Waliofutiwa Shahada za Udaktari Chuo cha St. Augustine, waanza kujisalimisha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Wahitimu 15 kati 162 wa Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Fransis, Ifakara, waliofutiwa shahada zao kwa kukiuka agizo la Seneti ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut) wamesalimisha taarifa za matokeo kunusuru shahada zao.

Uamuzi wa wahitimu hao umekuja siku tatu tangu Seneti ya Saut kupitia kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Costa Mahalu kutangaza kufuta shahada za udaktari za wahitimu 162 waliokaidi agizo la kurejesha taarifa zao za matokeo zilizotolewa bila kuidhinishwa na Seneti kwa mujibu wa sheria.

Shahada za wahitimu hao zilifutwa kupitia tangazo la Machi 27, 2023 lililosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (Saut), Profesa Costa Mahalu kutekeleza agizo la kikao cha dharura cha Seneti kilichoketi Machi 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi jijini Mwanza leo Machi 29, 2023, Profesa Mahalu amesema uamuzi wa wahitimu hao 15 umefanya ambao hawajatekeleza agizo la Seneti la kurejesha taarifa za matokeo kusalia kuwa 147 kati ya wahitimu 389 wa waliohitimu shahada ya udaktari kutoka Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara kati ya mwaka 2015 hadi 2019. Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara kiko chini ya Seneti ya Saut.

“Tunawaasa wahitimu 147 waliosalia kurejesha taarifa za matokeo yao. Wakifanya hivyo ndani ya kipindi cha wiki moja ijayo, suala lao litajadiliwa na kuamuliwa katika kikao maalumu cha Seneti kinachotarajiwa kuitishwa na naamini uamuzi wa kufuta shahada zao utafikiriwa upya,” amefichua Profesa Mahalu

Balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Italia amesisitiza kuwa uongozi wa Saut hauna tatizo lolote na wahitimu hao na uko tayari kupokea taarifa za matokeo yao, kuwapa nyingine mpya zilizoidhinishwa na Seneti na kuwarejeshea shahada zao.

Pia soma > SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Tatizo lilivyoanza
Akizungimzia sakata hilo, Profesa Mahalu aliyewahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaa (UDSM) amesema tatizo hilo limechangiwa na kitendo cha Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara kutumia bila idhini ya Seneti, grading system ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) ulioagiza alama A kutolewa kuanzia ufaulu wa asilimia 70 hadi 100 tofauti na viwango vya Saut inayoelekeza alama A kutolewa kwa ufaulu unaoanzia asilimia 80 hadi 100.

Muongozo huo wa TCU ulitolewa mwaka 2015 ambapo Mei, 2016, Seneti ya Saut iliagiza uanze kutumika kwa mwaka mpya wa masomo huku watahiniwa wa mwaka 2015 wakitakiwa kutumia mfumo wa chuo wa alama A kutolewa kwa ufaulu unaoanzia asilimia 80 hadi 100.

Kinyume cha maagizo hayo ya Seneti, Balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Italia amesema Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara kilitumia grading system mpya ya TCU kwa kuirejesha nyuma ambapo wahitimu wengi kuanzia mwaka 2015 transcripts zao ziliandikwa upya.

Kutokana na makosa hayo, viongozi wawili waliohusika kubadilisha mfumo tayari wamewajibishwa kwa kufukuzwa kazi baada ya kukiri makosa yao ya kurejesha nyuma matumizi ya muongozo wa TCU.

MWANANCHI
 
Uzuri kama ujuzi wa kukata govi daktari yuko nao hata wamnyanganye vyeti ataendelea kuyakata kwenye hospital bubu
 
Tatizo unaweza kujikuta una sapu hapo wakati ulishachomoa kimeo kitambo.
 
Back
Top Bottom