Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Waliobarikiwa Fedha za 'Escrow' Wazirudishe Mapema.. Labda.. na Labda...

Pascal Mayalla sasa unakiri kwamba fedha za escrow ni za Tanesco pamoja na IPTL then unapinga tena kwamba fedha hizo sio za Umma.

Hebu tujuze TANESCO sio Mali ya Umma?
 
Naomba nikupe tu kaushauri kadogo maana naona mapenzi yamekupofusha mzee mwenzangu...kumbuka mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichana (thanks to the late Edouard Masengo aka Masengo Edward aka "Katiti" 1933-2003)

Mchimba Kaburi huweza kujikuta anaingia mwenyewe...je umejiuliza sehemu kubwa ya mgao wa ESCROW ilitumikaje? Je una habari ya uwezekano wa malengo ya ESCROW mwaka 2014 kutotofautiana sana na malengo ya EPA mwaka 2004?

Kama Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepita, ingekuwa rahisi kufukua makaburi lakini wajanja wetu wakagutuka mapema na kahakikisha inazimwa, unajua kwa nini? Ni sanaa ya kuendeleza vita dhidi ya nyoka wa kufugwa kwa kumponda mkia.

Endelea kuota mzee mwenzangu...!
 
Mojawapo ya mada ambazo zijawahi kuzitolea maoni ya kina ni sakata zima la escrow. Tangu kuibuliwa kwa kashfa hii sikutaka kutoa maoni ya ndani zaidi ya mawazo yangu. Sikufanya hivyo kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni mojawapo ya kashfa za kipumbavu kabisa (foolish) ambazo zimewahi kutokea nchini. Ukilinganisha na ile ya fedha za EPA hii ya escrow ilikuwa ni rahisi sana kuonekana ufisadi wake kwani ilikuwa wazi kwa mtu yeyote yule anayefuatilia. Pili, kashfa hii ilionesha tu jinsi gani tuligoma kujifunza kutoka kashfa nyingine zilizopita. Nimewahi kuandika mwaka 2009 mada ya TEMPLATE OF CORRUPTION.

Katika mada hiyo nilidokeza tu jinsi gani mafisadi wa ndani wanafanya kazi kushirikiana na mafisadi wa nje na with some minor modifications wanatumia njia zile zile kuliibia taifa. Hii ya escrow haikuwa tofauti.

Sote tunajua kina nani walipewa fedha za escrow kwa mtindo wa kuchoteana kidogokidogo. Bahati mbaya wengi walichukulia zoezi lile hasa kuwan ni utakatishaji fedha (money laundering). Katika utakatishaji huu mtu anachukua fedha kwa njia haramu halafu anajaribu kuzibadilisha na kuziingiza kuzifanya ziwe halali; yaani fedha chafu zinasafishwa ili ziwe safi. Mtu anaweza kwenda kujengea nyumba, kuanzishia biashara, kutoa msaada mahali, kusomesha watoto, kutengeneza ajira n.k mwisho wa siku watu watashukuru kwani jamaa badala ya kuzila fedha amezitumia vizuri kwenye jamii.

Kama nilivyosema jana usicheze kamari dhidi ya Magufuli (don't bet against Magufuli) naomba kurudia leo kuwa wale wote waliochukua na kula fedha za 'escrow' wakiamini kuwa wameweza ku 'get away with it' huu kwao ni muda wa kujitafakari haraka. Wasije wakadhania au kuamini kuwa nyavu hii iliyorushwa itawakwepa. Wasije wakajifungia ndani na kuomba kwa miungu yao kuwa 'kikombe hiki kiwaepuke'. Sala zao hazitajibiwa.

Waamue kwa hiari yao wenyewe wazirudishe fedha hizo kabla hawajapewa nafasi ya kuzirudisha zote na adhabu juu (with penalty). Naamini - na nina sababu nzuri ya kuamini hivyo kutokana na kilichowahi kufanyika huko nyuma (predence) - hawa ndugu zetu wataambiwa wazirudishe fedha zote walizozipokea toka mikononi mwa Rugemalira na wenzake. Kama wana chembe ya hekima na uadilifu wajipeleke wenyewe machinjioni.

