Walimu karibu wote uwezo mdogo

Walimu karibu wote uwezo mdogo

Mi ni mwalimu tangu form four napata one na chuo ni first class. Nina rafiki zangu zaid ya ishirini ni walimu na wamefaulu sana.
Siwezi bishana na huyu mbumbumbu wa PSPA ambae am sure GPA yake inatisha.
Huu uzi haupunguzi chochote kwa walimu ila tuu mleta uzi kama kweli we ni msomi sizani kama ni busara kutumia elimu yako kuwakashifu wengine aseee
 
Kweli walimu mna matatizo!!! mleta mada ameelezea vizuri sana juu ya hilo, kwamba kuna sababu kama tatu au nne za watu kusoma ualimu, lakini akasema majority ni ufaulu mdogo (walimu walio wengi, siyo wote). Sasa kama wewe hauko kwenye ufaulu mdogo maana yake uko katika sababu nyingine. Hili nalo wewe kama mwalimu unashindwa kulielewa tu?
Wewe na mleta mada nyote mnatakiwa kupimwa akili zenu
 
Nimeweka hapo awali ukifundishwa kupika haimainishi aliyekufundisha ataendelea kuwa zaidi yako, juhudi zako ndizo humfanya mtu ampite...mwalimu aliyenifundisha uwezo wake ndio uliishia pale ila kwa juhudi zangu nikampita...kwahiyo kama alimaliza form four akapiga four akapelekwa ualimu kisha akaja kufundisha shule ya msingi, mie mwanafunzi wake nikasonga mpaka chuo kikuu bado utasema mwalimu ni bright?! Asilimia kubwa ya waalimu uwezo upstairs ni mdogo
Na kingine mie sikusoma ualimu Bali nilisoma PSPA (Political Science and Public Administration)

Then unajiona umesoma kozi yenye maana sana kuliko hao waalimu,yaani ulivyoanza nikajua umepiga BAF,bcom,au engineering au ADA,labda una MAF au CPA au acca,cisa kumbe umehangaika sana na history,kiswahili etc then unadharau waalimu??hujielewi na unahitaji ukombozi wa kifra sana!Mungu akusamehe kwa kudharau Waalim ambao ndio wewe na mm walitufikisha apa hata unaweza kuandika huo utumbo wako,badilika ndugu yangu
 
Kama ulinifuatilia vyema nilitoa sababu kadhaa za wengi kukimbilia ualimu...halafu pili wengi wanaomaliza kidato cha nne na kufeli wengi wabovu kichwani, tukubaliane hakuna kufeli kwa bahati mbaya au kufaulu kwa kubahatisha...hivyo basi hao wakishafeli ndio linakuja swala la familia kama lina uwezo wa kusimamia show mpaka amalize chuo kama hawawezi vilaza hawa hukimbilia udhamini wa wizara ya elimu na kupangiwa vyuo na hatimaye vilaza hawa humaliza na kusubiri kupangiwa shule kama wanavyosubiria kupangiwa wa sasa....
Hebu nijuze swala moja hivi iwapo mpo wawili mnasoma HKL halafu matokeo kutoka umefaulu na kupiga one ya tano na mwenzako akapiga three suppose ni 14 unadhani wewe utaenda kusoma education chuo?? Kama ni ndio basi linakuja swala la familia kwamba ukitaka kusoma law hutapata mkopo hivyo itakulazimu kusoma ualimu ila yule wa three hana option kwakuwa amefeli...kwahiyo tukubaliane waalimu wengi wabovu upstairs
Mtoa mada nahisi unatoka kijijini kama mimi. Mi sisi tunaotoka vijijini tunajifanya hatujui matatizo, unasema hakuna kufeli kwa bahati mbaya hivi kama shule ina walimu 2 watoto wakifeli ni vilaza. Mtoto amesoma shule ina walimu 3 akapat three na yule aliosoma shule ina walimu 30 akapata Two. Tuacheni dharau mazingira ya kusoma hayafanani njooni vijijni muone. Tatizo lingine mtu kamaliza Ngudu akienda kusoma mlimani anakaa kwa mjomba ake anajifanya hajui maisha ya vijijini
 
Nimeweka hapo awali ukifundishwa kupika haimainishi aliyekufundisha ataendelea kuwa zaidi yako, juhudi zako ndizo humfanya mtu ampite...mwalimu aliyenifundisha uwezo wake ndio uliishia pale ila kwa juhudi zangu nikampita...kwahiyo kama alimaliza form four akapiga four akapelekwa ualimu kisha akaja kufundisha shule ya msingi, mie mwanafunzi wake nikasonga mpaka chuo kikuu bado utasema mwalimu ni bright?! Asilimia kubwa ya waalimu uwezo upstairs ni mdogo
Na kingine mie sikusoma ualimu Bali nilisoma PSPA (Political Science and Public Administration)
SIONI FAIDA ZA HUU MJADALA.NGOJA NIPITE!!
 
