Waliohamia CCM hiki ndicho kitawapata!

Waliohamia CCM hiki ndicho kitawapata!

Habari wakuu!

Nikiwa miongoni mwa watu tulioshikwa na sintofahamu ya kile kinachoendelea hapa chini. Kitendo cha baadhi ya wenyeviti, madiwani na wabunge kutoka Vyama vya Upinzani kuhamia Chama tawaka cha CCM. Jambo hili limeleta maswali mengi sana vichwani mwa watu wakiwemo wanazuoni, wanasiasa na hata watu wakawaida.

Wapo baadhi husema kuwa hama hama hii ni matokeo ya Rushwa na hongo itolewayo na Chama Tawala. Wengine hudai jambo hili ni kutokana na utendaji uliotukuka wa Mheshimiwa Rais Magufuli. Binafsi ninavyoona ni ule woga wa viongozi wao katika jitihada za kutetea matumbo yao.

Nikirudi kwenye mada. CCM si wajinga mpaka waendeshe operesheni hii ya kuhamasisha wapinzani wahamie chama chao. Wanaohama ndio wajinga tena wapuuzi wasiofikiria vyema. Kama wahamiaji hawa wangekuwa na akili wasingethubutu kuhama kutoka vyama vyao. Mimi kama ningeambiwa niwape jina gani ningesema jina moja tuu nalo ni "Mambumbumbu".

Si kama nawatukana bali ndio uhalisia. Mtu mbumbumbu hafikirishi akili yake kufikiria kesho yake.
Huamua bila kufikiri na huendeshwa kwa mihemuko na hisia. Ni rahisi kumrubuni mtu mbumbumbu kwani hafikirii mara mbili.

Hiki ndicho kitakachowapata:
1.
Hawatapita katika kura za maoni ifikapo 2020.
Amini Amini nawaambieni ninao uhakika kuwa hawa mambumbumbu wataambulia patupu ifkapo 2020. Chama cha CCM katika kura za maoni kwenye ngazi ya kata na jimbo hawatapitisha tena hawa watu. Kwanza hawatakuwa na mtandao lakini kilichofanyika ni kuwarubuni wababa wa watu kwa upumbavu wao na ukosefu wa maarifa. Nauhakika Wanachama wa CCM katika chaguzi hizi wameambiwa wawapigie tuu kura ili wamalize miaka yao miwili iliyobaki alafu ikifika 2020 wamwagwe kama takataka. Hivi unawezaje kutema big G kwa karanga za kuonjeshwa kama sio umbumbumbu?

Ingekuwa busara wao wamalize miaka yao miwili hii iliyobaki wakiendelea kujijenga kisiasa na kwa wapiga kura wao. Lakini sitakuja kuamini kuwa CCM itawapitisha tena hawa viumbe.

Ninauhakika 100% hili halitatokea. Na hapa ndipo watakapojutia umbumbumbu wao. Hivi hawaijui CCM nini?

Nawasilisha
Cc:mambumbumbu wote
 
Ulafi unapozidi lazima litokee kuvimbiwa na hili likizidi basi na umauti unakuwepo.. Mjanja anakutumia wewe kumbeba ili avuke ilihali akijua unapomvusha pana nyoka wenye sumu kali inayoua taratibu.. Ukifika upande wa pili anakusifu wewe si shujaa ila usichokijua ni kwamba utaangamia muda usio mrefu.. Wahenga wenzangu mtanielewa tuuuuuuu...
Tumesha kuelewa wahenga wenzako
FB_IMG_1537109267619.jpeg
 
Ni kweli kabisa huku kwetu ndani ya chama changu Ccm makundi tayari yameshaanza kwa ajili ya japokuwa Mbunge anayetuongoza ni wa Cuf lakini kambi tayari
Tumekuelewa sana ndugu yetu kazeni buti msikubali kutawaliwa na wahamiaji haramu
 
Tumesha kuelewa wahenga wenzako View attachment 870609
Duuuuuuh!!!!!! Asante sana kwa kunikumbusha enzi zetu zile..hawa vijana wa mwendokasi watafikiri hapo ni Nanjilinji vijijini kumbe ni Daslam tulikuwa tunapanda tena wajanja tuu maana wengi walikuwa wanatembea tangu kimara/kawe shamba hadi kariakoo na posta town... Aksante kiongozi.. Waliopanda hii kitu hakika tugoshe glasi kidogo...
 
Back
Top Bottom