchini mwetu.koma basi au?
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Kama kweli ccm inaweza kuvuna wanachama 50 katika mkutano mmoja tu wilayani Tarime hata kama wamewanunua basi wangetuwekea picha. Lakini hizi kalinyekalinye za gazeti la uhuru ni katika jitihada za kujifurahisha na kuwadanganya wasioifahamu vizuri Tarime.

Kama ingekuwa kweli tungeshajionea kwa macho kupitia runinga ya kada wao, startv.
 
  • Thanks
Reactions: ESI
CCM na kufeli kwa wanafunzi..
Mulugo hajui Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unajumuisha nchi gani...
Mtoa mada hajui 256 + 600 =856 yeye anasema takribani 800 (yaani hata mia nane hawajafika,just approximation) wakati figures halisi anazo!
Okay...nendeni mkajiunge na hayo madudu mje mchekwe na vizazi vyenu...
Mwenzenu Kikwete atakumbukwa kama Chief Mangungo.....
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Uh hili gazeti bado lipo na linasomwa na watz? Kazi kweli kweli, labda kama ni wahariri na ...
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Uhuru sio authentic paper mtu unaweza kuliamini. Kwao propaganda ndio habari!
 
  • Thanks
Reactions: ESI
chanja mbuga chama tawala, ndio kazi iliyobaki...wao maneno sisi vitendo

Wewe kilaza si ndio wewe umeleta uzi kuwa bunge halitaoneshwa live? Wewe ni mtu wa magamba itakuwaje ugeuke ulete propaganda za kuwaumbua magamba wenzio wakina Makinda? Hujalipwa posho nini?
 
Back
Top Bottom