Walioingiza mabomu Arusha wakamatwa!

Walioingiza mabomu Arusha wakamatwa!

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
5,597
Reaction score
1,016
WATUHUMIWA walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenye mkutano wa wa hadhara wa CHADEMA, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema hayo jana katika mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti.

“Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani.

Mulongo alisema kwa sasa Polisi iko katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo.

Malengo mengine kwa mujibu wa Mulongo ni kuwafahamu watu wote waliopewa zabuni ya kuingiza mabomu hayo, ili hatua za kisheria zifuate.

Mulongo aliomba wananchi waendelee kutulia wakisubiri matokeo ya Serikali na hata wakitajwa wahusika waiachie Polisi ifanye kazi yake. Mabomu hayo yalirushwa Mei 5 kanisani Olasiti na Juni 15 uwanja wa Soweto, wakati wa hitimisho la kampeni za udiwani za Chadema mkoani hapa.

Kanisani Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla.

Mbali na Askofu Padilla, pia alikuwapo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha na waumini zaidi ya 2,000.

Wakati mgeni rasmi akitoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi, mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi, kwenda eneo lenye mkusanyiko wa watu na baada ya kutua, kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa uliosababisha taharuki miongoni mwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

Katika tukio hilo, watu wawili walifariki dunia, akiwamo Regina Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariki dunia siku ya tukio wakati akipewa matibabu katika hospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine James Gabriel (16) alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 6.

Bomu hilo lililipuka Juni 15, katika Uwanja wa Soweto wakati wanachama na wapenzi wa Chadema wakiwa wamekusanyika kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani humo.

Mlipuaji alilipua bomu hilo dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kumaliza kuhutubia mkutano huo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kisha kuacha maswali mengi.

Mulongo alitaja waliopoteza maisha kuwa ni Judith Mushi (46) ambaye alikuwa Katibu Kata wa Chadema, Kata ya Sokoni One na mkazi wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Justine (16) wa Sombetini ambaye alifariki dunia katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

Siasa Akizungumza katika mkutano huo wa kukaribisha wawekezaji jana, Mulongo alisisitiza Serikali inahitaji siasa zenye tija na anapotokea mwanasiasa mwenye kupinga maendeleo, atashughulikiwa.

“Kila mwanasiasa awe wa kuchaguliwa au kuteuliwa, aliposimama kuomba nafasi hiyo wote waliahidi maendeleo kwa wananchi, hivyo tufanye hivyo,” alisema.

Mulongo alisisitiza kuwa kutokana na umakini wa vyombo vya usalama, wanaomba wawekezaji wasiwe na hofu, wajitokeze kuwekeza maeneo ya mkoani hapo, bila hofu.

Alisema mkoa huo unatangaza fursa za uwekezaji kwa sababu ya kuongeza kipato na ajira kwa wakazi wa Jiji hilo pamoja na kupanua wigo wa masoko na bidhaa zinazozalishwa hapa.


CHANZO: HabariLeo
 
Kama wako kwenye mahojiano ya mwisho kulikuwa hakuna haja ya . kutumbia. Angesubiri wamalize mazungumzo yao then atuambie kitu kamili kuliko kuleta saisa kwenye upelelezi. Watu wengine bana...
 
Nadhani wanatakaa tu waturudishe kwenye ile sinema ya video ya CDM. Nayo hiyo ni karata bado kwa CCM.
 
Huyo mkuu wa mkoa angesubiri mahojiano yaishe kwanza ndo aje na hizo habari, sio kutuletea yale yale ya mtekaji wa Ulimboka. Politics at work!!
 
Hizi ni propaganda, jambo zito kama hilo msemaji wake lazima awe kutoka wizara husika au jeshi la polisi ama waziri ama rais nk.

Mkuu wa mkowa......??? Kama .... Upuuzi wake kwa lema ameutatua/unaendeleaje mbona halizunguzii hilo.....
 
wasitudanganye walio lipua bomu kwenye mkutano wa chadema ni polisi wenyewe alaf hao hao wanajifanya kuwatafuta walipuaji.

hawa polisi si wa kuwaamini kabisa wameshatengeneza picha lingine kama la ulimboka.
 
