Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Fanya research utuambie ile Simba Trust inayomiliki 70% ya IPTL ni ya nani.....CCM hamtudanganyi tena....tushachoka
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali

KUWENI NA NIDHAMU BAS HIVI KUANZIA MKURUGENZI WA TAKUKURU NA WENGINE WOTE NYUMA YAKE HAWANA AKILI MPAKA WAWAONEE WATU WAWILI TU NCHI HII KWA LIPI? PASKAL HATA KAMA HAMUPENDI DOLA KUWENI WASTAARABU MPUNGUZE DHARAU JAMANI ACHEN KUTETEA UPUUZ WALOKAMATWA SYO WANASASA WANGELKUWA WANASASA MNESEMA WALMSADA EL LAKN MZEE RUGE SIJAMSIKIA HATA SIKU MOJA WALA HUYO SINGA HANA HATA CHAMA YEYE NI MADEAL TU YA FEDHA
 
Sidhani kama uelewa wako upo sawa juu ya Tegeta Escrow Account.

Suala la escrow ni pesa Tanesco aliyomlipa IPTL wakati wanahisa wa IPTL (Mechmar na VIP) wakiwa na ugomvi.

Ugomvi huo ulisababisha pesa hizo kuwekwa kwenye escrow account mpaka mgogoro utakapotatuliwa.

Kabla ya mgogoro kuisha akatokea PAP na nyaraka za kughushi kwamba yeye amemnunua Mechmar (huku SCB-HK ikipinga kwani ndiyo yenye share certificate kwa mkopo iliyowapa).

PAP kutumia nyaraka za kughushi akalipwa pesa iliyopo kwenye escrow account. VIP akauza hisa zake kwa PAP.

Katika kulipwa fedha kutoka escrow account, BOT ilionyesha wasiwasi na kuomba ushahuri/kibali kutoka AG office na State House na zote zilimpa Go Ahead (hapa hawa utawakuta Stanbic).

BOT iliweka msisitizo kama itatokea mwingine kuja kudai pesa ya escrow account basi PAP alipe.

Sasa uliza Tanesco inadaiwa na SCB-HK kitu gani.. Bado paper trail ya green light ya AG na SH.

Upande mwingine VIP anaweza kushinda kesi lakini si Sethi. Hii yote inategemea tunarudi nyuma mpaka lini
Wew ndio kibubu hujua lolote kuhusu escrow kasome vizuri mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa a/c sio wa wanahisa bali ni watenesco na iptl
 
Unachosema inawezekana kwa kiasi ni sahihi. Lakini siyo sahihi kabisa. Wakati mwingine mtu unapokutwa na mali ya wizi si lazima ushtakiwe; ukishaoneshwa kuwa mali uliyopokea siyo ya haki yako unatakiwa urudishe tu; huwezi kusema hadi mnipeleke mahakamani. Maana huko siyo tu unaweza ukalazimishwa kurudisha lakini ukajikuta unaadhibiwa zaidi ya hivyo.

Kama wana akili nzuri ni kwa maslahi yao wao wenyewe kuamua kurudisha kwani ushahidi wote uko dhidi yao. Lakini wanaweza wakaamua "kubet" kuwa wakienda mahakamani wanaweza kuachiliwa mali hizo... itakula kwao!
Unahangaika sana mkuu. Si tunasemaGA sheria ichukue mkondo wake? Achana na story za betting.
Kama tumeamua kunyooshana basi acha iwe hivyo. Straight line lazima iwe na point mbili tu ili tuanze. Achana kabisa na betting maana options zake ni unlimited anyway...
 
KUWENI NA NIDHAMU BAS HIVI KUANZIA MKURUGENZI WA TAKUKURU NA WENGINE WOTE NYUMA YAKE HAWANA AKILI MPAKA WAWAONEE WATU WAWILI TU NCHI HII KWA LIPI? PASKAL HATA KAMA HAMUPENDI DOLA KUWENI WASTAARABU MPUNGUZE DHARAU JAMANI ACHEN KUTETEA UPUUZ WALOKAMATWA SYO WANASASA WANGELKUWA WANASASA MNESEMA WALMSADA EL LAKN MZEE RUGE SIJAMSIKIA HATA SIKU MOJA WALA HUYO SINGA HANA HATA CHAMA YEYE NI MADEAL TU YA FEDHA
Wewe niaje? Ruge na Ponjoro wanatuhuma ya kula mpunga wa umma, OK? Huku kwenye umma walishirikiana na nani? Simple tu kihivyo mazee!
 