Kuna sababu kubwa mbili kwanini wanatakiwa wazirudishe:

1. Walionesha kuwa siyo waadilifu kwa kupokea fedha hizi. Wote waliopokea fedha za escrow walipaswa kugundua mara moja kuwa "something is very wrong". Karibu wote ni wasomi na wengi wao ni watumishi wa umma au wa jamii. Baada ya taarifa za kuwa waligawiwa mamilioni ya fedha kwa makundi makundi na mtu ambaye anatajwa kuhusika na kashfa ya IPTL ambayo ilikuwa inajulikana kwa muda mrefu basi watu hawa wote kama wangekuwa na uadilifu hata kidogo tu wangesema hizi fedha za moto!

Badala yake katika njaa zao na ukosefu wao wa uadilifu (lack of integrity) wakazipokea kwa mikono mitupu na kila mmoja akijielezea kwanini anapaswa kubaki nazo. Unapokea fedha vipi wakati unaona majina ya watu toka TRA, Ikulu, wabunge, majaji, viongozi wa dini na bado ukadhani uko salama?

2. Tangu wapokee fedha hizo miaka kadhaa nyuma ndugu zetu hawa nina uhakika kama kuzila walishazila na kama kuzifanyia shughuli wameshafanyia shughuli zao mbalimbali. Lakini wamekula kisicho chao na wameshiriki kula visivyoruhusiwa kwao. Walifanya hivyo kwa sababu waliamini kabisa kuwa "they got away with it". Kwamba, wakija kuulizwa wao watasema tu "si tumepewa jamani kosa letu ni nini?". Tatizo ni kuwa hawa wote ni viongozi ambao wanajua kabisa au walipaswa kujua shetani hana zawadi ya bure (the devil has no free gifts).

Ukikuta hela imeingia kwenye akaunti yako ambayo hujui imetokana na nini au kwanini usikimbilie kuitumia tu. Mwezi Machi 2012 huko Philadelphia kijana mmoja wa miaka 22 alijikuta ameingiziwa kwenye akaunti yake dola 70,000 wakati yeye alikuwa na dola 35 humo. Jamaa akajua amebarikiwa akawa anaenda kwenye ATM kutoa hela, kwa karibu wiki mbili hivi akawa ametumia dola 2000! Benki ikagundua kosa na jamaa akaja kukamatwa na polisi kwa kupokea na kutumia fedha za wizi!

Huko Georgia kijana wa miaka 18 alijikuta ameingiziwa dola 30,000 kwa makosa kwa vile jina lake na ambaye alikuwa anatakiwa kuingizwa fedha yalifanana na teller alichanganya tu. Kijana huyo akaamua kuzila hizo fedha, aliposhtakiwa na kukutwa na hatia na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa miaka 10 na kutakiwa kurudisha fedha alizotumia.

Sasa ndugu zetu hawa wote maafisa wa umma, unapokea vipi fedha kwa mamilioni bila kushtuka isipokuwa kama ulikuwa umeshajua fedha zinakuja na unatakiwa uchangamkie. Hisia zangu ni kuwa sehemu ya fedha hizo zilirudishwa kwa kina Ruge au watu wengine (ikiwa sehemu ya utakatishaji) lakini sehemu yake ilibakia na kuliwa na waliokubali akaunti zao zitumiwe.

Huu ni ufisadi tu.

Sasa, hawa ndugu zetu wasome alama za nyakati (signs of the times); hawako salama, Mali zao haziko salama, uhuru wao hauko salama, na wasipoangalia familia zao zitajikuta haziko salama na kila walichodhania ni kinga kwao hakipo tena. Walikingiwa kifua na utawala wa Kikwete, lakini there is a new sherrif in town and he ain't bulls@$!!g!

Ili labda yasiwakute:
1. Ombeni utaratibu wa kurudisha fedha zile wenyewe kabla hawajawajia. What you gonna do when they come for you!

2.
Na kama mna utimamu andikeni cheki mzirudishe fedha hizo kwa serikali iziweke kwenye mfuko maalum ambapo zitakusanywa.

3.
Serikali inakuja dhidi yenu kuzirudisha fedha hizo na adhabu juu. Jiandaeni kwan labda... labda... labda.. mnaweza MSIPIGISHWE MAGOTI NA KUCHUCHUMAISHWA!


mmm
....na Mkwere pia atapigwa Magoti?
maana huyu aliutangazia UMMA kwamba Bwana KALA SINGH? na Mwenzie ule Mzigo waliokuwa wanagawa ulikuwa wao anyaway ngoja tuone mwisho wa hii NCHI... umefanikiwa kuona Charge sheet yao huko Mahakamani?
 
Moral values....mpaka maaskofu. And what about absolution?
 
