Waliokuwa wanamshangilia na kumsifu anayejiita 'Mdude Chadema' wako wapi?

Mkuu, kama sikosei, kwa bandiko hili, umejitanabahisha kuwa wewe binafsi ni msemaji wa “wenye siasa”. Sijui ni kina nani hao. Utaeleza ukipenda.

Halafu, ulichoandika hapa ni kama unatufikishia ONYO lao kwetu kwamba tusithubutu kabisa kuwakosoa (critique) wazi wazi kwa vile wana uwezo wa kutupitisha katika bonde la mauti na asiwepo mtu yeyote wa kutusaidia wala kuwachukulia hatua. SIO?

Basi vyema. Tunashukuru kutufahamisha hali halisi ya kisiasa iliyopo nchini leo hii. Itakuwa vyema zaidi ukitufahamisha hao “wenye siasa” ni kina nani ili tujihadhari na anga zao kabisa.

Kwa kuanzia, nimeshawapa tahadhari vijana wangu wasijihusishe kabisa na mijadala na harakati za demokrasia na haki za binadamu hapa nchini na wajitahidi sana kujua kinachoitwa “realpolitik” ili kuepuka masahibu kama yanayomfika mdude chadema. NIKO SAHIHI?
Siasa za Tanzania zina wenyewe!
 
Tuliokuwa tunamshangilia mdude wote kwa sauti moja tuseme tupoooo!, kumdhihirishia mleta mada kama tupo na tunaendelea kumshangilia nyuma ya vibodi vyetu.
Wakati akiwapa burudani mlikuwa pamoja lakini kwa sasa mko kwenye vibodi vyenu!
 
Umasikini unakufanya uwe na chuki tafuta hela hudumia familia yako na wazazi wako kama bado wako hai
 
Dah lakini bila shaka taarifa muhimu zinamfikia ikiwa ni pamoja na 01-01-2021 yule mgombea anarudi baada ya kumaliza kazi yake..
 
Siasa za nchi hii ukizivamia bila kujua vizuri historia yake lazima zitakupeleka sehemu ambayo ulidhani haiwezekani!

Wanasiasa wanaozijua vizuri siasa za nchi hii kwa sasa wako na familia zao huku wale ambao walizivamia bila kuzijua kwa sasa wako sehemu ambayo hawakutegemea!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' ni moja ya watu waliozivamia siasa nchini bila kuwa na ufahamu mpana!

Shangwe na sifa alizokuwa anazipata kwenye mitandao ya kijamii zilimpa sense of invincibility fable! Akadhani ni zaidi hata ya wale wanaomsifia na kumshangilia!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' hakujua wanaomsifia na kumshangilia wanamuona kama mtoa burudani kwa sababu baadhi ya watanzania wanazichukulia siasa kama burudani!

''Sense of invincibility fable'' ilimfanya azidishe burudani zake ambazo kiuhalisia hazikuwa na mwelekeo!

Baada ya ''kuguswa'' na wenye siasa, kwa sasa waliokuwa wanampa sifa na kumshangilia hawaonekani tena! Wamehamia kwa watu wengine ambao matendo yao ya kisiasa pia ni kama watoa burudani!

Nadhani anayejiita ''Mdude Chadema'' hakuwahi kuyasoma maneno ya hekima na busara yaliyosemwa na Mwanajeshi wa Kichina, Sun Tzu yasemayo, '' If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Wazee wetu pia walituasa wakisema, ''Akili za kuambiwa, changanya na za kwako''! Hii ina maana sikiliza na uchambue kwa makini na kutafakari ulichokisikiliza kabla hujafanya maamuzi!

Kwa sasa aliyebaki anahangaika ni yeye na familia yake huku waliokuwa wanamsifia na kumshangilia wakiendelea na burudani zingine za siasa! Waliokuwa wanamsifia na kumshangilia hawaonekani hata mahakamani ili kuendeleza sifa na shangwe!

Siasa za nchi hii zina wenyewe na kama unataka kuzifanya siasa kama burudani lazima kwanza ujue kikomo chake!

Methali inayosema, '' wajinga ndio waliwao'' haikuandikwa kama burudani!
Kwani wewe na wenzako mlimuweka huko jela mmepata nini? Kama sio ukosa akili ?
 
Wewemsema ukweli haya tueleze ukweli kipi ni kweli ambacho wanakiwakilisha hao wenye siasa zao ?

unipe jibu
 
Siasa za nchi hii ukizivamia bila kujua vizuri historia yake lazima zitakupeleka sehemu ambayo ulidhani haiwezekani!

Wanasiasa wanaozijua vizuri siasa za nchi hii kwa sasa wako na familia zao huku wale ambao walizivamia bila kuzijua kwa sasa wako sehemu ambayo hawakutegemea!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' ni moja ya watu waliozivamia siasa nchini bila kuwa na ufahamu mpana!

Shangwe na sifa alizokuwa anazipata kwenye mitandao ya kijamii zilimpa sense of invincibility fable! Akadhani ni zaidi hata ya wale wanaomsifia na kumshangilia!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' hakujua wanaomsifia na kumshangilia wanamuona kama mtoa burudani kwa sababu baadhi ya watanzania wanazichukulia siasa kama burudani!

''Sense of invincibility fable'' ilimfanya azidishe burudani zake ambazo kiuhalisia hazikuwa na mwelekeo!

Baada ya ''kuguswa'' na wenye siasa, kwa sasa waliokuwa wanampa sifa na kumshangilia hawaonekani tena! Wamehamia kwa watu wengine ambao matendo yao ya kisiasa pia ni kama watoa burudani!

Nadhani anayejiita ''Mdude Chadema'' hakuwahi kuyasoma maneno ya hekima na busara yaliyosemwa na Mwanajeshi wa Kichina, Sun Tzu yasemayo, '' If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Wazee wetu pia walituasa wakisema, ''Akili za kuambiwa, changanya na za kwako''! Hii ina maana sikiliza na uchambue kwa makini na kutafakari ulichokisikiliza kabla hujafanya maamuzi!

Kwa sasa aliyebaki anahangaika ni yeye na familia yake huku waliokuwa wanamsifia na kumshangilia wakiendelea na burudani zingine za siasa! Waliokuwa wanamsifia na kumshangilia hawaonekani hata mahakamani ili kuendeleza sifa na shangwe!

Siasa za nchi hii zina wenyewe na kama unataka kuzifanya siasa kama burudani lazima kwanza ujue kikomo chake!

Methali inayosema, '' wajinga ndio waliwao'' haikuandikwa kama burudani!
cc: Zitto Kabwe, Maalim Seif, Tundu Lissu, Godbless Lema, Fatma Karume, Maria Sarungi, Wasanii wote wa Siasa/Wanaharakati mavi
 
Badala. ya kuwapigia. Kelele watawala wasiotumia haki unamlaumu Mdude kwa kesi ya kubambikiwa ,Kesi haisikilizwi kila siku inapigwa kalenda, Wewe kweli ni hasara ya Taifa
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom