Walimu waandamana Lushoto

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,738
92,160
Walimu wa shule za Msingi Wilayani Lushoto wameandamana mchana huu wakidai kuwa Posho ya Uhamisho waliyopewa ni ndogo sana, wamepewa laki moja (100,000).

Ikumbukwe kwamba Walimu Wilayani Lushoto walihamishwa bila hata mpangilio kupelekwa maeneo mbali mbali hadi Mkurugenzi akaingia kwenye mgogoro na Mbunge, bahati nzuri wote ni Makada wa CCM.

Tunavyoongea baadhi ya Walimu wameswekwa ndani kwa kudai haki zao. Only in Tanzania
 
Mtoa mada naona umetoa mada kwa uchochezi. Mm kwa mtazamo wangu, hayo maneno uliyomalizia wala sijabarikiwa nayo
 
Mtoa mada naona umetoa mada kwa uchochezi. Mm kwa mtazamo wangu, hayo maneno uliyomalizia wala sijabarikiwa nayo

Mkuu Dundo_Boy pole, Sidhani Kama mleta Mada alitaka kumbariki mtu kwa post hii. Tafsiri ya "uchochezi" imekuwa Pana siku hizi, kutokana na namna tunavyopokea habari, ikikufurahisha inshaalah, usipoipenda, uchochezi!


Walimu wa lushoto wamedhulumiwa mkuu!
 
Kwetu huko

Hebu wawalipe mapema walimu wetu kabla hatuja rudi huko maana tusije itwa wachochezi. Hatuwezi kunyamaza kama wanawaweka ndani watu wanaodai haki zao.
Unamuhamisha mtu halafu unamlipa laki moja na sheria haisemi hivyo?
 
Back
Top Bottom