Jinsi singasinga alivyopiga magoti najua na hawa watapiga magoti tu. Na leo kasema kule kibaha ambaye hakuelewa basi ajiandaae.
....ila kutawala wadanganyika Raha sana maana maneno matupu watu wanaingia barababarani kutukuza.... ile Kesi Mahakama isipofika Msoga ni kupotezeana muda
 
Hayo maagizo umetoa wewe sio mahakama

why kimbelembele cha kutoa maagizo?

Si watuhumiwa wako mahakamani? si hadi wapatwe na hatia kwanza?
au hizi hukumu ni nje ya mahakama?
....nakwambia NCHI hii rahisi sana kutawala Wee wape maneno matupu.... Shangwe kila mahali...
ukitaka uone tunafanya Utani na hii VITA...hati za MASHTAKA... zinaonyesha wamepewa HELA na watu wa Serikali lkn hawatajwi
 
Naomba nikupe tu kaushauri kadogo maana naona mapenzi yamekupofusha mzee mwenzangu...kumbuka mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichana (thanks to the late Edward Masengo aka Masengo Edward aka "Katiti" 1933-2003)

Mchimba Kaburi huweza kujikuta anaingia mwenyewe...je umejiuliza sehemu kubwa ya mgao wa ESCROW ilitumikaje? Je una habari ya uwezekano wa malengo ya ESCROW mwaka 2014 kutotofautiana sana na malengo ya EPA mwaka 2004?

Kama Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepita, ingekuwa rahisi kufukua makaburi lakini wajanja wetu wakagutuka mapema na kahakikisha inazimwa, unajua kwa nini? Ni sanaa ya kuendeleza vita dhidi ya nyoka wa kufugwa kwa kumponda mkia.

Endelea kuota mzee mwenzangu...!
duu ina maana ilikuwa Kwa ajili ya kampeni?
 
Kama Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepita, ingekuwa rahisi kufukua makaburi
Hivi ile Rasimu ya serikali Tatu inatofauti gani katiba inayopendekezwa.. Tofauti kubwa ni idadi ya serikali, wabunge kutokuwa mawaziri, na Elimu ya wabunge, mengine yote ni ya kawaida.. Wabongo bana, ishu sio katiba.. Ishu ni uadilfu, ukiwa na kiongozi alieingia kwa Rushwa, hakuna cha katiba wala nini
 
There you are Mkuu Mzee Mwanakijiji. Escrow ni account ya custodian tuu wakati wa mgogoro, wenye pesa ni Tanesco na IPTL, the custodian ni BOT. Ikumbukwe fedha za escrow ni capacity charges only lakini Tanesco bado ilikuwa inadaiwa utility. Hivyo walioandika barua ku authorise BOT kulipa fedha zote PAP ni serikali kwa niaba ya Tanesco. Hivyo fedha zote ni za PAP sio fedha za umma.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali

Kama hizo pesa siyo za Umma, je ni za PAP au IPTL?
 
Suala la escrow yetu kwa sehemu ilikuwa hivi; tatizo ni kuwa mwisho wa siku kulikuwa na fedha yetu na fedha ambayo ilitakiwa ilipwe kule kwa kina Singh. Hiyo ilitakiwa ifanyike baada ya hesabu zote kupigwa na kuonesha ni kipi chetu na kipi kiende kule. Tatizo ni kuwa wao wakachukua chote bila kujali kuwa sehemu yake siyo yao.. hapo ndipo ufisadi ulipo.

Sidhani kama uelewa wako upo sawa juu ya Tegeta Escrow Account.

Suala la escrow ni pesa Tanesco aliyomlipa IPTL wakati wanahisa wa IPTL (Mechmar na VIP) wakiwa na ugomvi.

Ugomvi huo ulisababisha pesa hizo kuwekwa kwenye escrow account mpaka mgogoro utakapotatuliwa.

Kabla ya mgogoro kuisha akatokea PAP na nyaraka za kughushi kwamba yeye amemnunua Mechmar (huku SCB-HK ikipinga kwani ndiyo yenye share certificate kwa mkopo iliyowapa).

PAP kutumia nyaraka za kughushi akalipwa pesa iliyopo kwenye escrow account. VIP akauza hisa zake kwa PAP.

Katika kulipwa fedha kutoka escrow account, BOT ilionyesha wasiwasi na kuomba ushahuri/kibali kutoka AG office na State House na zote zilimpa Go Ahead (hapa hawa utawakuta Stanbic).

