Walimu shule ya msingi Goba Mpakani hamtendi haki

Walimu shule ya msingi Goba Mpakani hamtendi haki

Mama Nehemiah

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
275
Reaction score
475
Leo 14/07/2025 wanafunzi wa darasa la tatu wanaosoma shule ya msingi Goba Mpakani iliyoko Dar es Salaam ambao jumamosi ya 12/07/2025 hawakwenda tuisheni wamechapwa fimbo na walimu wao. Mwalimu mkuu wa S/msingi Goba Mpakani tunaomba uliangalie suala hili kwa umakini.

Kwanini wanafunzi wanawaambia watoto wa darasa la tatu kwamba wasipoenda Jumamosi na shilingi 500 kwa ajili ya kusoma tuisheni watachapwa?

Suala la mwanafunzi wa darasa la tatu kwenda tuisheni Jumamosi liwe ni hiari na sio lazima. Mwalimu mkuu na walimu wenzako mjiulize.

1) Vipi kwa mzazi ambaye hana uwezo wa kumpa hiyo sh 500 mtoto wake kwa ajili ya tuisheni?

2) Kwanini mwanafunzi tena malaika wa darasa la tatu achapwe fimbo kisa tu ameshindwa kwenda tuisheni J,mosi na sh 500?

3) Wanafunzi watapata muda wa kupumzika saa ngapi(siku ipi?)ili hali kuanzia jumatatu hadi ijumaa wanaondoka asubuhi sana na kurudi jioni kabisa wakiwa hoi(ba siku hizi za masomo wanakuwa wameunganisha na tuisheni j,tatu -ijumaa).

N:B Muelewa wazazi hatupingi swala la tuisheni kwa wanafunzi tatizo linakuja suala hili linapokuwa ni LAZIMA na mtoto asipokuja anachapwa hasa ikizingatiwa ni siku ya jumamosi ya watoto wadogo hawa kupata muda wa kupumzika.
 
Leo 14/07/2025 wanafunzi wa darasa la tatu wanaosoma shule ya msingi Goba Mpakani iliyoko Dar es Salaam ambao jumamosi ya 12/07/2025 hawakwenda tuisheni wamechapwa fimbo na walimu wao.Mwalimu mkuu wa S/msingi Goba Mpakani tunaomba uliangalie swala hili kwa umakini.kwa nini wanafunzi wanawaambia watoto wa darasa la tatu kwamba wasipoenda jumamosi na shilingi 500 kwa ajili ya kusoma tuisheni watachapwa?
Suala la mwanafunzi wa darasa la tatu kwenda tuisheni j,mosi liwe ni hiari na sio lazima.Mwalimu mkuu na walimu wenzako mjiulize.
1) Vipi kwa mzazi ambaye hana uwezo wa kumpa hiyo sh 500 mtoto wake kwa ajili ya tuisheni?
2) Kwa nini mwanafunzi tena malaika wa darasa la tatu achapwe fimbo kisa tu ameshindwa kwenda tuisheni j,mosi na sh 500?
3) Wanafunzi watapata muda wa kupumzika saa ngapi(siku ipi?)ili hali kuanzia jumatatu hadi ijumaa wanaondoka asubuhi sana na kurudi jioni kabisa wakiwa hoi(ba siku hizi za masomo wanakuwa wameunganisha na tuisheni j,tatu -ijumaa).
N:B Muelewa wazazi hatupingi swala la tuisheni kwa wanafunzi tatizo linakuja suala hili linapokuwa ni LAZIMA na mtoto asipokuja anachapwa hasa ikizungatiwa ni siku ya ,jmosi ya watoto wadogo hawa kupata muda wa kupumzika.
Nilisema hapa kuwaachia walimu maamuzi yote ni upumbavu. Walimu hawana akili. Nilisema kuwe na kanuni kuu za nchi kuhusu muda wa masomo... Siku za Jumamosi na Jumapili ziwe ni mapumziko kamili; kusiwe na hata home week yoyote. Tatizo, wapumbavu wa Sisiemu hawanielewi. Pia, muda wa wanafunzi kufika shule uongezwe kwa nusu saa zaidi ili wanafunzi waweze kwenda shule wakiwa wamekunywa chai na kujisafisha vizuri. Unakuta mtoto anakosa hata muda wa kupiga mswaki vizuri kisa kuwai shule.
 