Unachosema inawezekana kwa kiasi ni sahihi. Lakini siyo sahihi kabisa. itakula kwao!
unayoyazungumzia yalishapita, hela ya Chenge 1.6bn Tiba 1.6bn Ngeleja 1.6bn ziliingia kwenye Kampeni na chama kikashinda, labda kamdanganye makengeza ya nyoka, huku bomgo hela ikitoka mkagawana kila mtu na afwe na lwake
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali
Mbona inashangaza kwamba hata wewe Pascal kweli haujui kwamba kwenye hiyo Tegeta Escrow Account, fedha hiyo ilikuwa ni ya nani? Yaani ni kweli kabisa hata wewe hujui maana ya an escrow account? Yaani hata wewe unapaswa kuelimishwa kwa lugha ya ki layman kwamba an escrow account ni kama a joint account, yaani inamilikiwa na watu au parties wawili au zaidi na kwamba kwenye parties hizo TANESCO alikuwa mmoja wao na TANESCO ni shirika la umma. Hivyo kwenye hiyo Tageta account kiasi fulani kilichokuwamo humo zilikuwa ni za umma kupitia shirika lao la umeme.

Wakina Lugemalila na wenzake walipoona kwamba TANESCO wameshinda hiyo kesi iliyosababisha kufunguliwa kwa escrow account, wakaenda kuchukua pesa yote iliyokuwako kwenye account hiyo faster faster kwa mbinu za kitapeli wakisaidiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali, baadhi mawaziri, baadhi ya majaji, viongozi wa dini na wanasiasa wachache wenye ushawishi hata wa kumdanganya rais ili fedha hizo zote wazichukue peke yao na TANESCO iambulie hewa. Wakafanikiwa kuzichota zote na waliofanikisha deal hilo wakawalipa kwa kazi waliofanya. Kila mtu alilipwa kiwango kilichostahili na kazi aliyo play part: wapo waliolipwa million 40, 80 na billion 1.6 (after conversion of the dollar exchange).

Umesema you stand to be corrected. I have tried my best to correct you but I believe you know all this and you were not supposed to stand to be corrected. Then why are you pretending to stand to be corrected?

Jamani tusipende kumuumiza kichwa Mh Magufuri kwa mazuri anayoyafanya. Tumuumize kichwa kwa mabaya anayoyafanya. Tumpongeze na kumuombea kwa Mungu kwa mazuri anayofanya na kumpa nguvu ya kufanya mema kwa taifa letu. Kuwapeleka mahakamani watu hawa ni kitendo kizuri. Kuwachuchumaisha kidogo haipaswi kukuuma.

Wanahabari kuruhusiwa kuwapiga picha maeneo ya mahakama haina ubaya wo wote unaopaswa kuulalamikia. Wengi tu hupigwa picha wakiwa wanaingia au kutoka mahakamani na kuoneshwa kwenye vyombo vya habari. Tumewaona akina Lema, Lissu, watuhumiwa wa madawa ya kulevya, Scorpion, Mla watu - just to mention a few. Kwenye mahakama za kimataifa ndiyo usiombee. Tumewaona akina Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais wake Ruto wakirushwa live kutoka ndani ya mahakama na ulimwengu mzima ukiwaona. Sasa wewe asubuhi ya leo umelalamika sana kwa akina Mzee Lugemalila na Seith wake kupigwa picha kwenye maeneo ya mahakama, kweli watu unazani watakuelewa kweli? Mahakama zinaendesha kesi kwa uwazi. Justice should not only be done but it must be seen to be done. Na to be seen kwa ulimwengu wa sasa wa teknilojia ni pamoja na kuonekana hata kwa kutumia simu ya kiganja cha mkononi ukiwa nyumbani kwako au po pote pale. Hulazimiki hadi uende physically pale Kisutu kuona kinachoendelea. Hivyo vyombo vya habari vina jukumu la kufanikisha jukumu hili la mahakama linalotaka 'justice must be seen to have been done' kwa kutumia tekohama.
 
Hayo maagizo umetoa wewe sio mahakama

why kimbelembele cha kutoa maagizo?

