Walimu Sekondari ya Aga Khan wagoma kisa Ubaguzi wa Rangi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
ZAIDI ya walimu 50 wenye asili ya Kiafrika kwenye shule ya Sekondari ya The Agha Khan Mzizima wamegoma kuingia darasani kufundisha wanafunzi kwa kile walichodai kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa ukiwanyanyasa na kuwabagua kwa rangi.

MwanaHALISI kupitia chanzo cha kuaminika kilipata taarifa hizo na kufika shule hapo kushuhudia mgomo huo ulianza leo tarehe 24 Mei 2022 asubuhi.

Mwandishi wetu alipofika shule hapo aliwakuta wanafunzi wakirandaranda nje ya madarasa huku walimu wenye asili ya kitanzania wakiwa hawaonekani eneo hilo.

Mwandishi alifika mapokezi kwa ajili ya taratibu za kupata taarifa hizo na chanzo cha mgomo huo alimsikia mwanafunzi mmoja akimuomba mwalimu wa kike ruhusa “madam kama hatusomi mturuhusu turejee nyumbani mapema”

Hata hivyo uongozi wa shule hiyo haukuwa tayari kuzungumzia suala hilo lakini Mwana HALISI ilipata nafasi ya kuzungumza na walimu wa shule ambao walikuwa wamejikusanya pamoja kwenye jengo la nyuma wakisisitiza kuwa wamegoma kwa kile walichokidai kukithiri kwa ubaguzi na unyanyasaji.

Mwalimu Mohammed Haji mwalimu anayefundisha somo la Baiyolojia kwenye shule hiyo amesema kuwa shule hiyo ina waalimu wa kiafrika na walimu wanaotoka bara la Asia ambao wengi ni wahindi.

‘’Likifika suala la uamuzi, rangi inakuwa kigezo na wahanga wakubwa ni sisi watanzania, mpaka inafika kipindi tunakuwa hatuna imani na kesho yetu kwa sababu hapa unaweza kuzushiwa chochote kuchafuria CV zako mfano wale wenzentu waliosingiziwa kuvujisha mitihani.

“Mwaka jana kulitokea suala la kuvuja mitihani ambapo sisi tuna mashaka na kuvuja kwa mitihani hiyo lakini bila sababu yoyote walimu wa Kitanzania watatu waliangushiwa jumba bovu na kufukuzwa kazi, sisi ni watu wazima mambo yote yanayotokea hapa tunayaona,”amesema Haji.

Haji amesema kuwa ubaguzi huo umekwenda mbali mpaka kwenye masuala ya malipo kwa kuwa walimu wa kigeni wanalipwa kiwango cha juu mara nne zaidi ya kiasi cha Mtanzania ikiwa kiwango cha utendaji kazi ni sawa, “Tena walimu wa kitanzania wanafanya kazi zaidi”.

Anasema kuwa walimu wa Kitanzania hawaheshimiki, “ sisi walimu wa Kiafrika unaweza ukakemewa mbele ya wanafunzi na ukienda kulalamika unapewa onyo kali lakini hata kwenye ajira akiondolewa Mtanzania ataletwa raia wa kigeni na atapewa kiwango kikubwa cha mshahara.

“Tunanyanyaswa mpaka na walimu wenzetu wale wahindi wanatuona kama watu wa Second Class kwenye taasisi hii”

Issa Sumbi Mwalimu wa shule hiyo amesema kuwa ubaguzi huo unawaathiri na kwamba hivi karibu wameondolewa kazini walimu takribani watano bila kuwepo kwa sababu yoyote na waliojaza nafasi zao ni walimu wa kihindi.

Pamera Mboya Mwalimu wa TEHEMA katika shule hiyo amesema kuwa chanzo cha kuondolewa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ambaye alikuwa akisimama kutetea haki za walimu wa Kitanzania shuleni hapo kinaukakasi na kwamba wanahisi kuwa kuna shinikizo.

Samweli Kameme ni mmoja wa walimu wa The Agha Khan Mzizima amekiri kuwa uongozi wa shule huo unawabagua walimu hao wenye asili ya kiafrika.

“Unyanyasaji huu unafanyika kwa wazi kwetu sisi walimu kwa kubaguliwa na uongozi wa shule hususani Mkurugenzi wa shule anajua anachotenda hasa sisi walimu weusi , tunanyanyasika kwenye nchi yetu kwa kweli inauma”

“Mikataba inasitishwa bila sababu za msingi, wakiondolewa kazini walimu wa kiafrika wanaletwa walimu wenye asili ya kihindi tunaamini Rais Samia ataliona hili tunabaguliwa kwenye ardhi yetu,’ ameongeza.

