Sasa hata baada ya kuandika hayo lengo kuu ni lipi?
1.chuki kwa walimu
2.hasira za kukosa ajira
3.wivu kwa kuwa walimu wanapata ajira moja kwa moja na wewe upo mtaani huna kazi?
4.kuuambia umma kwamba walimu ni ma failures na wajinga kitaaluma?
5.dharau kwa kada zingine kwa vile wewe upo kada yenye heshima na mshahara mzuri zaid kuliko ualimu? Nk
Lakini haohao wenye marks hizo hizo na failure zao ndio walio kupa kiburi cha wewe ku type hapa na kuwadharau, hakuna msomi yeyote asiye pitia mikononi kwa mwalimu hivyo unacho kifanya wewe nikutukana wazazi wako baada ya kukuzaa na kukukuza, ni sawa na kukata daraja baada ya kuvuka mto ukidhan unaukomoa mto wakati wa kurudi uta hitaji daraja tena,, nadhan hata watoto wako hawata muhitaji mwalimu utawafundisha wewe na ukisha kuwa mfundishaji na wewe pia utakuwa umesha imgia kwenye kundi la walimu hasa tukitafsiri sahihi maana ya neno "MWALIMU"
Naweza sema mimi ni mwalimu na ni failure kama ulivyo sema lakini wanafunzi walio pita mikononi mwangu wengine ni engineer wengine ma Dr. Wengine walimu kama mimi na wengine wako kwenye fani zingine mbalimbali ,na wengine wanadharau kazi hii kama wewe ufanyavyo baada ya kuvuka
lakini wametoka kwenye mikono ya failure mimi kama sema yako.
Lakini pia unatakiwa kujua kuwa ualimu ni kazi inayo hitaji watendaji , na wala sio kazi ya class fulani, niseme ufinyu wako wa mawazo ndio ulio pelekea kufikiri hivyo na kuandika ulicho andika kwa vile ulitumia upande mmoja tu katika hoja yako hiyo
Neno mwalimu nineno lenye upana sana labda ulishindwa ku categorise huo ualimu unao usema ni upi maana hata wanao hubiri injili na kufundisha mafundisho ya mwenyezi mungu pia huitwa walimu
Lakini pia kwa kusema walimu wana uwezo mdogo ni katika lipi?
Maana kwa mfumo wetu wa elimu ulivyo bado haitosh kutambua uwezo katika uhalisia wake maana elimu hii hata mtu akiiiba mtihani au akapewa majibu ya mtihani hata kama hajui kusoma wala kuandika ingawa ana A kwa upande wako huyo ndio mwenye uwezo.ref darasa la saba anaye pata A masomo yote lakin hata kusoma kwa ufasaha kwake ni tatizo.lakini ana ufahuri mzuri kwenye cheti na hii sio huko tuu ipo hata shule za sekondari hadi vyuo.
Uwezo wa kitaaluma umegawanyika katika makundi mengi sana hivyo huwezi kutumia kigezo kimojaa kutoa majibu ya uwezo mdogo au mkubwa kama mtafiti ,maana kwa hoja yako hiyo umesha utia najisi huo utafiti wako
Na kwanini labda umeiona kada ya ualimu pekee ndio imekusanya failures na sio kada zingine? Maana kuna kada zingine hadi wenye ziro wako kazini na wanalipwa mshahara na serikali na ni watendaji wazuri mno kuliko hao wenye 1,2,3 nk. Lengo lako kuu lilikuwa ni lipi hadi ukapata wazo la kuwasakama walimu kwa hoja na kinadharia zaidi kuliko uhalisia?
Lakini hongera pia kwa utafiti wako wa kihisia kuliko uhalisia.