Waliokuwa na vibali vya ujenzi na kulipia kodi ya majengo hawawezi kwenda mahakamani kudai fidia?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,324
152,136
Kumekuwepo na madai/tuhuma kuwa baadhi ya watumishi wa serikali ndio walitoa vibali vya ujenzi kwa watu waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa na zaidi serikali ilikuwa inapokea kodi ya majengo kutoka wananchi waliokuwa wanamiliki nyumba hizo.

Kama kweli waliotoa vibali ni watumishi wa serikali,kwanini serikali isishitakiwe mahakamani na kutakiwa kulipa wananchi fidia kutokana na makosa ya watumishi wake?

Sitaki kuamini kama kila aliejenga katika eneo lisiloruhusiwa alihonga bali huenda kuna ambao hawakupewa taarifa sahihi.

Wanasheria na Watetezi wa haki za binadamu mbona mpo kimya kiasi hiki?!
 
Tuanze mambo ya kusumbuana na serikali, wakati inapopambana kuweka mambo sawa kwa faida zetu wenyewe.

Tutambue kwamba, ni kweli serikali ya ccm ndio imetufikisha hapa tulipo, lakini kama serikali hiyo hiyo imekaa kurekebisha mambo, let's give our support, hatujapata serikali nyingine badala bado.

Ikumbukwe kuwa, there is no gain without pain.
 
Tuanze mambo ya kusumbuana na serikali, wakati inapopambanea kuweka mambo sawa kwa faida zetu wenyewe.

Tutambue kwamba, ni kweli serikali ya ccm ndio imetufikisha hapa tulipo, lakini kama serikali hiyo hiyo imekaa kurekebisha mambo, let's give our support, hatujapata serikali nyingine badala bado.

Ikumbukwe kuwa, there is no gain without pain.

Na yenyewe kama inapaswa kuwajibika ni shariti iwajibike.
 
Watumishi wengi wa idara ya aridhi waliouza maeneo yawazi wengi wao ni marehemu.
Imekula kwetu
 
Wengi walio nunua hivi viwanja walifanya hivyo wakijua sio sahihi, nani hasiyejua open space au chanzo cha Maji au ukingo wa mto, au njia ya Maji ya msimu.
 
Tatizo ni kwamba, upuuzi huo, na mwingine mwingi kama huo, uligeuka kuwa ndio utaratibu wa kawaida wa kujipatia fedha huko serikalini, mkaburu kama chukua chako Mapema.

Now that Kuna mtu ameonyesha dhamira ya dhati na anatumbua majipu kweli kweli, si jambo bana, tumpe ushirikiano, kesi za kupinga, ni kurudi nyuma

Ila watakaokamatwa ndio hivyo wawajibike.
 
ulipata kitu halali kwa njia haramu.... ama ulipata kitu haramu kwa njia halali. ... yote ni majipu meza maumivu

Aliyepata kitu halali kwa njia halali SINA SHAKA NAYE atalipwa fidia
 
Hahaha unahangaika sana kupingana na utawala huu, jitahidi kusukuma kitu kinacho sukumika otherwise you exhausting your self without reasonable grounds.

Kudai fidia bila kuwa maelezo na vielelezo sahihi vya uhalali wa umiliki,hati na vibali bado hutalipwa! Wengi wana hati na vibali vyenye harufu ya rushwa.

Ni wachache sana wenye umiliki usio na collusion.
 
Hapo umenena mkuu mtu analipa kodi ya jengo halafu unaenda kumbomolea mbona kuna magholofa yapo chini ya kiwango na hayajabomolewa huo ni uonevu
 
Hahaha unahangaika sana kupingana na utawala huu, jitahidi kusukuma kitu kinacho sukumika otherwise you exhausting your self without reasonable grounds.

Kudai fidia bila kuwa maelezo na vielelezo sahihi vya uhalali wa umiliki,hati na vibali bado hutalipwa! Wengi wana hati na vibali vyenye harufu ya rushwa.

Ni wachache sana wenye umiliki usio na collusion.
CCM yenyewe ni jipu kuwa kuliko yote alafu unaongea nini?Hiki chama kinapaswa kilichokuwa kinasimamia serikali chenywe kinapaswa kuwajibika kwanza.Nyinyi ndio mlikuwa wasimamizi wakuu wa kila kitu ila mlikaa kimya kwa miako yote alafu leo mnajifanya kama hamna hatia!
 
Rule of Law/Sustainable Development/Public Interest/Dictatorship Democracy/Independence of Judiciary/Natural Justice
 
Be assured people mambo yakinyooka, utaratibu ukianza kufuatwa, nchi ikawa kwenye mstari ni lazima tuwaunge mkono, tumeishi kama mazombi kwa muda mrefu. Now its time to wake up, be redeemed, viwanja kuuzwa kuna utaratibu ulio dhahiri, hamna urongo urongo
 
Tuanze mambo ya kusumbuana na serikali, wakati inapopambana kuweka mambo sawa kwa faida zetu wenyewe.

Tutambue kwamba, ni kweli serikali ya ccm ndio imetufikisha hapa tulipo, lakini kama serikali hiyo hiyo imekaa kurekebisha mambo, let's give our support, hatujapata serikali nyingine badala bado.

Ikumbukwe kuwa, there is no gain without pain.

Ushawahi kumiliki nyumba?
 
Back
Top Bottom