Walevi wanajifariji sana

Kwenye maofisi nawaamini Sana wanatumia kinywaji. Hao wengine nawaona Kama wakuda ..

Huyo dogo mwache apige vyombo mradi haharibu kazi.

Tunywe pombe kistaarabu .
 
Huyo labda chuoni alikua msongo......wengine tulishafanya starehe zote chuoni tulivorudi kitaa tunaona hamna jipya
 
Magu hanywi, according to watu wake wa karibu
 
Ulevi si tu ule wa kukaa baa na kunywa maji maji yenye kileo ndani.

Hata kujiona upo perfect na mtindo wako wa maisha na kuwaona wengine ni mazwazwa ni ulevi wa akili pia. Kila kitu kwa kiasi.
 
Mzee Mkapa hakuheshimika na kukubalika? Maana alikua mtumia mzuri sana wa kilevi.
 
Kwa hiyo ambao hawanywi pombe ndio wake wao hawawezi kuliwa?
...akili zako zimekaa kushoto kweli!
Tena wewe utagongewa sana, tena wala siyo na wahuni bali hao hao unawaita walevi na hutakuwa na uwezo wa kuwafanya chochote!
Nikweli mwamba.
 
Bandiko hili laweza onekana kama ni ushauri nasaha, kumbe ni tilalila za kawaida sana tu zisizokuwa na maana yoyote.

Duniani hapa kila mtu huishi kwa vipaumbele vyake, ambavyo kwa wengine huonekana ni vituko ama ni ujinga, kumbe ndiyo maisha ya mtu!

Pasingekuwa na vipaumbele mbali mbali na mchanganyiko vichwani mwa watu, dunia isingekuwa na sura iliyonayo leo, maana tungefanya mambo yenye mfumo na mrengo mmoja kama enzi za mwenyekiti Mao.

Sazingine mtoa mada hautumii pombe kwa imani zisizotafitiwa lakini ukawa teja wa mambo yetu yalee, tena ukiyafanya kwa siri kubwa na kujibaraguza kwiiingi!

Ama waweza kuwa ni teja wa misosi mitamu tamu,unakula sana na kitambi unaning'iniza kwa sifa bila wasi wasi wowote bila kuelewa madhara ya kifo yanayokukabili kwa sababu unayoiona wewe kuwa siyo sababu!

Wapo watu wanaojitokeza leo na kukiri:...' siku niliyoacha bhangi'...'siku niliyoacha desh desh'...hao wameona madhara ama wamechoka tu.

Na binadamu mwenye uhuru na utashi ndivyo anatakiwa kuwa, afanye, atafiti na aamue mwenyewe bila ya kushikiwa akili na mtu.
 
Walevi mmetisha sana kwenye huu uzi.
Ila mkumbuke familia zenu basi maana tunawaona wenzenu wengine huku mitaani wametelekeza familia kisa gambe.

Na pia muwe mnafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa afya zenu kwani mtake msitake pombe ina madhara kiafya kwa kiwango chochote kile inachonywewa na hapa msilete ngonjera za "unywaji pombe kupita kiasi...".

Chengine mkumbuke starehe duniani sio pombe tu na sio kila anayekunywa pombe ni mjanja na mtu wa dili kama vile ambavyo wasiokunywa pombe sio wote ni washamba na wasiojua starehe.

Venginevyo endeleeni kula maji maisha ni kuchagua na kila mtu afurahie chaguo lake.

Mleta uzi wasindikize masela na wimbo wa "Dear gambe" kutoka kwa Young Killer Msodoki wasukutue koo kabla ya kushushia vyombozzz!.
 
Aache ujinga aseme ni kitu gani amefanya extra ordinary kwa kuwa hanywi pombe.. kwanza kwa thread yake tu anaonekana snitch wakati naye ni mwajiriwa!
Bora umeliona kama mimi, watu kama hawa kazini upenda kujipendekeza na kuwachongea wengine.
Wana tabia za kishamba.
 
Yan heading inasema walevi wanajifariji sana, halafu humo ndani mambo mengine kabisa.......we jamaa bwana.
 
Kwani hizo soda hazina madhara kiafya?
 
We endelea kutokunywa pombe ili uzidi Kuaminika na kupandishwa Vyeo kwenye ofisi za Umma, Sisi walevi acha tue tuendelee kukutana bar tu discuss Dili za maana na mwisho wa siku tuendelee kushikilia investment zetu, Ile hali wewe ukilamba miguu ya ma boss zako na kusubiri promotion Kazini kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