Wapeni izo 500 kuepusha kelele kelele zote umeombwa 500 tupige kelele za reform bado tupige kelele za wewe kuombwa 500 ya tuition
 
Leo 14/07/2025 wanafunzi wa darasa la tatu wanaosoma shule ya msingi Goba Mpakani iliyoko Dar es Salaam ambao jumamosi ya 12/07/2025 hawakwenda tuisheni wamechapwa fimbo na walimu wao.Mwalimu mkuu wa S/msingi Goba Mpakani tunaomba uliangalie swala hili kwa umakini.

kwa nini wanafunzi wanawaambia watoto wa darasa la tatu kwamba wasipoenda jumamosi na shilingi 500 kwa ajili ya kusoma tuisheni watachapwa?

Suala la mwanafunzi wa darasa la tatu kwenda tuisheni j,mosi liwe ni hiari na sio lazima.Mwalimu mkuu na walimu wenzako mjiulize.

1)Vipi kwa mzazi ambaye hana uwezo wa kumpa hiyo sh 500 mtoto wake kwa ajili ya tuisheni?

2)Kwa nini mwanafunzi tena malaika wa darasa la tatu achapwe fimbo kisa tu ameshindwa kwenda tuisheni j,mosi na sh 500?

3)Wanafunzi watapata muda wa kupumzika saa ngapi(siku ipi?)ili hali kuanzia jumatatu hadi ijumaa wanaondoka asubuhi sana na kurudi jioni kabisa wakiwa hoi(ba siku hizi za masomo wanakuwa wameunganisha na tuisheni j,tatu -ijumaa).

N:B Muelewa wazazi hatupingi swala la tuisheni kwa wanafunzi tatizo linakuja suala hili linapokuwa ni LAZIMA na mtoto asipokuja anachapwa hasa ikizungatiwa ni siku ya ,jmosi ya watoto wadogo hawa kupata muda wa kupumzika.
hapa mchawi ni hiyo 500/=, shule ya jirani hapa kuna kipindi wazazi walitaka kuzua balaa kisa 100/= ya kikombe cha uji.


walimu waendelee kukabia juu tu
 
Hapa ni mzazi kumfata mwalimu wa mwanao na kumwambia mtoto hawezi kwenda jumamosi umemaliza....
 
Wapeni izo 500 kuepusha kelele kelele zote umeombwa 500 tupige kelele za reform bado tupige kelele za wewe kuombwa 500 ya tuition
Soma post kwa umakini na utulivu uelewe hoja vizuri sio kurukia rukia...

Sijaona tatizo wanafunzi kwenda tuisheni... sababu kuanzia J. tatu mpaka ijumaa wanaingia tuisheni na wazazi hawana shida wameridhia hili... Tatizo linakuja kwa nini malaika wa darasa la tatu achapwe bakora tatu kwa kutoenda siku ya mapumziko- Jumamosi tuition?
 
Mchawi sio 500 hata...mchawi hapa ni kwa nini mwanafunzi alazimishe na kuchapwa asipoenda tuisheni tena siku ya j,mosi
 
Shule za dsm hawa walimu wana njaa, siyo shule tu. Ni shule karibu zote za msingi na secondary. Darasa la tatuz la nne na la sita ni majanga. Form one, form two na form four ni majanga mengine. Juzi nimekaa nikawazaa nikapata jibu kwamba... Hamna mtu mwema akiwa na ajira ya serikale. Lazima kuna namna ya dhuruma itatengenezwa alafu ilazimishwe kuhalalishwa... Watajinunisha na hoja zao za kipumbavu povu juu kama wamegongwa na kobra.

Usiombe uwe maskini au unajitambua na kusimamia msimamo dhahiri hapo ndo utajua kuwa ile misemo kuwa elimu ni ukombozi au ufunguo wa maisha ni Upumbavu mtupi.

Mungu tuzindue sisi, wazindue na hawa wote na wakumbushe hii ni dunia tu na sisi binadamu tunapita hivyo hamna kitu bora kabisa kama kutenda wema na haki.
 
Back
Top Bottom