Si watuhumiwa wako mahakamani? si hadi wapatwe na hatia kwanza?
au hizi hukumu ni nje ya mahakama?
Hii ndo thinking capacity ya mtu ambaye ana writings za kutosha hapa jf sasa imagine kule kwetu thinking capacity ikoje, yaani ukikamatwa na dola tayari hukumu hata km dola yenyewe ipo kwenye maigizo
 
Hivi unakumbuka tibaijuka aliambiwa nin jk . Kuwa yeye anaingiziwa bilion moja hata ashtuki


That was a show. Kumbuka Kikwete hakuchukua hatua zozote mpaka baada ya umma kupiga kelele na dili lote kubumbuluka. Halafu sasahivi tunaambiwa tusimseme chochote kwasababu yeye ni Rais mstaafu ilhali ukweli upo wazi kwamba madudu yote haya yanayoibuka sasahivi yana maswali yanayohitaji majibu kutoka kwa Marais waliopita.
 
Tatizo mnafikiri Rais akisema jambo basi ndio limekuwa tu; hata mengine yanayofanywa na Magufuli sasa anaweza akaja Rais mwingine akayatengua na kuyasahihisha au kufutilia mbali. Ndio maana umeona huko US Obama aliondoa vikwazo vingi dhidi ya Cuba kaingia Trump akafutilia mbali...

nakuelewa lakini hapa ni irrelevant.Masuala ya Cuba mimi sitajui,Mkuu. Manaa siweiz kusikiliza CNN kutaka kujua ukweli wa mambo.
Pili,suala la nchi nathani nina mtazamo tofauti kidogo hata pale nisipokubaliana na raisi. Hapa raisi anaitendea haki nchi.

tutapiga kelele katika mambo mengine lakni suala la nchi na mali asili lazima tusimame pamoja. Hapa raisi anasema ukweli.
 
Mojawapo ya mada ambazo zijawahi kuzitolea maoni ya kina ni sakata zima la escrow. Tangu kuibuliwa kwa kashfa hii sikutaka kutoa maoni ya ndani zaidi ya mawazo yangu. Sikufanya hivyo kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni mojawapo ya kashfa za kipumbavu kabisa (foolish) ambazo zimewahi kutokea nchini. Ukilinganisha na ile ya fedha za EPA hii ya escrow ilikuwa ni rahisi sana kuonekana ufisadi wake kwani ilikuwa wazi kwa mtu yeyote yule anayefuatilia. Pili, kashfa hii ilionesha tu jinsi gani tuligoma kujifunza kutoka kashfa nyingine zilizopita. Nimewahi kuandika mwaka 2009 mada ya TEMPLATE OF CORRUPTION.

Katika mada hiyo nilidokeza tu jinsi gani mafisadi wa ndani wanafanya kazi kushirikiana na mafisadi wa nje na with some minor modifications wanatumia njia zile zile kuliibia taifa. Hii ya escrow haikuwa tofauti.

Sote tunajua kina nani walipewa fedha za escrow kwa mtindo wa kuchoteana kidogokidogo. Bahati mbaya wengi walichukulia zoezi lile hasa kuwan ni utakatishaji fedha (money laundering). Katika utakatishaji huu mtu anachukua fedha kwa njia haramu halafu anajaribu kuzibadilisha na kuziingiza kuzifanya ziwe halali; yaani fedha chafu zinasafishwa ili ziwe safi. Mtu anaweza kwenda kujengea nyumba, kuanzishia biashara, kutoa msaada mahali, kusomesha watoto, kutengeneza ajira n.k mwisho wa siku watu watashukuru kwani jamaa badala ya kuzila fedha amezitumia vizuri kwenye jamii.

Kama nilivyosema jana usicheze kamari dhidi ya Magufuli (don't bet against Magufuli) naomba kurudia leo kuwa wale wote waliochukua na kula fedha za 'escrow' wakiamini kuwa wameweza ku 'get away with it' huu kwao ni muda wa kujitafakari haraka. Wasije wakadhania au kuamini kuwa nyavu hii iliyorushwa itawakwepa. Wasije wakajifungia ndani na kuomba kwa miungu yao kuwa 'kikombe hiki kiwaepuke'. Sala zao hazitajibiwa.

