Walimu tunanyanyaswa sana

Nimepata shida saba kusoma uzi wako, kwasababu ninahisi mwalimu wako alikufundisha kuandika bila kituo . Ila usijali, lengo lako ni kutuambia tujue fani yako na chuo unachosoma. Nastaajabu pia kuona wewe sio mwanafunzi makini, yaani hutaki kufuata unayofundishwa. Ukiwa unafundishwa mbinu za ufundishaji kuna sehemu umeambiwa mwanafunzi akikosea basi mshushie MAKONDE ya namna ile?. Hakuna mbinu nyingine za kumfundisha mwanafunzi pale anapokosea?. Na ukimpiga vile unahisi ukirudi darasani tena kumfundisha atakuelewa?. Au chuoni kwenu hamfundishwi elimu ya saikolojia?.
 
Walimu hao hao wanakesha kwenye mwege, hao hao wanaisho nyumba moja wanne duh
 
Mwalimu anachukuliwa kama kitu gani sijui, kila baya anatupiwa yeye.
 
Samahan lakin umeshajaaliwa kupata MTT????
 
Hoja inatetea upande wako kama mwalimu lkn jua skopioni ni yeye na hajafanya katika sekta but huyo mwalimu ni kafanya ujinga katika wizara kubwa tz nakipndi kibaya. Wacha muwajibishwa et skopioni wee
waliowachapa makofi walimu wameshawajibishwa
 
Ikiwa kama ya kideo hakuna haja kabisa ya kupewa nafasi ya kujitetea.

Nanyi mrekodi mkiwa mnaonewa iwasaidie hata kwa audio.
kesi ya gwajima inayoendelea mpaka sasa, upande wa jamuhuri walitaka kupeleka audio ya gwajima akizungumza maneneo yaliyopelekea kupata kesi hio; ila mahakama ilikataa. sasa hio video inatumikaje kutoa hukumu ya moja kwa moja bila mhusika kupewa nafasi. binafsi mm sitamfuatilia mtoto wa mtu, kila mtu atafanya yake. dogo akizingua tu, fasta haingii kwenye kipindi changu na atafundishwa na mkuu wa mkoa au baba yake au mwingulu au ndalichako. sina muda wa kujadili mambo ya mtoto asiyekua na faida kwangu sana kuhatarisha kibarua changu, muda wangu ni kuwaza kutafuta hela ili kuziba pengo la mshahara mdogo ninaopokea
 
Kosa la Scorpion halihalalishi makosa ya walimu

Scorpion uhalifu wake ni kwa watu wazima
sio kwa watoto wadogo

walimu ni wazazi pia......hasira zenu msipeleke kwa wanafunzi
sasa mwalimu ambaye ni mzazi kamuadhibu mwanaye mkaidi anayekunja ngumi kupambana na mzazi wake. sijui ww mzazi utafanyaje mara utapotaka kumuadhibu mwanao naye akakukunjia ngumi? kuna uwezekano mwingulu na ndalichako wakaanza kwenda kuwafundisha watoto wakaidi shuleni. mimi mtoto mkaidi sitataka mazungumzo eti twende kwa mkuu, atatoka darasani niendelee na wengine. nikifanya mazungumzo sana napoteza muda wa kufikiria pesa. mshahara wenyewe huu!!!
 
wale wanaopigwa na kutoka damu na polisi wenu, wao wanakua wanapewa keki!!!
 
Tsh565,000 ndio wanabaki nayo,sasa kwani hujui kuwa walimu wa sekondari wana degree.
Na wa msingi ni Tsh419,000 hivyo bado umepotosha hapa.
Pia msingi kuna walimu wengi wana degree.
chukua hio 565000 toa laki na kidogo ya bodi ya mikopo, kwani bodi ya mikopo wameanza kukata 15% badala ya 8%. itabaki laki nne na kidogo. hicho kiasi atachokipokea mwalimu mwenye degree kama takehome, ni sawa na posho ya polisi aliyeishia form4 kwa mwezi
 
Haimtoshi ambaye yupo busy na watoto wa wenzake.
Sifundishi kwa sasa ila nakumbuka nilikuwa natumia muda wa kazini kuwa kwenye biashara zangu.

Nashauri Walimu wajitambue waachane na kuhangaika na wanafunzi.
 

Mmmmmmmmh!!!!!!

Kontakti mnazo saini huwa zinawaambiaje?
 
Haimtoshi ambaye yupo busy na watoto wa wenzake.
Sifundishi kwa sasa ila nakumbuka nilikuwa natumia muda wa kazini kuwa kwenye biashara zangu.

Nashauri Walimu wajitambue waachane na kuhangaika na wanafunzi.
kweli huu ni muda wa kila mtu kufanya yake. mwalimu atakua mpuuzi akiendelea kupewa adhabu na mwningulu na ndalichako kwa kumfuatilia mtoto mwenye wazazi wake.
 
mwisho wa haya ni kuwa mwanasiasa kama Sizonje, hata mi nna mpango huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…