Walimu waliotandikwa bakora wadai bil.3! weee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu waliotandikwa bakora wadai bil.3! weee

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mwalimu Jr., Jun 12, 2009.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Jun 12, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Aidha, Serikali inaandaa
  mradi mkubwa wa kujenga nyumba za walimu nchi nzima kwa
  kuanzia na maeneo ya pembezoni yenye mazingira magumu ili
  kuondoa kero za makazi ya walimu."


  Kuna uhusiano wa moja kwa moja na wale walimu wa Katerero kuchapwa viboko na DC baada ya kuchelewa kuripoti kazini kutokana na umbali uliopo kati ya walimu wanakoishi na shule ilipo. Bila shaka walimu wote sasa wataimba: "Kikwete wetu tu, mwingine hatuna haja naye hata mapadri waseme vipi!!! "
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wale walimu 15 wa Bukoba Vijijini waliotandikwa bakora viruri kabisa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Bw. Abert Mnali wameiburuta serikali ya JK kwa pilato wakitaka kulipwa fidia ya sh. bilioni tatu.

  Hayo yaliwekwa wazi na katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Kagera, Bw. Aron Masalu, ambapo alisema hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kujibu notisi ya siku 90 waliyotandikwa na CWT.

  "Tumefungua kesi tayari tukidai kulipwa shilingi bilioni tatu na kinachosubiriwa sasa ni kupangiwa Jaji wa kuisikiliza...tunataka kupata haki yetu," alisema Bw. Masalu.
  I
  Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba ambako tukio hilo lilitokea na kila mwalimu anadai fidia ya sh. milioni 200.

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa CWT,alinukuliwa akisema "Hawakutaka kujibu notisi wala kutuita kwa kufanya mazungumzo ya kuangalia namna gani wangeweza kuwalipa walimu hao fidia, uamuzi tuliochukua ni wa kwenda mahakamani," alisema.

  Alifafanua kuwa walimu hao wanastahili kulipwa fidia hiyo kutokana na udhalilishwaji uliofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Mnali ambaye alishirikiana na Koplo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) kuwacharaza viboko walimu.

  Hivi karibu walimu 15 wa shule za msingi wa Bukoba vijijini walicharazwa viboko na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba kwa madai ya kusababisha wilaya hiyo kufanya vibaya katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka jana.

  Hatua hiyo iliikwaza Serikali na Rais Jakaya Kikwete alimtimua kazi mara moja, Bw. Mnali baada ya tukio hilo.

  Walimu waliotandikwa bakora wadai bil.3! weee
   
 3. A

  August_Shao Senior Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 23, 2007
  Messages: 158
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  wameula wa chuya hawa jamaa.......serikali hihi iwape hivi hivi 3.o bil? mbona hata mimi nitafungua kesi....
   
Loading...