BOT iliweka msisitizo kama itatokea mwingine kuja kudai pesa ya escrow account basi PAP alipe.

Sasa uliza Tanesco inadaiwa na SCB-HK kitu gani.. Bado paper trail ya green light ya AG na SH.

Upande mwingine VIP anaweza kushinda kesi lakini si Sethi. Hii yote inategemea tunarudi nyuma mpaka lini
 
Mimi naona maigizo tu hivi tuache unafiki jk alisema pesa sio za umma naye ana mgao wake na mkuu kasema wasigushe wastaafu sasa kuna kesi hapo
 
Kidikteta sawa; ila kisheria sidhani kama ndoto zako Mwanakijiji zitatimia. Hakuna "paper trail" kwa wizi wote mkubwa ulifanyika huko nyuma. Kikwete oversaw all the theft but your messiah Magufuli won't dare to ask him where the records are. So, this is likely to be all show, but true justice won't be served.
Hivi unakumbuka tibaijuka aliambiwa nin jk . Kuwa yeye anaingiziwa bilion moja hata ashtuki
 
Sioni ni kwa vipi serikali ifungue shauri la hivyo wakati serikali hiyohiyo imeshatoa msimamo kuwa hizo pesa si za serikali bali ni za IPTL na wadau wengine. Msimamo wa kisheria wa serikali kupitia kwa mwanasheria wake mkuu imeshatoa msimamo wake kupitia kwa Jaji Werema kuwa hizo si pesa zake bali ni za IPTL!. Serikali ikienda mahakamani kuzidai hizo pesa itabidi iadress kwa nini misimamo yake ya kisheria inabadirikabadirika

Tutofautishe mfano uliotoa wa foreign policy issues na Legal issues.
Kwani kama pesa zilichezewa mchezo kuna ugumu gani kufanya kuwa si za serikali ili kuficha uchafu? Hapa kuna harufu kubwa sana na tutayaona mengi ndiyo maana mkulu leo hakugusa kabisa hii habari hataki ionekane anaingilia uhuru wa mahakama. wenye macho waone.
 
There you are Mkuu Mzee Mwanakijiji. Escrow ni account ya custodian tuu wakati wa mgogoro, wenye pesa ni Tanesco na IPTL, the custodian ni BOT. Ikumbukwe fedha za escrow ni capacity charges only lakini Tanesco bado ilikuwa inadaiwa utility. Hivyo walioandika barua ku authorise BOT kulipa fedha zote PAP ni serikali kwa niaba ya Tanesco. Hivyo fedha zote ni za PAP sio fedha za umma.

Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !

Paskali
lakini mkuu si tuliambiwa huyu mhindi alifanya ujanja ujanja kwa mtaji wake wa pesa kiduchu
 
Escrow account ni ring fencing of money ziko kwenye fence sio za Tanesco wala sio za IPTL. Baada ya mgogoro kumalizika, serikali ndio ilitoa go ahead fedha zi change hands from no man's money to IPTL.

Kwa vile ndani ya escrow some of the money ni VAT ambapo IPTL was TRA collecting agents ambaye ni VAT registered, lakini BOT ikazilipa kwa PAP ambaye sio TRA, VAT collecting agents hivyo VAT yote iliyokuwa ndani ya escrow imeibiwa na PAP ila kwa sababu Tanesco wanadaiwa na IPTL fedha za utilities ambazo ni nyingi zaidi ya hiyo VAT, then PAP will make it good kwa ama kwa ku register VAT na kulipa, au ku deduct VAT equivalent na kuwaacha Tanesco wafanye remittance.

The bottom line ni fedha za Escrow sio fedha za umma!.
Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !.

Paskali
Paskali na wewe unakubali kabisa kiini macho kama hicho mpaka watu wagawane pesa kama korosho? Kweli zile pesa kama zilikua wao wana wema gani kugawa vile kama njugu. Duh kweli Mayalla umepata tender nini ya kuwatetea hao jamaa labda umehamia katika fani yako nyingine ya sheria.
 
kiongozi wao Jk alizisafisha na kusema pesa sio za serikali.Unataka zisafishwe mara ngapi?Hvyo,walikuwa na haki zote kupokea.Tuanze kwanza na kichwa then tutashuka chini taratibu.
Wewe wadanganye tu wenzako eti Jk alisema siyo za umma.

Jk siyo Magufuli.... Rugemalila na Sighseth wako Ukonga Sasa na wengine watafuata.
 
Back
Top Bottom