Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,251
Reaction score
44,586
Mojawapo ya mada ambazo zijawahi kuzitolea maoni ya kina ni sakata zima la escrow. Tangu kuibuliwa kwa kashfa hii sikutaka kutoa maoni ya ndani zaidi ya mawazo yangu. Sikufanya hivyo kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni mojawapo ya kashfa za kipumbavu kabisa (foolish) ambazo zimewahi kutokea nchini. Ukilinganisha na ile ya fedha za EPA hii ya escrow ilikuwa ni rahisi sana kuonekana ufisadi wake kwani ilikuwa wazi kwa mtu yeyote yule anayefuatilia. Pili, kashfa hii ilionesha tu jinsi gani tuligoma kujifunza kutoka kashfa nyingine zilizopita. Nimewahi kuandika mwaka 2009 mada ya TEMPLATE OF CORRUPTION.

Katika mada hiyo nilidokeza tu jinsi gani mafisadi wa ndani wanafanya kazi kushirikiana na mafisadi wa nje na with some minor modifications wanatumia njia zile zile kuliibia taifa. Hii ya escrow haikuwa tofauti.

Sote tunajua kina nani walipewa fedha za escrow kwa mtindo wa kuchoteana kidogokidogo. Bahati mbaya wengi walichukulia zoezi lile hasa kuwan ni utakatishaji fedha (money laundering). Katika utakatishaji huu mtu anachukua fedha kwa njia haramu halafu anajaribu kuzibadilisha na kuziingiza kuzifanya ziwe halali; yaani fedha chafu zinasafishwa ili ziwe safi. Mtu anaweza kwenda kujengea nyumba, kuanzishia biashara, kutoa msaada mahali, kusomesha watoto, kutengeneza ajira n.k mwisho wa siku watu watashukuru kwani jamaa badala ya kuzila fedha amezitumia vizuri kwenye jamii.

Kama nilivyosema jana usicheze kamari dhidi ya Magufuli (don't bet against Magufuli) naomba kurudia leo kuwa wale wote waliochukua na kula fedha za 'escrow' wakiamini kuwa wameweza ku 'get away with it' huu kwao ni muda wa kujitafakari haraka. Wasije wakadhania au kuamini kuwa nyavu hii iliyorushwa itawakwepa. Wasije wakajifungia ndani na kuomba kwa miungu yao kuwa 'kikombe hiki kiwaepuke'. Sala zao hazitajibiwa.

Waamue kwa hiari yao wenyewe wazirudishe fedha hizo kabla hawajapewa nafasi ya kuzirudisha zote na adhabu juu (with penalty). Naamini - na nina sababu nzuri ya kuamini hivyo kutokana na kilichowahi kufanyika huko nyuma (predence) - hawa ndugu zetu wataambiwa wazirudishe fedha zote walizozipokea toka mikononi mwa Rugemalira na wenzake. Kama wana chembe ya hekima na uadilifu wajipeleke wenyewe machinjioni.

Kuna sababu kubwa mbili kwanini wanatakiwa wazirudishe:

1. Walionesha kuwa siyo waadilifu kwa kupokea fedha hizi. Wote waliopokea fedha za escrow walipaswa kugundua mara moja kuwa "something is very wrong". Karibu wote ni wasomi na wengi wao ni watumishi wa umma au wa jamii. Baada ya taarifa za kuwa waligawiwa mamilioni ya fedha kwa makundi makundi na mtu ambaye anatajwa kuhusika na kashfa ya IPTL ambayo ilikuwa inajulikana kwa muda mrefu basi watu hawa wote kama wangekuwa na uadilifu hata kidogo tu wangesema hizi fedha za moto!

Badala yake katika njaa zao na ukosefu wao wa uadilifu (lack of integrity) wakazipokea kwa mikono mitupu na kila mmoja akijielezea kwanini anapaswa kubaki nazo. Unapokea fedha vipi wakati unaona majina ya watu toka TRA, Ikulu, wabunge, majaji, viongozi wa dini na bado ukadhani uko salama?

2. Tangu wapokee fedha hizo miaka kadhaa nyuma ndugu zetu hawa nina uhakika kama kuzila walishazila na kama kuzifanyia shughuli wameshafanyia shughuli zao mbalimbali. Lakini wamekula kisicho chao na wameshiriki kula visivyoruhusiwa kwao. Walifanya hivyo kwa sababu waliamini kabisa kuwa "they got away with it". Kwamba, wakija kuulizwa wao watasema tu "si tumepewa jamani kosa letu ni nini?". Tatizo ni kuwa hawa wote ni viongozi ambao wanajua kabisa au walipaswa kujua shetani hana zawadi ya bure (the devil has no free gifts).

