Waliokuwa wanamshangilia na kumsifu anayejiita 'Mdude Chadema' wako wapi?

Soma Historia ya Nelson Mandela na harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Tunaongelea siasa za nchi yetu. Hayo ya Afrika kusini hayatuhusu. Siasa zetu ni za burudani kama za Yanga vs Simba.
 
Yaani kwa akili zangu timamu nifanye ''vituko'' kama alivyofanya anayejiita Mdude Chadema?

Wewe mbona mpaka sasa hujawekwa ndani?
Sio ufanye vituko wewe ni kituko halisi. Haya majina huwa kinyume kuficha uhalisia au ni chui kuvikwa ngozi ya kondoo. Shakespeare alipata uliza what's a name? Akajijibu kuwa waridi liite jina lolote lile labaki waridi tu. Lanukia.
Chama cha Hitler kiliitwa Nationalist. Akina mjungu/mzungu ni weusi ti. Siku wakiita huyo tall akaja utazimia. Mbele yako utadhani tolo kakaa. Hapana tolo ni emolo kama mwongo anavyojiita MsemajiUkweli!
 
Soma Historia ya Nelson Mandela na harakati zake dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Ndiyo maana CHADEMA/upinzani kuna matatizo. Msilinganishe harakati za upinzani na zile za Mandela. Hapo unapoteza dira. Mandela alikuwa ana harakati za kuwaondoa mabeberu (wazungu). Upinzani harakati zake ni kuiondoa CCM ambayo si mabeberu. CCM ni ya Watanzania kama upinzani ulivyo wa Watanzania. Huwezi ukamfanya mtanzania wa kawaida akaelewa kuwa CCM ni sawa na makaburu. Ila CCM inaweza kufanikiwa kuwabia Watanzania kuwa upinzani unatumwa na Mabeberu, maana kila wakikwazwa wanakimbilia huko. Ili upinzani kuondokana na hili la "nitakushitaki kwa mama/baba, lazima wasimame kideded kunadi sera zao na kukosoa bila kutishia kushtaki kwa baba/mama, maana kama mashtaka yakifanikiwa atakayeumia ni yule unayetaka akubaliane nawe. Hawezi kukubaliana na wewe kwa sababu vitendo vyako vinamfanya aumie zaidi kuliko vile ambayo CCM inalalamikiwa. Mafanikio ya upinzani yatategemea siku ile upinzani utaacha kulinganisha CCM na mabeberu, maana kufanya hivyo ni kuwaita wananchi wote ambao ni CCM mabeberu, hapo huwezi kupasua. Waone au ione CCM na wanachama wake kama watu wenye siasa mbovu na uwe na uwezo wa kuonyesha ubovu wake. Msiwe kama Trump anayedai kuibiwa kura akiambiwa alete ushahidi, anashindwa.
 
Sina zaidi ya kuongeza kwenye maoni yako zaidi ya kukupongeza kwa uelewa mpana wa siasa.
 
Hawa chadema hawajielewi kabsa nliwazarau kipindi kile cha Bunge lakatiba walipotoka nje ,kipindi cha corona pia walitaka kuwe na lockdown wakidai watu wanakufa sana,vijana tuache kutumika vibaya ,hongera nyingi sana kwa Raisi Magufuli maana kipindi chakorona alisimama na msimamo wake kwakuitangazia Dunia kua Tanzania hakuna covid 19 Mungu endelea kumbariki jpm na umpe maisha marefu
 
Waswahili waliishasema Mchuma Janga hula na wa kwao, pole sana Mdude Nyagali ipo siku yatakwisha na uterejea uraini.
 
Hongera sana mdude chadema kwa kuvuna ulichokipanda.. Endelea kuchezeshwa sebene na manyampara
Wala hakuna sebene analochezeshwa. Nimekaa nae stoo wiki kadhaa, nadiriki kusema huyu jamaa sio mtu wa kawaida! Yuko na amani na furaha kama vile hakuna kitu anachopitia
 
Siasa za nchi hii ukizivamia bila kujua vizuri historia yake lazima zitakupeleka sehemu ambayo ulidhani haiwezekani!

Wanasiasa wanaozijua vizuri siasa za nchi hii kwa sasa wako na familia zao huku wale ambao walizivamia bila kuzijua kwa sasa wako sehemu ambayo hawakutegemea!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' ni moja ya watu waliozivamia siasa nchini bila kuwa na ufahamu mpana!

Shangwe na sifa alizokuwa anazipata kwenye mitandao ya kijamii zilimpa sense of invincibility fable! Akadhani ni zaidi hata ya wale wanaomsifia na kumshangilia!

Anayejiita ''Mdude Chadema'' hakujua wanaomsifia na kumshangilia wanamuona kama mtoa burudani kwa sababu baadhi ya watanzania wanazichukulia siasa kama burudani!

''Sense of invincibility fable'' ilimfanya azidishe burudani zake ambazo kiuhalisia hazikuwa na mwelekeo!

Baada ya ''kuguswa'' na wenye siasa, kwa sasa waliokuwa wanampa sifa na kumshangilia hawaonekani tena! Wamehamia kwa watu wengine ambao matendo yao ya kisiasa pia ni kama watoa burudani!

Nadhani anayejiita ''Mdude Chadema'' hakuwahi kuyasoma maneno ya hekima na busara yaliyosemwa na Mwanajeshi wa Kichina, Sun Tzu yasemayo, '' If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Wazee wetu pia walituasa wakisema, ''Akili za kuambiwa, changanya naza kwako''! Hii ina maana sikiliza na uchambue kwa makini na kutafakari ulichokisikiliza kabla hujafanya maamuzi!

