Waliomo na Wasiokuwemo

Waliomo na Wasiokuwemo

NNYAMBALA

Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
85
Reaction score
12
Kuna Mkulima ktk kijiji fulani alikuwa anasumbuliwa sana na panya, ili kujikwamua na tatizo hilo,akaamua kutega mtego na badala ya panya kunaswa, akanaswa nyoka, mara kuku akatokea na nyoka akamuomba amsaidie kutegua, kuku akakataa, akaja mbuzi naye akakataa kumsaidia, mara akatokea ng'ombe alipoombwa msaada na nyoka naye akakataa. Mara Mkulima akafika akidhani aliyekamatwa ni panya ile kushika tu mtego akang'atwa na nyoka. Sumu ikaanza kusambaa mwilini na kuanza kuugua, Mke wake akamkamata kuku akachinjwa ili kiwe kitoweo cha mgonjwa, baadaye,Ndugu wakaja kumuangalia ikabidi mbuzi achinjwe kwa ajili ya kitoweo cha Wageni, mara Mkulima akafariki na watu wengi wakaja kwenye mazishi ikabidi Ng'ombe achinjwe kwa ajili ya kitoweo.
 
kama wangelimtegua isingefikia hadi wao kuchinjwa
 
hata kama wangemtegua ipo siku tu wangejiskia kuchinja mifugo yao
 
Back
Top Bottom