Waliojenga kwenye fukwe Dar waonja shubiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliojenga kwenye fukwe Dar waonja shubiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka


  Wizara ya Maliasiali na Utalii, Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni wameendesha operesheni ya kubomoa nyumba na kuta zilizojengwa kwenye viwanja zaidi 100 vilivyopo ndani ya hifadhi ya misitu ya mikoko kwenye fukwe za bahari na mito kinyume cha sheria.

  Utekelezaji wa zoezi hilo umekuja miezi michache tu tangu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, atoe tahadhari kwa watu waliojenga nyumba zao ndani ya mita 60 kutoka usawa wa bahari na kwenye mito ikiwa ni mkakati wa kuokoa maeneo oevu na fukwe na kuilinda mikoko.

  Operesheni hiyo ilianza saa 1:00 asubuhi jana kwa kusimamiwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, Charles Kenyela.

  Mbali na nyumba za kuishi ambazo baadhi zinamilikiwa na watu maarufu wakiwemo wanasheria, pia kanisa la Kipentekoste la Dar es Salaam Christian Chapel pamoja na nyumba ya mchungaji ni miongoni mwa zilizobolewa.

  Zoezi hilo lililofanywa kwa kushtukiza, baadhi ya wamiliki wake walikutwa bado hawajahamisha vifaa vyao licha ya kuwekewa alama ya X muda mrefu na walipata wakati mgumu kukimbizana na matingatinga ya kampuni ya Majembe Action Mart yaliyokuwa yakibomoa nyumba hizo.

  Wakati bomoboa hiyo ikiendeshwa katika maeneo ya Mbezi Beach, kandokando ya bahari ya Hindi, mto Ndubwe na Mbezi, baadhi ya vijana wanaoishi na maeneo hayo walikuwa wakifurahia hatua hiyo huku wengine wakisika wakisema ‘bomoboa hizo nyumba za mafisadi’.

  Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji NEMC, Dk. Robert Ntakamtenga, alisema zoezi hilo linalenga kulinda mazingira ya bahari na mito hiyo.

  Alisema ni kosa kujenga nyumba ndani ya mita 60 kutoka usawa wa bahari lakini watu wamekuwa wakifanya hivyo makusidi.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali na Wakala wa Huduma za Misitu, Zawad Mbwambo, alisema wananchi wa maeneo yaliyobomolewa walielezwa tangu mwaka 2008 wasijenge maeneo hayo lakini walipuuza.

  Alisema mwaka 2009 serikali iliamua kufanya tathimini kwa kutumia tume iliyoundwa kuchunguza tatizo hilo na ilibainika kuwa kuna viwanja zaidi ya 100 ambavyo vimevamiwa na wananchi kwa kujenga makazi katika maeneo ya mito na kando ya bahari.

  Naye Kenyela, alisema baadhi ya nyumba ikiwemo ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Getrude Rwakatale ambayo licha ya kujengwa kandokando ya ufukwe wa bahari haijabomolewa kwasababu kuna zuio la Mahakama.
  CHANZO: NIPASHE

   
 2. t

  testa JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huyu mama yeye ni nani kwenye nchi hii
   
 3. Bandabichi

  Bandabichi JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi namkubali sasa waziri husika, na hongera zake huyu mama,

  Aje na huku halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Kwa maana sioni sababu ya watu kujenga eneo la Sambara Logde wakati eneo hlio linazungukwa na taasisi tupu, Pembeni ya eneo hilo kuna Makao ya FFU, Opposite kuna Shule ya Highland na chuo cha Klerruu na Uwanja wa kanisa zamani Kichangani Pr school na Nyuma yake kuna Lugalo Secondary Hivi viwanja vimetoka wapi?

  Ukienda maeneo ya Gangilonga ndo aibu kabisa Raia wanaamisha Milima Wanajenga kwenye njia za maji.
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni waziri wa ardhi kwani humjui status yake?????
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tena asiyebabaishwa na mafisadi kwani aliwahi kusema hana shida ya pesa ya kula!!! Namkubali vipi huyu mama!!!!
   
Loading...