Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa [REMIDIAL CLASS].
aweke na picha mkuu
Tukisema tatizo ni Rais watu wanamkingia kifua. Kikwete ni Janga la nchi hii. Kamwe hatutafanya makosa tena kuchagua Rais kutoka Sampuli yake.
Niliingia chaka mwaka 2005, lakini 2010 I Swear to my almighty GOD sikumchagua.Mkuu kwani hata wewe ulimchagua
Hii wizara kweli ina watu
OPERESHENI YA KICHWA BADALA YA MGUU NA MGUU BADALA YA KICHWA, those students are the future doctors,teachers,magistrates,ole wako upite anga zao,utafanyiwa miujiza,inabdi nijipange kusomesha my kid in the best schools na matibabu japo kenya au south africa than to risk
Mkuu, sikubaliani na nia ya serikali kuwaruhusu waliofeli kuendelea na masomo kidato cha tatu, ni kwa sababu imekwishaona madhara yake katika kipindi cha miaka 2 huko nyuma. Lakini pia nakupinga moja kwa moja kuwa kusolve tatizo hilo eti wewe utamsomesha mwanao katika shule nzuri, hiyo ni kuonyesha ulivyo mbinafsi maana hapa tunaongelea issue ya kitaifa. Pia mwanao hatasoma akawa na profession zote, atakuwa medical doctor sawa lakini atabobea mfano katika macho, atakusaidia sana ukiugua macho lakini ukiumwa moyo utapelekwa kwa doctor atakayekufanyia operesheni ya figo so unakuwa hujatatua tatizo.
Hoja yangu: Tulijadilo suala hili kitaifa na sio kifamilia.
Mkuu tatizo la wizara limekaa kifamilia zaidi. Kawambwa na Mchome wameoa nyumba moja kwa hiyo maamuzi yanayogusa taifa yanafanyika nyumbani wakifika ofisini ni kutoa tu matamko yasiyo na maslahi kwa maendeleo ya nchi hii. Yaani hawa Kawambwa, Mchome na Kamishna Bhalalusesa hawana hata chembe ya uzalendo kwa taifa hili. Maamuzi yao yote tanalenga kuua Elimu. R.I.P Elimu ya Tanzaniakwa Tanzania tutabadili mno viongozi lakini elimu imefariki. Kuingia mchome kama katibu mkuu nikadhani mambo yatakuwa mswanu kwa kuwa ni prof tena wa sheria akisaidiana na waziri wa elimu dr wa vyuma( Sido) kawambwa div.5 ukawa mkwara wa mchome wa kuingilia, imeshindikaka sasa free pass form 2, haya bana mimi sio prof nisije onekana sina adabu kumchalenge prof wa Uds mchome, naka degree kangu kaku unga unga.Ni samehe prof mchome na Dr kawambwa.