Ukikuta hela imeingia kwenye akaunti yako ambayo hujui imetokana na nini au kwanini usikimbilie kuitumia tu. Mwezi Machi 2012 huko Philadelphia kijana mmoja wa miaka 22 alijikuta ameingiziwa kwenye akaunti yake dola 70,000 wakati yeye alikuwa na dola 35 humo. Jamaa akajua amebarikiwa akawa anaenda kwenye ATM kutoa hela, kwa karibu wiki mbili hivi akawa ametumia dola 2000! Benki ikagundua kosa na jamaa akaja kukamatwa na polisi kwa kupokea na kutumia fedha za wizi!

Huko Georgia kijana wa miaka 18 alijikuta ameingiziwa dola 30,000 kwa makosa kwa vile jina lake na ambaye alikuwa anatakiwa kuingizwa fedha yalifanana na teller alichanganya tu. Kijana huyo akaamua kuzila hizo fedha, aliposhtakiwa na kukutwa na hatia na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka 10 na kutakiwa kurudisha fedha alizotumia.

Sasa ndugu zetu hawa wote maafisa wa umma, unapokea vipi fedha kwa mamilioni bila kushtuka isipokuwa kama ulikuwa umeshajua fedha zinakuja na unatakiwa uchangamkie. Hisia zangu ni kuwa sehemu ya fedha hizo zilirudishwa kwa kina Ruge au watu wengine (ikiwa sehemu ya utakatishaji) lakini sehemu yake ilibakia na kuliwa na waliokubali akaunti zao zitumiwe.

Huu ni ufisadi tu.

Sasa, hawa ndugu zetu wasome alama za nyakati (signs of the times); hawako salama, Mali zao haziko salama, uhuru wao hauko salama, na wasipoangalia familia zao zitajikuta haziko salama na kila walichodhania ni kinga kwao hakipo tena. Walikingiwa kifua na utawala wa Kikwete, lakini there is a new sherrif in town and he ain't bulls@$!!g!

Ili labda yasiwakute:
1. Ombeni utaratibu wa kurudisha fedha zile wenyewe kabla hawajawajia. What you gonna do when they come for you!

2.
Na kama mna utimamu andikeni cheki mzirudishe fedha hizo kwa serikali iziweke kwenye mfuko maalum ambapo zitakusanywa.

3.
Serikali inakuja dhidi yenu kuzirudisha fedha hizo na adhabu juu. Jiandaeni kwan labda... labda... labda.. mnaweza MSIPIGISHWE MAGOTI NA KUCHUCHUMAISHWA!

mmm
 
wale wote waliochukua na kula fedha za EPA wakiamini kuwa wameweza ku 'get away with it' huu kwao ni muda wa kujitafakari haraka. Wasije wakadhania au kuamini kuwa nyavu hii iliyorushwa itawakwepa. Wasije wakajifungia ndani na kuomba kwa miungu yao kuwa 'kikombe hiki kiwaepuke'. Sala zao hazitajibiwa.

Waamue kwa hiari yao wenyewe wazirudishe fedha hizo kabla hawajapewa nafasi ya kuzirudisha zote na adhabu juu (with penalty). Naamini - na nina sababu nzuri ya kuamini hivyo kutokana na kilichowahi kufanyika huko nyuma (predence) - hawa ndugu zetu wataambiwa wazirudishe fedha zote walizozipokea toka mikononi mwa Rugemalira na wenzake. Kama wana chembe ya hekima na uadilifu wajipeleke wenyewe machinjioni.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali
 
Kaka Tanzania inaendeshwa kwa kufuata sheria, Ni mpaka serikali ifungue shauri mahakamani kuwashitaki wanufaika na ikishinda ndo itakuwa na haki wazilipe, Otherwise Serikali haina justification ya kisheria ya kuwaharass hawa watu!, na ikifanya hivyo kibabe itajikuta inashitakiwa na kujikita inalipa damages kwa hatua za kibabe kinyume cha sheria!.
 
Kashalewa 'Magufuli'
anafikiri nchi inaendeshwa tu kwa amri bila sheria
 
kiongozi wao Jk alizisafisha na kusema pesa sio za serikali.Unataka zisafishwe mara ngapi?Hvyo,walikuwa na haki zote kupokea.Tuanze kwanza na kichwa then tutashuka chini taratibu.

