Walimu wote tafadhali someni hapa

Walimu wote tafadhali someni hapa

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Ni mwaka mpya ambao utaambatana na mambo mengi ukiwamo uchaguzi mkuu,uboreshaji wa daftari la kudumu na upigaji wa kura za maoni ya katiba mpya. Katika matukio yote hayo utakuta walimu hutumiwa na kulipwa pesa kidogo.

Najiuliza maswali kama walimu wana umuhimu kiasi hicho hv serikali inashindwaje kuwalipa madai yao? Mfano nauli za likizo,mapunjo ya mishahara, kupandishwa madaraja kwa wakati?

Walimu tuungane pamoja na kuimbia wazi tumechoka na hatutaipigia kura CCM kwani wanatuona sisi matoi, tumechoka kuonewa,kama kuna wakati wa kutangaza mgogoro ndiyo huu.

Rai wa cwt tafadhalini tangazeni mgogoro na kama hawaelewi walimu tupige kampeni serikali ya ccm iache hadaa tusikubali kuendelea kudharauliwa na kama hawajui umuhimu wapuze madai yetu wajue watalia 2015!
 
Hilo halipo kwa Walimu wa Tanzania hii ninaowafahamu.
 
Kwa walimu wa hapa nchi ya kusadikika haiwezekani kugoma wala kususia labda watu jamii ya daktari Ulimboka wabadili fani na kuwa walimu.
 
Acha uzushi safari hii ni wanajeshi ndo watatumika na wanatumika tayar kwenye vitambulisho vya utaifa
 
Kwa walimu wa hapa nchi ya kusadikika haiwezekani kugoma wala kususia labda watu jamii ya daktari Ulimboka wabadili fani na kuwa walimu.

Skype siku nyingi sikuoni. umerundi nisha-develop kwa sasa najua kuandika kiswahili fasaha kama bakita.
 
Last edited by a moderator:
Huu ni mwaka wao nao kula posho mana wengine posho ni uchaguzi hadi uchaguzi.
 
Nisingekua mwalimu kama sijitambui maana nisingekua na uwezo wa kujieleza mbele ya wanafunzi kama wewe unajitambua jaribu kusimama mbele ya watoto kumi fundisha halafu uone maana yako ya kujitambua, hujielewi umeandija nini hapo
 
Nisingekua mwalimu kama sijitambui maana nisingekua na uwezo wa kujieleza mbele ya wanafunzi kama wewe unajitambua jaribu kusimama mbele ya watoto kumi fundisha halafu uone maana yako ya kujitambua, hujielewi umeandija nini hapo

Mwl hawezi kuanzisha thread kama hii ya uchonganishi nina wasiwasi na wewe pia aliesema hujitambui hakukosea.
 
Wa Kutanganza Mgogoro na CCM si waalimu wa Tanganyika hii. Wanadanganywa na CCM eti uwaliamu ni wito hiyo hicho kidogo hata hawapaswi kukipat. Lakini hata hivyo waalimu wa Bongo wanapigika vilivyo;

Pamoja na Kupigika na maisha lakini walivyo mbumbumbu Hawako tayari kuiacha CCM; CCM kwao ni mamayao na babayao na wala hawaambiwi kitu. Lakini wakumbuke cha moto wanakipata.
 
walimu wenyewe ni four failures,hawajitambui

So mimi na wewe tumefundishwa na failures? sasa sijui uwezo huu wa kugundua kua wao failures tumeupata wapi ufike wakati teheshimu mchango wa mwalimu kumbuka ulienda shule haujui kitu ukafundishwa hadi kufuta kamasi leo unawageuka na kuwatusi sio sawa.
 
Mimi ninashauri kila wali katika wilaya zote tujikusanye kwenye ofisi za CWT wilaya tuanze kuwashushia kipondo makatibu wa CWT maana wanakalia kula 2% zetu na hawafanyi kazi yoyote kutuunganisha ili tutangaze mgogoro na serikali
 
Jaman punguzeni jazba mm ni mwalimu, nina mwaka mmoja kazini.

BAED UDSM 2010 - 2013 walimu niliowakuta hasa walioajiriwa kabla ya 2000's kiukweli ni waoga sana sijui walifanywa nini.ila kwa changamoto tunazowapa sisi walimu vijana watabadirika na kuwa sehemu ya ukombozi badala ya kuwa wakala na nguzo ya nyinyiemu.

Kuweni wapole vijana tupo kazini kwa wanafunzi na walimu waoga ila siyo failures ni uhakika wa ajira kutokana na hali ya familia zetu ndicho wengi wetu kimetuleta huku ila tulifaulu vizuri tu!
 
walimu wengi ni mbulula hawajitambui , wangejitambua ccm 2010 isingeshinda

Siipendi Ccm lakini sidhani kama walimu ndio walisababisha ushindi wao. Kwani pale kituoni hakuna mawakala wa vyama vyote? Kwa taarifa yako kura huwa zinachakachuliwa katika vituo vya kuunganishia matokeo na mwalimu huwa hayupo hapo.
 
Back
Top Bottom