mkuu mbiza,
nataka tu nikueleze jambo moja kuwa michezo hii ni real nimeishuhudia live south africa mwaka jana julai.
What does" real" stand for, kwakuwa umeuona live?
Kweli binadamu tunauelewa tofauti, sitaki kuamini kama kwa akili zako timamu unaweza kuamini yote yanayojiri ni real
Ukweli ni kwamba ili mchezo huu unoge ni lazima wawepo watu kama wewe watakao amani kwamba ni kweli na hakuna kuigiza
Labda nikupe hints, unapoona labda cena na edge wanapigana basi jua walifanya mazoezi yote unayoyaona ulingoni, kuumia kunakuja pale panapokua na miss taiming
Eti Daniel kavunjwa shingo next week ulingoni na kila week anapanda mara kibao
Angalia wanaume wa boxing au kickboxer sheria unaweza kupigana mara tatu kwa mwaka
Hivi ujiulizi majitu kila siku yanapigana hayo hayo tuuuuu iwe Uarabuni iwe SA iwe UK
Mchezo gani hauna sheria za kueleweka? uongozi unakula deal na wapiganaji tena mbele ya kamera na ukumbi mzima unaona
Hivi unadhani kean aliingiaje na kutokea katikati ya ulingo kwa kupasua na kuanza kunvuta mke.wa daniel, angalia alipo angukia angalia na jamaa alipotokea
hivi unaamini ndoa za madiva wapiganaji ni kweli?
ZAKUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO
Hebu nishawishi labda nitakuelewa mkuu kwamba huu mchezo ni kweli tupu kama wanavyocheza michezo mingine ya mashindano