Waliosimamishwa UONGOZI na MBOWE, wahamia CCM

Waliosimamishwa UONGOZI na MBOWE, wahamia CCM

Sijakusoma!!!,Kwa uelewa wako hii movie anayejidanganya na kujipa tumaini hewa ni CHADEMA sio CCM¿¿?Kalagabhaho!!!:msela::msela::fear:
 
Katika tukio lingine la hivi karibuni lenye kudhihirisha kasi ya CCM kuibomoa CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime, kimevuna wanachama wapya 800 ambao awali walikuwa ni wanachama na wafuasi wa CHADEMA.

Wanachama hao ambao idadi yao imetimia takriban 800 wamekuwa wakiingia CCM kwa muda wa wiki tatu mfululizo tangu kumalizika kwa ziara ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA katika wilaya ya Tarime, ambapo wanachama zaidi ya 600 walijiunga wiki mbili zilizopita na 256 walijiunga na CCM jumanne iliyopita katika mikutano ya hadhara.

Mikutano hiyo ya hadhara ambayo inaendelea wilayani humo, jumanne ya juzi ilifanyika katika uwanja wa kituo cha Sirari, ukihutubiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Rashid Bogomba, ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa eneo hilo na katika mkutano huo ndipo wanachama wengine 256 waliporudisha kadi za chadema na kujiunga na CCM na kutimiza idadi ya wanachama hao wapya kutoka chadema kutimia zaidi ya 800.

Wanachama hao wamedaiwa kuhamia CCM baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa , Freeman Mbowe kuwasimamisha uongozi viongozi wa CHADEMA wa wilaya hiyo ya tarime, ambao waliamua kuhamia CCM wakifuatwa na wafuasi wao kutoka katika chama hicho.

Source: Uhuru_ukurasa wa 8

Mamluki hawatapata nafasi katika safari hii ya ukombozi wa Taifa! Si kila anayeutamka cdm ana nia ya dhati wengine wanaingia kusoma upepo tu! Hakika hakuna kukata tamaa cdm mkijua safari ya mamba hata kenge wapo!! Msihesabu idadi ya wanao ingia na kuondoka, bali hesabuni nafsi zile zilizotayari katka ukombozi wa fikra na mageuzi ya kweli
 
hawa jamaa wanaohama vyama hawafai kuwa viongozi maana wanatakiwa wapambane na matatizo na sio kuyakimbia hayo matatizo.hawa ndo sometimes wanakimbia familia kwa kwenda kutafuta maisha mteremko

Kama vile Babu Slaa. Hawafai hata kidogo.
 
Katika tukio lingine la hivi karibuni lenye kudhihirisha kasi ya CCM kuibomoa CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tarime, kimevuna wanachama wapya 800 ambao awali walikuwa ni wanachama na wafuasi wa CHADEMA.

Wanachama hao wamedaiwa kuhamia CCM baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa , Freeman Mbowe kuwasimamisha uongozi viongozi wa CHADEMA wa wilaya hiyo ya tarime, ambao waliamua kuhamia CCM wakifuatwa na wafuasi wao kutoka katika chama hicho.

Source: Uhuru_ukurasa wa 8
Ndugu yangu naomba unisadie mwenyewe ukianza kwa kuunganisha hapo kwenye RED na BLUE! Hivi hapo WAMEVUNA au WAMEOKOTA?
 
Kama taarifa hii ni ya kweli basi mpaka kufikia 2015 Chadema wanaweza wasiwe na kiti cha Ubunge hata kimoja. Haiwezekani kila kukicha tupate taarifa za watu kukihama chama hiko na kisha tuendelee kujipa imani kuwa kipo salama na kitavuka bahari pamoja na mawimbi haya mazito ambayo chombo chao kimeshaonyesha udhaifu wa kuyakabili.

Kama chanzo chenyewe ni UHURU unategemea nini?
 
Source of information, uhuru news peper;
ipo kazi hapo!!!
Hivi uhuru inatoka siku gani vile kwa wiki, na linauzwa bei gani vile?
Kama una mtu anafanya serikalini muulize maana govt ndio reliable market kwa gazeti hilo la chama tawala.
 
Tunaomba uthibitisho wa uhakika sio unasema tu wanachama 800 onyesha picha, hasa wakati wanarudisha kama ambavyo CHADEMA ilifanya kuleee LOLIONDO
Tukio na hatimaye Kifo cha Chacha Wangwe ndi unataka uthibitishio huo?
Chadema kupoteza Jimbo hilo ndio uthibitisho huo
au kujazana watu ndio uthibitisho mliouzoea
subirini Ballot Box 2015 maana mapovu na matusi sio kujaza jukwaa kuwa kila kitu ni kibaya kuonewa nk
 
Uhuru ni gazeti linalomilikiwa na c c m. Na huu ni uwongo mwendelezo wa yalee ya akina mwigulu na dondoo za nape
 
Back
Top Bottom