Waamue kwa hiari yao wenyewe wazirudishe fedha hizo kabla hawajapewa nafasi ya kuzirudisha zote na adhabu juu (with penalty). Naamini - na nina sababu nzuri ya kuamini hivyo kutokana na kilichowahi kufanyika huko nyuma (predence) - hawa ndugu zetu wataambiwa wazirudishe fedha zote walizozipokea toka mikononi mwa Rugemalira na wenzake. Kama wana chembe ya hekima na uadilifu wajipeleke wenyewe machinjioni.

Kuna sababu kubwa mbili kwanini wanatakiwa wazirudishe:

1. Walionesha kuwa siyo waadilifu kwa kupokea fedha hizi. Wote waliopokea fedha za escrow walipaswa kugundua mara moja kuwa "something is very wrong". Karibu wote ni wasomi na wengi wao ni watumishi wa umma au wa jamii. Baada ya taarifa za kuwa waligawiwa mamilioni ya fedha kwa makundi makundi na mtu ambaye anatajwa kuhusika na kashfa ya IPTL ambayo ilikuwa inajulikana kwa muda mrefu basi watu hawa wote kama wangekuwa na uadilifu hata kidogo tu wangesema hizi fedha za moto!

Badala yake katika njaa zao na ukosefu wao wa uadilifu (lack of integrity) wakazipokea kwa mikono mitupu na kila mmoja akijielezea kwanini anapaswa kubaki nazo. Unapokea fedha vipi wakati unaona majina ya watu toka TRA, Ikulu, wabunge, majaji, viongozi wa dini na bado ukadhani uko salama?

2. Tangu wapokee fedha hizo miaka kadhaa nyuma ndugu zetu hawa nina uhakika kama kuzila walishazila na kama kuzifanyia shughuli wameshafanyia shughuli zao mbalimbali. Lakini wamekula kisicho chao na wameshiriki kula visivyoruhusiwa kwao. Walifanya hivyo kwa sababu waliamini kabisa kuwa "they got away with it". Kwamba, wakija kuulizwa wao watasema tu "si tumepewa jamani kosa letu ni nini?". Tatizo ni kuwa hawa wote ni viongozi ambao wanajua kabisa au walipaswa kujua shetani hana zawadi ya bure (the devil has no free gifts).

Ukikuta hela imeingia kwenye akaunti yako ambayo hujui imetokana na nini au kwanini usikimbilie kuitumia tu. Mwezi Machi 2012 huko Philadelphia kijana mmoja wa miaka 22 alijikuta ameingiziwa kwenye akaunti yake dola 70,000 wakati yeye alikuwa na dola 35 humo. Jamaa akajua amebarikiwa akawa anaenda kwenye ATM kutoa hela, kwa karibu wiki mbili hivi akawa ametumia dola 2000! Benki ikagundua kosa na jamaa akaja kukamatwa na polisi kwa kupokea na kutumia fedha za wizi!

Huko Georgia kijana wa miaka 18 alijikuta ameingiziwa dola 30,000 kwa makosa kwa vile jina lake na ambaye alikuwa anatakiwa kuingizwa fedha yalifanana na teller alichanganya tu. Kijana huyo akaamua kuzila hizo fedha, aliposhtakiwa na kukutwa na hatia na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka 10 na kutakiwa kurudisha fedha alizotumia.

Sasa ndugu zetu hawa wote maafisa wa umma, unapokea vipi fedha kwa mamilioni bila kushtuka isipokuwa kama ulikuwa umeshajua fedha zinakuja na unatakiwa uchangamkie. Hisia zangu ni kuwa sehemu ya fedha hizo zilirudishwa kwa kina Ruge au watu wengine (ikiwa sehemu ya utakatishaji) lakini sehemu yake ilibakia na kuliwa na waliokubali akaunti zao zitumiwe.

Huu ni ufisadi tu.

Sasa, hawa ndugu zetu wasome alama za nyakati (signs of the times); hawako salama, Mali zao haziko salama, uhuru wao hauko salama, na wasipoangalia familia zao zitajikuta haziko salama na kila walichodhania ni kinga kwao hakipo tena. Walikingiwa kifua na utawala wa Kikwete, lakini there is a new sherrif in town and he ain't bulls@$!!g!

Ili labda yasiwakute:
1. Ombeni utaratibu wa kurudisha fedha zile wenyewe kabla hawajawajia. What you gonna do when they come for you!

2.
Na kama mna utimamu andikeni cheki mzirudishe fedha hizo kwa serikali iziweke kwenye mfuko maalum ambapo zitakusanywa.