Kama wako kwenye mahojiano ya mwisho kulikuwa hakuna haja ya . kutumbia. Angesubiri wamalize mazungumzo yao then atuambie kitu kamili kuliko kuleta saisa kwenye upelelezi. Watu wengine bana...

>Hao ndo wakuu wa mikoa wa bwana mkubwa...!
 
hizi ni propaganda, jambo zito kama hilo msemaji wake lazima awe kutoka wizara husika au jeshi la polisi ama waziri ama rais nk.

Mkuu wa mkowa......??? Kama .... Upuuzi wake kwa lema ameutatua/unaendeleaje mbona halizunguzii hilo.....

sitoshangaa na nape akatolea ufafanuzi hili jambo.
 
Majangaa sio machizi kama wa issue ya ulimboka wale..?H aiwezekani ulipue wewe na ujihoji mwenyewe kweli magamba majangaaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kinachotafutwa hapo nikupoza joto la kashifa ya mauwaji na uteseji wa raia huko zanziba/tanganyika kwa kemikali.

Wale wakuu wa mikowa na baadhi ya viongozi wanaotumika kwa siri kama usalama wa Taifa ndiyo wazushi wa kamata

kamata za kishenzi na baada ya muda na hali kutulia wote waliokatwa kwa kubambikia na uzuliaji huachiwa.
 
Kama bomu lilithibitishwa kuwa lilitengenezwa China,na kwa kuwa Balozi wa China ameonekana wazi kuwa bega kwa bega na CCM huku Nape akitolea ufafanuzi kuwa China na CCM ni marafiki toka enzi,je si ni dhahiri shahiri CCM ndio waliohusika na mabomu hayo!Nawasilisha
 
wanajaribu kufunika maovu ya zanzibar ya tindikali.this country bana ni banana kweli kweli.MABOMU YAMETOKA CHINA WASISAHAU
 
sitoshangaa na nape akatolea ufafanuzi hili jambo.


kabisa kwa akili ya Nape inawezekana, wala hujakosea.......vipi Rais akatae kuunda tume huru kuubaini ukweli kinyume

chake wale wanaotiliwa mashaka wanaachwa kujichungulia.....huwezi kuwa na kashifa kwa kujichungulia........ siwewe

mwenyewe.....ila ukichunguliwa na watu tofauti hapo hamaki nk huwezekana.
 
Suala la kujua chanzo cha bomu pale Arusha ilikuwa haihitaji hata elimu ya sekondari. kama bomu lilikuwa na serial No. kutoka China inashindikana vipi kumpata aliye nunua hilo bomu. au hakukua na willingness ya kuwatafuta hao watu. au alisubiliwa afe nani ndio uharaka uwepo?
 
Suala la kujua chanzo cha bomu pale Arusha ilikuwa haihitaji hata elimu ya sekondari. kama bomu lilikuwa na serial No. kutoka China inashindikana vipi kumpata aliye nunua hilo bomu. au hakukua na willingness ya kuwatafuta hao watu. au alisubiliwa afe nani ndio uharaka uwepo?

HUU ni usanii haingiii akilini walipuaji kulipua ktk matukio tofauti na sehemu tofauti na siku tofauti na malengo tofauti halafu waje wakamtwe kwa siku moja na muda mmoja.FULL USANIII.Ipo siku kweli itatuweka HURU
 
Nimekuja nakimbia nikijua ni RPC, kumbe huyo Mulongo!!! Hajasema mtwara anaenda lini?
 
Huyo mkuu wa mkoa angesubiri mahojiano yaishe kwanza ndo aje na hizo habari, sio kutuletea yale yale ya mtekaji wa Ulimboka. Politics at work!!

>WANAFUNIKA SUALA LA PADRI KUMWAGIWA TINDIKALI... Hiyo ndo ccm inayojiendesha ''kimatukio'' tutafika kweli
 
s vuvuzela nape alisema chadema ndio walijilipua?
 
Back
Top Bottom