Kila aliesoma c muelewa na kipimo cha akili c makaratasi Bali ni uwezo wa kutetea makaratasi wako wengi hawajafaulu c Kwa kupenda ila mazingira na wapo waliofaulu kwa kuwa mazingira yaliruhusu hivyo mtizamo wako uko sawa ila utafiti wako haukuzingatia mambo muhim
 
UNAWEZA KUSEMA MAMA ZETU KARIBU WOTE NI WAGUMBA AU BABA ZETU NI HANITHI ?
 
Kwa mitazamo ya watu wengine humu wanavyokandia ualimu ni sawa na mtu anayeponda wazazi wake kwamba Mwenyezi Mungu hakuwaumba vizuri wazazi wake ila yeye ndo kaumbika vizuri kwa maana hiyo anajiona kama kajizaa vile.
 
Acha uongo uliokubuhu kuna watu wana division 2 na 3 walichukua education bachelor pale udsm na ninawajua..... Ila pole naona uzi umekukwaza
Sasa 2 and 3 ndio sio kilaza...??wenye 2 weng HKl hao
 
we jamaa hazikutoshi uwezo wa mtu haupimwi kwa kujaza makaratasi na kalamu hayo wanaopata division 1 mpaka sasa wanalipi jipya ktk maisha zaidi ya kuzunguka na vyeti kutafuta ajira na scolaship
 
Habari wanajamvi?

Ashakum sio matusi ila leo nimeamua kuleta mada hii baada ya kufanyia utafiti binafsi kwa muda hivi.Kwanza nilianza kuambiwa na rafiki yangu enzi hizo 2012 pale UDBS kwamba asilimia kubwa kama sio wote waalimu uwezo wao ni mdogo upstairs nikakataa akanitaka nifanye utafiti binafsi.

- Walimu wengi kama sio wote hawakupenda kuwa waalimu ila ufaulu wao ndio ulipelekea wakose option na kujikuta kwa shingo upande wanadumbukia kwenye fani ya ualimu bila kupenda.

-Asilimia kubwa ya walimu hawakupenda kwenda ualimu ila ukiachilia mbali ufaulu kuwa hafifu pia urahisi wa kuajiriwa, hii inatokana na ajira kuwa ngumu hivyo wengi kukimbilia ualimu ili kutatua matatizo yao ya ajira.

-Uchumi mbovu umepelekea wengi kuishia kuwa waalimu, hapa nina maana zile familia ambazo hazina uwezo wa kumlipia mwanafunzi kusoma kitu anachokipenda hivyo kujikuta akisoma ualimu ili apate ufadhili wa serikali.

Naomba nisieleweke vibaya ila jaribu kufuatilia kwa umakini uje unaimbie mwanafunzi aliyepata division one nzuri kabisa akawa mwalimu, asilimia kubwa ya waalimu ni waliosoma arts au biashara kwakuwa wengi matokeo yao hayakuridhisha hatimaye option pekee ikawa ualimu.

Waalimu wengi wa science walifeli hapa naomba uniletee mwalimu ambaye ama alisoma PCM, PCB, PGM n.k akapata divion one au two akaenda kusoma ualimu? Wanaokuwa waalimu wengi huangukia kwenye point ya ufaulu mbovu darasani na ni wachache sana huangukia kuwa waalimu sababu ya uchumi wa familia ila wengi saaana walifeli.

Hata kama walijiendeleza na kuwa na masters still ukirudi nyuma utakuwa wengi walifeli, ndio maana nikasema asilimia kubwa kama sio wote uwezo wao ni mdogo.
Fallacy!!! Utafiti fake umejikita katika Lusaka u maarufu. Kuna walimu kibao ufaulu wao unakutisha hata wewe,.Kuna sababu nyingi zinamfanya MTU akasome ualimu,1. Family background,hali mbaya ya umaskini na ambitions za kupata ajira mapema.
 
Mleta mada siyo anisi lakini huwezi mwita babako msengi wakati alimtia mamako mbegu ukazaliwa.Mdharau mwl. Mmamake
 
Mleta mada siyo anisi lakini huwezi mwita babako msengi wakati alimtia mamako mbegu ukazaliwa.Mdharau mwl. Mmamake
Tusimtukane mleta mada kwa maana yuko sahihi.
Wewe mwenyewe unajua asilimia 80 ya walimu wanafanya hyo kazi kwakuwa walikosa points zakuwapeleka kwenye kada nyingine!.
 
TEACOLTD Kwanza hongera kwa kuwa na ujasiri wa kuleta uzi huu maana sio viongozi wanaoongoza/simamia sekta ya elimu wala serikali kuu ilishawahi kukiri kuwa tuna tatizo la walimu wenye uweledi na kuwa na mkakati makhsusi wa kulitatua tatizo hilo.

