Wale wa taarabu!!!

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,905
13,949
wakuu kuna huu wimbo wa taarabu wenye maneno haya

...duka lako la asali sasa linanuka shombo...ukipewa bia mbili hujiwezi huna nyimbo...

....wanakugombania kama mpira wa kona...

nani aliimba huu wimbo na unaitwaje??
 
aiss utafiti hebu niitie mtu aje aniambie huu wimbo unaitwaje au hata aniwekee hapa niusikilize...
 
Last edited by a moderator:
wakuu kuna huu wimbo wa taarabu wenye maneno haya

...duka lako la asali sasa linanuka shombo...ukipewa bia mbili hujiwezi huna nyimbo...

....wanakugombania kama mpira wa kona...

nani aliimba huu wimbo na unaitwaje??

Nyama ya Bata ni tamu

TOT Taarabu
 
Ulipigwa na TOT Taarabu,aliimba Ally Star....

Kaka nilichanganya na Nyama ya bata maana ni mwimbaji mmoja na bendi ni moja

nadhani unaitwa ZUMBUKUKU/ZUMBWEKUKU

Ni kweli kabisa, wimbo umeimbwa naTOT Taarab, umetungwa, umetiwa muziki na umeimbwa na Ally Star, unaitwa Kala hasara (Mdogo wa kimo unamambo wewe).

wakuu nashukuru kwa michango yenu nimekipata kitu kinaitwa

wakuu na kitu chenyewe ndo hiki!ama kweli google iko juu unaweza ingia kwenye hiyo link ukasikiliza kitu kama wakipenda pia!!

KIITIKIO:

Ama kweli mlezi wako alokulea, Kala hasara
Ama kweli mwalimu wako alokufundisha, Kala hasara
Ama kweli mzito wako alokulea, Una mambo
Ama kweli mchumba wako ulompata, Kala hasara

Mdogo wa kimo una mambo wewe, una mambo wewe, una mambo

Nimeshaamini chochote kizuri hakikosi kasoro
Mama mkata umoja kala hasara huyo
Mtega uchumi kumbe nawe umo
Japo hauvumi kumbe nawe umo
Huko mitaani umepewa jina waitwa mama huruma we

Sikutegemea wala sikudhani kama una mambo

Wala hufanani na jambo la mtoto, una mambo wewe

Kila uonacho, Wakitolea macho wataka kukichukua
Japo siyo chako, Wakitolea macho wataka kukichukua

MABETI

1. Nilidhani mimi chanda Na wewe ni pete yangu
Nikawa ninakupenda Kukuona u mwenzangu
Kumbe nimefuga donda Lilowashinda wenzangu
Ikawa wagawa tenda Hata kwa rafiki zangu
Ikawa wagawa tenda Hata kwa wadogo zangu
Toka bibi fanya nenda Bora niishi kivyangu
Mimi sili vya kuvunda Hili ni zindiko langu
Wewe si mtu ni sanda Na hofu uhai wangu

2. Si kama nakutania Nakueleza bayana
Kwa kweli sikudhania Kama huna maana
Kumbe wewe kisinia Kote unajulikana
Umekuwa zabania Kugonganisha mabwana
Wewe siwakutania Wengi wanapongezana
Wanavyokugombania Kama mpira wa kona
Umegeuka gunia Kubeba kila aina

3. Mambo yako yanatanda Yazagaa kama wingu
Hupumziki kuranda Kutwa kucha wanguwangu
Unachokijua kwenda Huoni hata uchungu
Mgongo umekupinda Kwa kutaka vya uvungu
Pepo aliekupanda Hapungwi hata kwa nyungu
Nakuambia utakonda Huwezi ulimwengu
Umekuwa paka nunda Wa kunusanusa vyungu

4. Duka lako la asali Sasa linanuka shombo
Waja wamekutapeli Usiyepitwa na jambo
Hivi sasa huna dili Yanakuendea kombo
Ukipewa bia mbili Umekwisha huna nyimbo
Wajanja wenye akili Wanakuuza kimombo
Hujui lile na hili Kazi kufuata mkumbo
Umegeuka egoli, Hupigwi la mgambo

Source: Sikutegemea wala sikudhani kama una mambo. Japo hauvumi kumbe umo? - wavuti.weebly.com
 
wakuu kuna huu wimbo wa taarabu wenye maneno haya

...duka lako la asali sasa linanuka shombo...ukipewa bia mbili hujiwezi huna nyimbo...

....wanakugombania kama mpira wa kona...

nani aliimba huu wimbo na unaitwaje??

Hao ni TOT chini ya Ally Star!!!Na jina la wimbo ni"hawavumi lkn wamo"
 
Back
Top Bottom