Hivi Mdude Nyagali ni kiumbe wa namna gani?

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,422
18,056
Kwenye hotuba yake ya kwanza akiapishwa Rais Samia mnamo 19/03/2021 alitamka kuwa magazeti yafunguliwe, wananchi waikosoe Serikali kwa mujibu wa sheria. Akasisitiza na kesi za kubambikizwa zifutwe. Akakemea Kodi za DHULUMA zikusanywazo na TRA, na kuikemea TAKUKURU na Polisi kwa kuwanyanyasa watu bila makosa.

Kweli tukaanza kuona nuru mpya baada ya siku chache. Ikawa kama ni kupindua kabisa mambo ya ukatili na uuaji ambayo yalitamalaki wakati wa Magufuli.

Kesi ya Akwilina ikapinduliwa na Mahakama ya Rufaa, yule Mdude CHADEMA wa Mbozi maarufu kwa matusi naye akashinda kesi

Mara tukaanza kusikia kauli za matusi kwenye mikutano ya CHADEMA. Mfano ni ile kauli ya Mdude siku 4 tu baada ya kuachiwa alisikika akiongea Jukwaani Barracuda Tabata kuwa "Mwambieni huyo Mama yenu, nitamnyoa kwa wembe uleule niliotumia kumnyoa mtangulizi wake"

Alitamka maneno mbele ya Mbowe na viongozi wengine wa CDM na hawakumchukulia hatua mpaka leo.

Kwa mtazamo wangu Serikali imeona pengine bado hatuna busara katika kutumia uhuru wa maoni. Tunaleta matusi badala ya kutoa maoni.
 
Hapo matusi yako wapi?
 
Kwenye hotuba yake ya kwanza akiapishwa Rais Samia mnamo 19/03/2021 alitamka kuwa magazeti yafunguliwe, wananchi waikosoe Serikali kwa mujibu wa sheria...
Tatizo hiki kikundi cha magaidi inatakiwa kifutwe kabisa kipotee kabisa. Hapo dawa ni kukamata na kuweka ndani mbowe na kurejesha ile kesi ili ahukumiwe kunyongwa mpaka kufa
 
Ninamlaumu Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA kwa kutomsaidia Mdude kisaikolojia na kumwacha aangamie. Mbona kina Malisa GJ na yule mtoto wa Mbowe hawapati kashkash kama za Mdude?

Jibu ni kuwa wazazi wao ambao pia ni wamiliki wa CHADEMA wanawaongoza vizuri na kuwaonya kuhusu uropokaji. Mdude kwasababu ni mtu baki ni kama wamemtoa kafara.

Anachoambulia ni hashtag ya free mdude. Kina Mnyika wao huwa hawakamatwi kwa sababu wanajua timing ya kuongea.

Mdude kama watoto wengine kutoka familia maskini wanawekwa mstari wa mbele kimakusudi na mmiliki wa CHADEMA Sultan Mbowe.
 
Hakuna kukosoa kwa usraarabu.
A ni A na B ni B Samia kakosea na inabidi akemewe hadharani.
Kwanini asigawe na bandari za Zanzibar?
Je, ni upendo gani mkuu alio nao kwa Tanganyika kuliko Zanzibar ambako ndio kwake?
Huyu Stuxnet ni wa ovyo kweli,
Magufuli alifanya huu ujinga, alimkosoa kweli, hilo sio shida, hata Mimi nilimkosoa JPM

Leo Samia anafanya ujinga ule ule, eti anasema serikali imeona hatuna busara. Huu ni ujinga wa ovyo. Na nakuonya Stuxnet uache kutumika na serikali hii ktk ujinga kama huu.

Halafu kama ni kukomaa, mbona comments zako tena za maneno makali sana zipo humu dhidi ya JPM? Sasa hiyo kusema saivi hatuna busara , mara hatujakomaa, ndio nini.. au kisa ni Samia!

Acheni ujinga bhana
 
Back
Top Bottom