John Kayoa Ofisa Rasilimali watu (HR) Msaidisi wa shule hiyo ambaye alimtaka mwandishi wa habari hizi aache maswali yake yote kwake ili siku inayofuata apate majibu.

Kayoa amesema kuwa kuhusu tuhuma za ubaguzi anaweza kuzisemea kidogo kuwa si za kweli.

“Unajua Mwandishi hapa kuna watu wanaotoka nchi tofauti tofauti na kila mtu anautamaduni wake hayo mambo hayana ukweli na kuhusu ajira kwa walimu wa kigeni sisi tunawaalimu zaidi ya 103 kwenye hao walimu raia wa kigeni ni walimu 13 tu,” amesema.

MWANAHALISI
 
Hili suala sio la kuvumilia kabisa.. Yaani ndani ya nchi yako bado unanyanyasika utoke uende kwenye nchi zao nako unyanyasike... hii si sawa.

Kama Serikali imeshindwa kusimama na kukemea wazi wazi vitendo hivi vya ubaguzi ifike hatua wananchi tuanze kuwanyoosha hawa ma gabachori.


#MaendeleoHayanaChama
 
Ukoloni ulishawafanya wahindi wawe second class citizens na waafrika third class citizens.

Hata utawala wa nchi unaona hivyo, ndio maana hizi kesi za ubaguzi zinapotezewa.

Hakuna muhindi anaempenda muafrika, iwe kwenye malipo, heshima na utu.
 
Waafrika ni watu pekee ambao wanalia kubaguliwa na kila mtu hata kwenye nchi yao, once again takwimu zinasema Wahindi Tanzania ni <200 000 au laki 2 lkn wanamiliki > 85% ya Uchumi wa Tanzania.

Kuna kitu hakipo sawa hapo, kwa hali ya kawaida Muhindi ndiye aliyepaswa kulalamika kubaguliwa Tanzania na siyo kinyume chake.

Kuna watu wanamtetea Rostam wanasema ni mwenzao lakini yeye Rostamu hawaoni hivyo!
 
Waafrika ni watu pekee ambao wanalia kubaguliwa na kila mtu hata kwenye nchi yao, once again takwimu zinasema Wahindi Tanzania ni <200 000 au laki 2 lkn wanamiliki > 85% ya Uchumi wa Tanzania.
Kuna kitu hakipo sawa hapo, kwa hali ya kawaida Muhindi ndiye aliyepaswa kulalamika kubaguliwa Tanzania na siyo kinyume chake.

Kuna watu wanamtetea Rostam wanasema ni mwenzao lkn yeye Rostamu hawaoni hivyo!
Hizo ni data za kuchemsha, takwimu haziko hivyo
 
Ukoloni ulishawafanya wahindi wawe second class citizens na waafika third class citizens.

Hata utawala wa nchi unaona hivyo, ndio maana hizi kesi za ubaguzi zinapotezewa.

Hakuna muhindi anaempenda muafrika, iwe kwenye malipo, heshima na utu.
Umenikumbusha yule Kanjibayi tajiri sana TZ anayewalipa wasomi wenye bachelor degrees mishahara ya 300, 000/= kwa kila mwezi
 
Nasikia huko Ulaya(UK) inatoa fursa za ajira kwa wahitimu wenye vipaji kutoka vyuo vya nje isipokuwa Afrika. Ila na sisi tuna matatizo yetu, hivi inawezekana tukafanya mambo yetu mapya bila kuiga kutoka sehemu nyingine??

Wanasayansi wetu tunaowategemea ndiyo kwanza wako kwenye siasa. Tunapanga bajeti kubwa hela hatuna, tunawekeza kwenye vitu badala kwenye Elimu.

Anyway, hao waalimu ni bora waje kwenye shule zetu, hatuna ubaguzi.
 
Yaani mpaka wamefikia Kugoma, basi tujue ukweli kwamba hali ni mbaya sana. Huyo HR Msaidizi ni Mtanzania na kwa kauli yake hiyo inaonyesha wazi anawatetea Wahindi.

Jiwe mwenyewe alishindwa kwa Mr. Aga Khan pamoja na kukutana Uso kwa Uso; kuhusu Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) kupokelewa katika Hospitali zake na wananchi waliliongelea sana hili suala mpaka aibu lakini mpaka kesho bado 'Ngoma Ngumu'.

Sembuse hili la Unyanyasaji wa Walimu Wazawa? Serikali ile ile tuitegemee tena!!?

Nawatakieni Kila la Kheri.
 
Back
Top Bottom