Kimsingi yote uliosema ni kweli though naona Kuna simbilisi wanao comment kwa hoja zisizo na mashiko na nadhani ni kwasababu tu na wenyewe ama ndugu zao wamenufaika na huo mfumo ambao umetufikisha hapa kitaaluma.

Pili ualimu kama ilivyo kazi nyingine kama upolisi, jeshi hazichukuliwi serious na ndio imepelekea watu kuona hizi ni kazi za watu waliofeli, au kupata ufaulu duni hizi ndio kimbilio lao (kwa walimu wadau wameonyesha ufaulu na wako wanasoma wapi) Tatizo hili linaanzia primary huko ni zaidi ya time bomb watoto wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika but education system haijali, serikali ina focus kwenye enrolments, utawasikia tumevuka lengo la kuandikisha kwa 85% but does it make sense anyway! If at all these students finish std 7 and can't read and write! In 7yrs neither teachers themselves nor wasimamizi wa elimu has clue on what is going on! Halafu eti baada ya matokeo ya mitihani unakuja kutuambia watoto wameandika kat uni! !!!!!!

Hawa walimu wa shule za msingi hawawezi hata kufaulu ule mitihani wa darasa la saba kama ukiwapa wafanye sasa wanamfundisha nani? Hivyo Hivyo secondary wachukue walimu wa O-level wafanye mitihani wa kidato cha pili uone matokeo yake .

Elimu ni sekta ambayo inaelekea kuzimu TZ na si kwa bahati mbaya lakini ni matokeo ya makusudi ya serikali. Huwezi kuwa na serikali dhalimu iliyokosa hata haya , kama mtakumbuka awamu ya 4 pale watoto 60% walipofeli baada ya ku-acknowledge tatizo na kutafuta ufumbuzi serikali hatua iliyochukua ni ku-standardise matokeo ili tu kuwafool watanzania. Na IJULIKANE ni hao hao failures ndio waliobadilishiwa ufaulu na hatimae kuendelea na masoma na Leo/kesho ndio walimu so obvious mjinga atamfundisha mjinga mwenzake and we all know what will be the outcome!.

Leo mijadala mingi inajadili uwezo wa graduates wa Kitanzania(not only teachers) Kwamba hawana uwezo hata wa kujieleza wachilia mbali uwezo wa ku-deliver katika shughuli zao, the reasons ni kwamba Hawa si wengine ila ni matokeo ya huu huu uozo ambao for years umekua ukiendelea.

Ikumbukwe every child/person has the capacity to learn be it quicker or slow leaner it doesn't matter but it's upon the teacher to be able to;
1. Understand what he/she is supposed to teach (be conversant on the subject matter)
2. Be able to navigate that the class understand what he/she is teaching (teach-measure and evaluate)
3. Be warm, accessible enthusiastic and caring as it will open the desire for the students to ask where they don't understand
4. Set high expectations for all students
5. Inspire the students with his/her passion for education and for the course materials and constantly renews herself/himself as a professional on his/her quest in provide students with the highest quality education possible
6. Be able to "shift gear" -flexibility when a lesson isn't working. This kind of a teacher assesses his/her teaching throughout the lessons and finds new ways to present materials to make sure that every student understands the key concepts.

Mwisho serikali kupitia wizara husika andaeni walimu wenye sifa na sio utaratibu wa sasa wa mikakati zima moto. Let's be serious and select well qualified students for teaching career na sio failures ndo wanao kwenda ualimu na baadae kuja kufundisha watoto kwa level zote
Kweli mkuu waalimu kipekee Wa shule za serikali aka za kata ni vilaza kuliko hata baadhi ya wanafunzi wao. Kusoma kutamka maneno shida ni aibu! Kusema kweli wapo ambao ukiwapa mtihani wa form2 watafeli. Elimu bora ianze kukagua waalimu baadaye warudishwe chuo. Vinginevyo wanafunzi wataendelea kuwa vilaza.
 
Tanzania Ellimu ingikuwa inatusaia tungekuwa mbali sana, bahati mbaya tumebaki, hata asiekua na lolote kichwani atamkosoa hata mwenye PHD. Sababu tu yupo forums haonekani, Eti wali karibu wote wanauwezo mdogo, kufanyia kazi benki si kweli kuwa una Elimu kubwa kuliko mwalimu.
 
Mleta mada! Kwahiyo wewe mwenye uwezo mkubwa ilikuaje ukafundishwa na walimu wenye uwezo mdogo? Nadhani hao walimu waliokuvusha kutoka uko hadi sasa mie nadhani walikufundisha pumba ndo maana unakuja na argument km hizi...Next time utakuja na mada hivi baba na mama ako walikuzaaje? simple mind discuss pple
 
Inaonekana mleta post hukunyonya vizuri maziwa ya mama yako ulipokua mdogo.Hakuna mtu ninayemuheshimu kama mwalimu wangu hata iweje bila yeye hapa nisingefika.
 
Back
Top Bottom