Kwa sasa aliyebaki anahangaika ni yeye na familia yake huku waliokuwa wanamsifia na kumshangilia wakiendelea na burudani zingine za siasa! Waliokuwa wanamsifia na kumshangilia hawaonekani hata mahakamani ili kuendeleza sifa na shangwe!

Siasa za nchi hii zina wenyewe na kama unataka kuzifanya siasa kama burudani lazima kwanza ujue kikomo chake!

Methali inayosema, '' wajinga ndio waliwao'' haikuandikwa kama burudani!
Jitambue we kijanaa ulipaswa kukemea anayemfanyia uovu MTU kisa ametoa maoni yake na sio mtoa maoni!! Nyerere aliwaasa vijana kama wewe kuhusu kutokuwa waoga na kuacha kujipendekeza mtaliwa!!!
Hujiulizi kwann mwenzie katolewa na kutunukiwa kwenda mjengoni?? Huoni michezo ya kijinga ktk hili au kujipendekeza kwako kunakufanya mpofu??
Kama wakiume basi badilika ili watoto wako wajifunze utu,ujasiri na usemaji kweli whatever the situation badala ya woga,kujipendekeza na kupalilia uovu which is shameful. CHANGE kijanaa and be a man!!.
NB. Jela IPO kwaajili yetu tutakaa ikibidi yote mapito mradi Muumba wetu anatuwazia mema kwakuwa tumetenda hayo.
 
Nikionacho kwani ni ile hali aisikiayo mtu pale mwenzie asagapo tofali. Huhisi kama meno yanapata shida lakini msagaji yupo na Furaha. Mdude huo mchezo anaupenda hasa pale anapoibainisha bayana uovu wa serikali kuonea wananchi wake.
Mdude anaungana na wanasiasa nguli duniani waliofungwa kwa sababu ya misimamo mkali ya kisiasa. Hata wewe Unajua siasa yake ndio inayomuweka ndani na Unajua kuwa anaonewa kwa mujibu wa andiko lako. Yeye anatunukiwa prison graduation award like Jomo Kenyatta of Kenya, Mahatma Gandhi, Mandela na wengine wengi. Mwenzio anajilia pilipili yake wewe unatokwa chozi.
Sasa hivi Mdude yupo salama sana hasa Kipindi hiki cha kesi yake dhidi ya serikali. Mara mbili kanusurika kuuwawa baada ya kutekwa. Lengo ilikuwa ni kumzuia asifungue kesi pia asiendelee nazo. Hivi sasa yupo salama na kuendelea kujenga usugu na kuacha kuogopa magereza hata mapambano dhidi ya dola kama walivyofanya Lugemalila na Sethi
Wewe upo nje huru na Kisimu chako ndio maana unadhani Mdude anafurahi kuwa jela muda huu. Jela ni jehanam ya duniani, yaani Jail is hell in earth.

Jela siyo mahali kuzuri, hakwenda by choice, kule kulala kama kuku, mahitaji mengi ya kibinadamu kama tendo la ndoa, mavazi atakayo, kuongea na kutembea muda atakayo, kula chakula atakacho, kutibiwa hospital atakayo, hivyo vyote hapati.

Jela magonjwa mengi sana. Huku mtaani biashara zake haziendi, akitoka atajikuta muda mwingi amepoteza na chama chake kipo hoi hakina msaada nae kivile.
 
Wala hakuna sebene analochezeshwa. Nimekaa nae stoo wiki kadhaa, nadiriki kusema huyu jamaa sio mtu wa kawaida! Yuko na amani na furaha kama vile hakuna kitu anachopitia
Huwezi kusindikizwa na kimemo wakati wa kuingia mule usichezeshwe sebene
 
Kwa hiyo unakubali kafungwa kwa sababu za kisiasa na sio kukutwa na madawa ya kulevya?
Kukutwa nayo kakutwa nayo.
Swali hapa linapaswa kuwa , Hayo madawa yalikuwa yake au alipandikiziwa na mtu?
Was that evidence his property or was planted in his personal belongings?
Evidence was planted in his premises?
 
Wewe upo nje huru na Kisimu chako ndio maana unadhani Mdude anafurahi kuwa jela muda huu. Jela ni jehanam ya duniani, yaani Jail is hell in earth.

Jela siyo mahali kuzuri, hakwenda by choice, kule kulala kama kuku, mahitaji mengi ya kibinadamu kama tendo la ndoa, mavazi atakayo, kuongea na kutembea muda atakayo, kula chakula atakacho, kutibiwa hospital atakayo, hivyo vyote hapati.

Jela magonjwa mengi sana. Huku mtaani biashara zake haziendi, akitoka atajikuta muda mwingi amepoteza na chama chake kipo hoi hakina msaada nae kivile.
Hayo huwa hawaangalii watu waliochafukwa robo na uonevu. Siku ukiacha kujikomba na akili za kuona uovu zikikurudia utafanya uamuzi.
Mie sijakamatwa ikitokea nitafurahi kupata prison graduation.
Kwa kuwa wewe ni mwizi au jambazi tapeli ukienda kule utaona shida.
Utawala unapata shida sana kwa hawa wanaoonewa kuwa ndani na kusoma kusalim amri. Sheria ya prior bargain imeletwa wakadhani Luge na Seth watairukia ili kuondoa aibu wapi. Peleka ushahidi hakuna. Mashetani mnafurahia udharimu.
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom