Walimu shule ya msingi Goba Mpakani hamtendi haki

Leo 14/07/2025 wanafunzi wa darasa la tatu wanaosoma shule ya msingi Goba Mpakani iliyoko Dar es Salaam ambao jumamosi ya 12/07/2025 hawakwenda tuisheni wamechapwa fimbo na walimu wao.Mwalimu mkuu wa S/msingi Goba Mpakani tunaomba uliangalie swala hili kwa umakini.

kwa nini wanafunzi wanawaambia watoto wa darasa la tatu kwamba wasipoenda jumamosi na shilingi 500 kwa ajili ya kusoma tuisheni watachapwa?

Suala la mwanafunzi wa darasa la tatu kwenda tuisheni j,mosi liwe ni hiari na sio lazima.Mwalimu mkuu na walimu wenzako mjiulize.

1)Vipi kwa mzazi ambaye hana uwezo wa kumpa hiyo sh 500 mtoto wake kwa ajili ya tuisheni?

2)Kwa nini mwanafunzi tena malaika wa darasa la tatu achapwe fimbo kisa tu ameshindwa kwenda tuisheni j,mosi na sh 500?

3)Wanafunzi watapata muda wa kupumzika saa ngapi(siku ipi?)ili hali kuanzia jumatatu hadi ijumaa wanaondoka asubuhi sana na kurudi jioni kabisa wakiwa hoi(ba siku hizi za masomo wanakuwa wameunganisha na tuisheni j,tatu -ijumaa).

N:B Muelewa wazazi hatupingi swala la tuisheni kwa wanafunzi tatizo linakuja suala hili linapokuwa ni LAZIMA na mtoto asipokuja anachapwa hasa ikizungatiwa ni siku ya ,jmosi ya watoto wadogo hawa kupata muda wa kupumzika.
Vikao vyenu vya wazazi huwa mnajadiliana nini? Hakuna michango inayotolewa shuleni bila kupitishwa na wazazi.
 
Shule za dsm hawa walimu wana njaa, siyo shule tu. Ni shule karibu zote za msingi na secondary. Darasa la tatuz la nne na la sita ni majanga. Form one, form two na form four ni majanga mengine. Juzi nimekaa nikawazaa nikapata jibu kwamba... Hamna mtu mwema akiwa na ajira ya serikale. Lazima kuna namna ya dhuruma itatengenezwa alafu ilazimishwe kuhalalishwa... Watajinunisha na hoja zao za kipumbavu povu juu kama wamegongwa na kobra.

Usiombe uwe maskini au unajitambua na kusimamia msimamo dhahiri hapo ndo utajua kuwa ile misemo kuwa elimu ni ukombozi au ufunguo wa maisha ni Upumbavu mtupi.

Mungu tuzindue sisi, wazindue na hawa wote na wakumbushe hii ni dunia tu na sisi binadamu tunapita hivyo hamna kitu bora kabisa kama kutenda wema na haki.
Ili jambo la shule na michango lianzishiwe uzi maalum. Tutaje tu hayo majina ya shule na walimu wao Ubaya ubaya tu
 
Vikao vyenu vya wazazi huwa mnajadiliana nini? Hakuna michango inayotolewa shuleni bila kupitishwa na wazazi.
JINSI​
A​
B​
C​
D​
E​
​
WASICHANA​
0​
34​
29​
3​
0​
​
WAVULANA​
1​
28​
27​
5​
0​
​
JUMLA​
1​
62​
56​
8​
0​

Matokeo yao mwaka jana yalikua mabaya inawezekana ndio maana walifikia maamuzi hayo
 
Hayo ndio matokeo ya shule nyingi za serikali tho! Tena bora wao wana B nyingi, wengi hudondokea C.
 
Mwezi wa sita siku ya kufunga shule kikao na wazazi kilikuwepo na mambo mengi ya msingi yalizungumzwa....nielewe tatizo sio michango ya tuisheni au yoyote ile.... maana michango mingi tu wazazi waliridhia pamoja na tuisheni.j,tatu mpaka ijumaa shida inakuja mtoto kuchapwa asipoenda tuisheni siku ya mapumziko jumamosi ..hii haiko sawa
Vikao vyenu vya wazazi huwa mnajadiliana nini? Hakuna michango inayotolewa shuleni bila kupitishwa na wazazi.
 
Mwezi wa sita siku ya kufunga shule kikao na wazazi kilikuwepo na mambo mengi ya msingi yalizungumzwa....nielewe tatizo sio michango ya tuisheni au yoyote ile.... maana michango mingi tu wazazi waliridhia pamoja na tuisheni.j,tatu mpaka ijumaa shida inakuja mtoto kuchapwa asipoenda tuisheni siku ya mapumziko jumamosi ..hii haiko sawa
Ndio mzungumze kwenye vikao vyenu.
 
Basi acha ufitini na umbea , mind your business
Wewe hata maana ya neno umbeya na fitina ukiulizwa nina uhakika utapata sifuri(0)...hujui maana ya umbeya wala fitina.huzuni....
Pia hii assignment ya kuongelea wengine ni mojawapo ya business zangu humu duniani
 
Leo 14/07/2025 wanafunzi wa darasa la tatu wanaosoma shule ya msingi Goba Mpakani iliyoko Dar es Salaam ambao jumamosi ya 12/07/2025 hawakwenda tuisheni wamechapwa fimbo na walimu wao.Mwalimu mkuu wa S/msingi Goba Mpakani tunaomba uliangalie swala hili kwa umakini.

kwa nini wanafunzi wanawaambia watoto wa darasa la tatu kwamba wasipoenda jumamosi na shilingi 500 kwa ajili ya kusoma tuisheni watachapwa?

Suala la mwanafunzi wa darasa la tatu kwenda tuisheni j,mosi liwe ni hiari na sio lazima.Mwalimu mkuu na walimu wenzako mjiulize.

1)Vipi kwa mzazi ambaye hana uwezo wa kumpa hiyo sh 500 mtoto wake kwa ajili ya tuisheni?

2)Kwa nini mwanafunzi tena malaika wa darasa la tatu achapwe fimbo kisa tu ameshindwa kwenda tuisheni j,mosi na sh 500?

3)Wanafunzi watapata muda wa kupumzika saa ngapi(siku ipi?)ili hali kuanzia jumatatu hadi ijumaa wanaondoka asubuhi sana na kurudi jioni kabisa wakiwa hoi(ba siku hizi za masomo wanakuwa wameunganisha na tuisheni j,tatu -ijumaa).

N:B Muelewa wazazi hatupingi swala la tuisheni kwa wanafunzi tatizo linakuja suala hili linapokuwa ni LAZIMA na mtoto asipokuja anachapwa hasa ikizungatiwa ni siku ya ,jmosi ya watoto wadogo hawa kupata muda wa kupumzika.
Unataka wakale wapi? Jero tu mzazi unalia kama umeambiwa uchangie Figo au jicho
 
Mchawi sio 500 hata...mchawi hapa ni kwa nini mwanafunzi alazimishe na kuchapwa asipoenda tuisheni tena siku ya j,mosi
Asipoenda wako na wa yule hauoni makusanyo yatapungua . Tutampa kibano mtoto wako mpaka cheche zimtoke asipokuja jmosi hii. Subiria uone
 
Halafu unasema walimu hawana akili🙆‍♂️🙆‍♂️
Walimu awana akili kabisa 0 .....kama amjui umuhimu wa kupumzika kisaikolojia....mnatumia nguvu nyingi na kuvuna kidogo tatizo akili zenu finyu ....jumamosi na jumapili ni mapumziko muhimu kwa mtoto ...kwani hao wasomi mnaowazalisha kwa kusoma bila ya mapumziko wamefanya kitu gani cha maana Tanzania au duniani kuzidi wengine?
 
Mchawi sio 500 hata...mchawi hapa ni kwa nini mwanafunzi alazimishe na kuchapwa asipoenda tuisheni tena siku ya j,mosi
mfano wangu wa 100/= ya uji umeusoma? -- lazima waende kwa lazima ndo uwajibikaji huo
 
Vikao vyenu vya wazazi huwa mnajadiliana nini? Hakuna michango inayotolewa shuleni bila kupitishwa na wazazi.
Hii kauli ya kwamba wazazi ndio wanapitisha michango ya kipumbavu ndio inayotugharimu,nimeshahudhuria vikao vingi sana vya wazazi shuleni huwezi amini kuna wazazi feki huwa wanapangwa na shule ili wakomalie ajenda hiyo ipite na huwa wana mgao wao na jinsi wazazi wengi wasivyokuwa na uwezo wa kuongea basi unakuta ajenda zinapita kwa lazima hata kama walioafiki ni wazazi wawili kati ya wazazi 200,na mara nyingi vikao vya shuleni huwa hivyo.UKIONA SHULE INA MICHANGO MICHANGO MINGI YA KIPUMBAVU BASI JUA HIZO NI BIASHARA ZA WALIMU KATIKA NAMNA NYINGINE

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom