Wale Tuliosoma sana O-level tukapelekwa shule za Vipaji, Huko Nature ikatuchagua

Nilijichanganya kuhama shule fulani hivi ipo katavi nikiwa '0' Level nikahamia Shybush(Shinyanga) secondary shule ya vipaji maalum kilicho nikuta Mungu ndiye anajua, nmehamia sijasoma wala nini alafu nilikuwa Form 2 nkakuta mijamaa imecover topic , nilianza kuchezea 20% hv,30% nikawa nafunga kamkia kidogo.

Ila nashukuru nilipata ki division 3, nikasema shule usinitanie hapo hapo nikaenda zangu chuo sector ya Afya, maana ningeenda 'A' level ningewazungushia viuno mpaka wangenikubali .

Sent using Jamii Forums mobile app
Shybush siyo shule ya vipaji wewe dogo. Shule za vipaji kwa wavulana ni nne tu; Ilboru, Mzumbe, Kibaha na tabora Boys. Na kwa wasichana ni Msalato na Kilakala. Ingawa wadau walishasema hamna umalumu bali kusongoka na kufauli mitihani ya NECTA maana huku mtaani wameshindwa hata kugundua dawa ya CORORA. Wote wanapiga nyungu na Msukuma aliyeishia darasa la nne B.
 
Kupata scholarship Kwa PCB n ngumu,labda PCM....mm nliingia top ten Kwa PCB,nikaanza kufatilia scholarship za nje,nikapata ya USA,inshu ikaja kuwa kama hii secondary education hujasomea USA inabid uende pre medical school miaka minne then ndio uingie medical school miaka mingine minne then ufanye intern,yaan utumie miaka 9 kusoma degree Moja na ukirudi bongo hiyo MD ya huko wanaweza kukwambia upige intern tena,infact n almost 10 yrs kusoma degree Moja wakati ukisomea muhas hyo 10 yrs utakuwa unamaliza kuwa super specialist...

Lkn pia wale jamaa walinuambia "sisi tunaweza kukulipia pre medical school miaka minne,je hyo minne mingine ya medical school utaweza kujilipia??"namm kwetu n kijijini,hzo ada za USD nitoe wapi,so nikaunga muhas...


So scholarship for undergraduate n ngumu hasa za kulipiwa,labda uende china na urusi.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Huenda
 
Ni ngumu kuelewa/ kuamini ila kati ya watu waliojutia kusoma sana na kufaulu vizuri ni mimi.

Nilitumia nguvu nyingi kusoma O-level, na kweli nguvu zile hazikwenda bure, Nilichomoka na div 1.11, shule ya hovyo hovyo na hakuna aliyewahi pata hio tangu ianze.

Ilikua shangwe, kitu ambacho nilikuja kushukuru baadae sikuonesha masifa mtaani kipindi nilivyo faulu form 4 na hata watu wengi hawakujua.

Mzee baba nikapelekwa PCB shule kubwa ya vipaji maalum, nilifurahi sana nisijue kumbe nimejipeleka bucha na panga langu.

Sasa kule ndio Nature ika ni select, test ya kwanza nikala za uso, ndio nilifaulu lakini nahisi nilikua wa mwisho, maana kila unayemwona Kapasua si mchezo, ya pili ile nili confirm kabisa ile nimefunga kitasa.

Sikuamini macho na akili yangu, kama ni mimi wa kufunga dimba a.k.a kuzima taa? ingawa bado nipo juu ya wastani,

Sasa kuna Mwana nakaa naye karibu alikua na 66 yake akajua sijui ndio wa kwanza, bwana akaenda kwa vipanga wa darasa eti kuwachora sababu alisikia wakilalamikiana kuwa nimefeli, asijue kuwa ni kufeli katika next level ya battle lao wenyewe yeye alidhani ni wastani akajipeleka.

Anafika huko mwenye ndogo ana 93, alirudi taratibu kinyume nyume akakaa kwenye dawati akainama nikamwona anatafuna mtihani wake, Nilikua kila nikimwona nakufa kwa kicheko, Hakumaliza week akahama.

Nikajiuliza hawa watu ni wa namna gani? Ni kweli nilizembea sana katika usomaji zaidi hata ya vipanga wenyewe na mbaya zaidi kumbe wana walipiga twitions karibuni topic zote za form V kabla hata ya kuanza shule, lakini hili gap ni kubwaa, zikaja test nyingine nazo ni kukimbizwa tu.

Nikaona hapa nitaaibika mzee mzima, nikaanza kusoma upepo, uzuri Science hasa PCB tulikua wengi, nikagundua kuna mananga kama mimi na wengine ni zaidi yangu tuliofaulu kwa sifa.

Nikasema sasa hawa ndio guard yangu huku nyuma, nisije nikawa wa mwisho, pale ndio nikafufua ule msuli tena.

kwa kweli awamu hii Matokeo hayakuendana na Jitihada, Binafsi chemistry ndio ilinitesa zaidi kwenye mitihani, ila kwenye usomaji ni kawaida tofauti na physics iliyokua ngumu kwenye usomaji ila kwenye mtihani mambo kiasi yanashuka.

Zile njemba zilizo jaaliwa yaani kwao kila upande akishika kalamu ni kama inajiandika, unamwita mtu akuelekeze anakuja (uzuri sio wachoyo na uzuri zaidi mimi nilikua rafiki wa kila mtu) anakuelekeza speed anayoshuka nayo unaishia kuguna tu, kuna vitu unashindwa kuuliza maana unahisi atashangaa huyu jamaa amekujaje huku?..