3.
Serikali inakuja dhidi yenu kuzirudisha fedha hizo na adhabu juu. Jiandaeni kwan labda... labda... labda.. mnaweza MSIPIGISHWE MAGOTI NA KUCHUCHUMAISHWA!


mmm

Wanadhani kumsifia Rais JPM ndio jibu kama ilivyo kuwa kawaida yao. Kiila zama na nyakati zake!
 
Wakina Lugemalila na wenzake walipoona kwamba TANESCO wameshinda hiyo kesi iliyosababisha kufunguliwa kwa escrow account, wakaenda kuchukua pesa yote iliyokuwako kwenye account hiyo faster faster kwa mbinu za kitapeli wakisaidiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali, baadhi mawaziri, baadhi ya majaji, viongozi wa dini na wanasiasa wachache wenye ushawishi hata wa kumdanganya rais ili fedha hizo zote wazichukue peke yao na TANESCO iambulie hewa. Wakafanikiwa kuzichota zote na waliofanikisha deal hilo wakawalipa kwa kazi waliofanya. Kila mtu alilipwa kiwango kilichostahili na kazi aliyo play part: wapo waliolipwa million 40, 80 na billion 1.6 (after conversion of the dollar exchange).

Umesema you stand to be corrected. I have tried my best to correct you but I believe you know all this and you were not supposed to stand to be corrected. Then why are you pretending to stand to be corrected?

Well put, I couldn't have said it better myself. Ila sidhani kama hawaelewi. Ni kwamba hawataki kuelewa.
 
Wewe niaje? Ruge na Ponjoro wanatuhuma ya kula mpunga wa umma, OK? Huku kwenye umma walishirikiana na nani? Simple tu kihivyo mazee!
KASOME CRIMINAL INVESTIGATION UTAJUA KUWA UKAMATAJI UNAANZA NA ALIYEVUNJA MLANGO KISHA ALIYEMWAZIMA KIVUNJIO AU BUNDUKI, SUBIRI HATA HAWA NAAMNI HUKUTEGEMEA KAMA WATAKAMATWA, NANI ALITEGEMEA PONJORO ATALALA LUPANGO? BWANA YULE ALISHASEMA HAWAKAMATIKI WAKATI DOLA IKO MIKONONI MWAKE?
 
Well put, I couldn't have said it better myself. Ila sidhani kama hawaelewi. Ni kwamba hawataki kuelewa.
Mimi sidhani kuwa hawataki kuelewa. Wana lao jambo. Labda wanaweza kuwa walifaidika na huo waliouita wema wa matapeli hawa, au wanataka kiki ya kisiasa au tu hawamtakii mema rais wetu hivyo kumpigia hizo kelele za 'Huyoo! huyooo! amepoteaa!' alizotabiri Mwl. Nyerere ili rais angeuke nyuma na kuwa jiwe.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali

Pasko katika suala la escrow Umekuwa mtetezi mzuri sana wa Rugemarila na seth..Hongera

Zile pesa walikuwa wanagawa za nini? kwa minajili ipi?
 
kiongozi wao Jk alizisafisha na kusema pesa sio za serikali.Unataka zisafishwe mara ngapi?Hvyo,walikuwa na haki zote kupokea.Tuanze kwanza na kichwa then tutashuka chini taratibu.
Kaka usiwe na ubongo nzito kama gundi....kama ingekuwa sio hela ya serekali...wale wazee wasingepiga goti pale kisutu
 
Sioni ni kwa vipi serikali ifungue shauri la hivyo wakati serikali hiyohiyo imeshatoa msimamo kuwa hizo pesa si za serikali bali ni za IPTL na wadau wengine. Msimamo wa kisheria wa serikali kupitia kwa mwanasheria wake mkuu imeshatoa msimamo wake kupitia kwa Jaji Werema kuwa hizo si pesa zake bali ni za IPTL!. Serikali ikienda mahakamani kuzidai hizo pesa itabidi iadress kwa nini misimamo yake ya kisheria inabadirikabadirika

Tutofautishe mfano uliotoa wa foreign policy issues na Legal issues.
Inaonekana ulipata mgao ww....alafu inaonekana ww ni mccm....maana ndio waliopiga hiyo dili....mjiandae kuyamba
 
Back
Top Bottom