Tatizo mnafikiri Rais akisema jambo basi ndio limekuwa tu; hata mengine yanayofanywa na Magufuli sasa anaweza akaja Rais mwingine akayatengua na kuyasahihisha au kufutilia mbali. Ndio maana umeona huko US Obama aliondoa vikwazo vingi dhidi ya Cuba kaingia Trump akafutilia mbali...
 
Wote waliopata fedha kwa udanganyifu WARUDISHE PESA HARAKA KABLA RUNGU LA CHATO KUWASHUKIA
 
Kaka Tanzania inaendeshwa kwa kufuata sheria, Ni mpaka serikali ifungue shauri mahakamani kuwashitaki wanufaika na ikishinda ndo itakuwa na haki wazilipe, Otherwise Serikali haina justification ya kisheria ya kuwaharass hawa watu!, na ikifanya hivyo kibabe itajikuta inashitakiwa na kujikita inalipa damages kwa hatua za kibabe kinyume cha sheria!.
Unachosema inawezekana kwa kiasi ni sahihi. Lakini siyo sahihi kabisa. Wakati mwingine mtu unapokutwa na mali ya wizi si lazima ushtakiwe; ukishaoneshwa kuwa mali uliyopokea siyo ya haki yako unatakiwa urudishe tu; huwezi kusema hadi mnipeleke mahakamani. Maana huko siyo tu unaweza ukalazimishwa kurudisha lakini ukajikuta unaadhibiwa zaidi ya hivyo.

Kama wana akili nzuri ni kwa maslahi yao wao wenyewe kuamua kurudisha kwani ushahidi wote uko dhidi yao. Lakini wanaweza wakaamua "kubet" kuwa wakienda mahakamani wanaweza kuachiliwa mali hizo... itakula kwao!
 
Kidikteta sawa; ila kisheria sidhani kama ndoto zako Mwanakijiji zitatimia. Hakuna "paper trail" kwa wizi wote mkubwa ulifanyika huko nyuma. Kikwete oversaw all the theft but your messiah Magufuli won't dare to ask him where the records are. So, this is likely to be all show, but true justice won't be served.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali
Ndio sasabu wamepelekwa mahakamani, wakamweleze Mheshimiwa jaji kuwa ni fedha za watu binafsi.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, I know you ment fedha za escrow lakini ukaandika ni fedha za EPA.

Pili I stand to be corrected, Fedha za Escrow sio fedha za umma!. Hawa jamaa wanaonewa bure na karma iko juu yao!.

Mtu pekee aliyeibiwa na kudhulumiwa ni Stan Chart HKN.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali
Asante bosi nimesahihisha pale juu. Tatizo ni kuwa labda kuna watu hawakuelewa maana ya 'escrow'. Hapa Marekani ukinunua nyumba kwa mkopo wa benki mojawapo ya fomu unazojaza zinaitwa "escrow form". Lengo la fomu hii ni kuwa unakubali akaunti maalum ifunguliwe ambapo fedha za kodi ya ardhi (property tax) zitaingizwa huko kila mwezi na mara moja kwa mwaka zitalipwa kwa mji au jiji unaloishi. Fedha hizi za "escrow" unazilipa kwa mtoaji wako mkopo (benki au taasisi nyingine ya mikopo) na inajumuishwa kwenye malipo yako ya mwezi (mortgage payment). Wao (benki) wanakata chao na wanakata ile nyingine ya ardhi na kuiweka kwenye hiyo akaunti.

Sasa fedha hizo zinakaa huko kila mwezi na kila mwaka; kukitoa mabadiliko yoyote ya kisheria kwa mfano ikaonekana kwa mwaka umelipa fedha nyingi kwenye hiyo escrow kuliko kodi yenyewe ya ardhi basi kampuni ya escrow inakurudishia kile kilichozidi.

Suala la escrow yetu kwa sehemu ilikuwa hivi; tatizo ni kuwa mwisho wa siku kulikuwa na fedha yetu na fedha ambayo ilitakiwa ilipwe kule kwa kina Singh. Hiyo ilitakiwa ifanyike baada ya hesabu zote kupigwa na kuonesha ni kipi chetu na kipi kiende kule. Tatizo ni kuwa wao wakachukua chote bila kujali kuwa sehemu yake siyo yao.. hapo ndipo ufisadi ulipo.
 
Back
Top Bottom