Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka
huu.
Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.
Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.
Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema,matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea.
Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.
Source: Habari Leo
wenzio wanafikiria ni jinsi gani watakavyo nunua kura kwa hela yako, badala ya kuweka mfumo au msingi wa elimu tzhizo hela wangepeleka kuboresha maabara na kununua vitabu!
Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.
Maneno yako murua kabisa ila ukiwaambia hivyo wanachukiiiiia........siku na zipite hawa watu waondoke.Gharama hizo ni kubwa sana ni lazima Waziri wa Elimu awajibike. Hatuwezi kuwalipia watoto hawa mara ya pili kwasababu ya usingizi wa mtu tuliyempa mamlaka awaelimishe vijana wetu.
Gharama hizo ni kubwa sana ni lazima Waziri wa Elimu awajibike. Hatuwezi kuwalipia watoto hawa mara ya pili kwasababu ya usingizi wa mtu tuliyempa mamlaka awaelimishe vijana wetu.
Mkuu emilwayne wewe bado upo usingizini?:crying:
Ni kweli na ni dhahiri hawa watu hawakua serious katika marking maana nimesikia mwanafunzi wa Green Acres ambaye hakufanya mtihani kaandikiwa kafanya lichaya ya hivyo pia kajaziwa grade nzuri tuu. Je hizo grade mezipatia wapi??? pia solution sio baraza LA MAWAZIRI kujiuzuli maana hata wakijiuzuli bado taifa limeshaangamia.