#COVID19 Ummy Mwalimu: UVIKO-19 bado upo, ni muhimu kupata chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Waziri Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa UVIKO19 bado upo na namna nzuri ya kuepuka maradhi hayo ni kupata chanjo hivyo ametoa wito kwa wananchi kupata chanjo ambazo zinaendelea kugawiwa bure.

Waziri amesema hayo katika ziara ya Rais Samia Mkoani Njombe ambapo amesema siku ya Jumamosi, Agost 13 kutakuwa na tamasha kubwa ambapo wanamuziki wote watakuwepo mkoani Njombe kuhamasisha utoaji chanjo.

Waziri Ummy amesema hadi sasa watanzania milioni 15.5 wamepata chanjo ya UVIKO 19
 
Mwambie achanje mwenyewe mara nyingi iwezekananvyo ili asife mapema!

Ila sisi wabishi kamwe hatuchanji hiyo chanjo isiyo na manufaa yoyote yale mwilini.
 
Waziri Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa UVIKO19 bado upo na namna nzuri ya kuepuka maradhi hayo ni kupata chanjo hivyo ametoa wito kwa wananchi kupata chanjo ambazo zinaendelea kugawiwa bure.

Waziri amesema hayo katika ziara ya Rais Samia Mkoani Njombe ambapo amesema siku ya Jumamosi, Agost 13 kutakuwa na tamasha kubwa ambapo wanamuziki wote watakuwepo mkoani Njombe kuhamasisha utoaji chanjo.

Waziri Ummy amesema hadi sasa watanzania milioni 15.5 wamepata chanjo ya UVIKO 19
Si achanje tu yeye kwa niaba yetu wenye nchi jamani!!
 
Back
Top Bottom