Maisha yangu katika usomaji yalikua magumu sana, japo ya nje yalikua mazuri na ya furaha sana. Nilijitahidi sana kukaza, maajabu ambayo niliyafanyaga ni kuwa wa 8, baada ya hapo nikatupwa na sijawahi hata kuikaribia tena. Maana ile nafasi niliipata baada ya kujitesa sana.

Kwa kweli hapa nikakata tamaa, Tofauti na O-level masomo yalikua marahisi na unaokimbizana nao ni warahisi.

Huku masomo ni Jiwe, unaokimbizana nao ni Nondo, yaani huna pa kuchomokea. Nikaamua mimi ni kusoma tu na kufaulu hizi higher grades niwachie watabe, Ila hawa mananga wenzangu nihakikishe hawanipiti, basi...

Tatizo wengi walikua na roho nyepesi, wengi walihama, wengine walibadili Comb, kwahiyo kadiri wanavyopungua mimi nakaribiwa, maana anaacha nafasi moja nyuma, ikawa kila akiondoka mmoja naongeza kasi na wengi walikua wanatoka hizi St...... kuna jamaa mmoja yeye alizunguka round about kbsa, Hatukujua alipitia wapi na hatujawahi mwona tena. alituachia tu tranka lenye mazaga kama yote.

Mwisho wake nika ambulia 2 iliyochoka, wazee kama kawa ni div 1 na hata kwenye Top 10 walikuwepo, japo wengine walizingua pia.

Selection inatoka Natakiwa kwenda SUA tena, nikaona huu ni ujinga sasa, si ndio kule kule na watu wale wale, wengi sana naenda nao tena Course Moja, Yaani ilifika hatua nafikiria kuwakwepa sasa lakini wao walikua wanakubali sana kampani yangu.

Raha ya kusoma, ni kufaulu kadiri ya jitihada na mwishowe kupata kile unachotafuta...
kinyume na hapo ni msalaba, na mm elimu yangu ya advance ni niliiona kero...pale ndio niliamini kuna watu wamejaaliwa akili za darasani, sisi wengine tunasogeza tuu gurudumu..

Mwisho, ni matamanio makubwa sana kwa mzazi kua na mtoto mwenye jitihada darasani na baadae maisha kwa ujumla, na kwa kweli inaleta furaha sana, Pia nahisi uwezo wa mtoto kupambanua mambo umeunganika na mambo flani kutoka kwa wazazi na malezi labda.

Usione kila kijana mtaani akirudi likizo akakutajia shule nzuri na kubwa anayosoma ukasema kimoyomoyo huyu ni kichwa, Wengine ni wazunguka round about tuu, na wanachopitia huko wanakijua wenyewe.

Mwanao kama ni Nanga, usimlazimishe elimu unamtesa, ukimpatia ile basic ya kusoma, kuhesabu na kuandika ambayo ndio elimu kuu inatosha mtafutie njia nyingine, Narudia tena unamtesa mwanao, unamjengea hofu na dhana ya kushindwa kuanzia utoto matokeo yake anakua nayo na kujihisi yeye si chochote panapo wenzake.

Msikilize, msapoti kwa njia nzuri anayoihitaji, mfanye mshindi tangu utoto, Ushindi sio Darasani tu, mfanye Mshindi wa maisha.

Tusidanganyane, hakuna shule za vipaji maalum, ni shule za waliosongoka na kufaulu vizuri
Sent using Jamii Forums mobile app
Always alipenda kunambia Am 4 real yaan wew umebarikiwa akili za darasani.....ila hauna akili za maisha. Alipenda kunisimanga for sure nimebarikiwa akili za darasani......Ni Moja ya marafik zangu wakike....ni MWANAMKE Alie gundua kipaji ya kua nime barikiwa akili za darasani kuliko za maisha....
Tumepotezana miaka mingi sasa baba Ake alikua mtu mzito.... popote alipo ajue Am 4 real nowadays Nina akili za maisha.....
 
Aiseee sitasahau Loyola nimeingia kuna wahuni wamemaliza Topic za 5, mi sijui hata Topic 1
 
Halafu najiulizaga hawa jamaa vipanga wengi wao yan hawanaga majingambo kabisa,na wanaonekana simple sana......
 
Huwa inaumiza sana.
Unajipindaaaa unafaulu kiaina lakini wa mwisho nakumbuka matokeo yalivyotoka aliniangalizia jembe letu wakati ananipa taarifa kanipa kinyonge sana wakati nimefaulu vizuri tu lakini ndo wa mwisho nwisho tena.

Kusoma na watu wenye vipaji na wale wanaoanza advance wameshamaliza topics zote za form 6 wenyewe wanaita kucover inataka moyo.

Wewe unaingia class kujifunza mwenzako alishasoma topics zote ana fanya kureview past papers.

mama wawili
Nimecheka kwa sauti.
 
Dah mzee A level ni habari nyingine kabisa wengi wanaopita vizuri hapo ni kweli huwa wako vizuri hasa science kama PCB na PCM nakumbuka nimetoka O level na kadivision kangu mzee naingia darasani pindi la physics linapigwa naona nyotanyota tu piga test ya kwanza nikala zero hapo ndio akili ilikaa kabisa
Kunajamaa alitoka iyunga na 1.16,akapangiwa mkwawa miaka ya 2000 tulipo maliza2002 alitaga.😂😂😂😂😂
 
Primary nimekimbiza balaa sijawai kuwa wa pili nimesoma zangu private huko sina stress nikapata shule private nzuri tu bro mmoja akaniambia subiria uende gavoo shule zimetoka nikapangiwa ilboru nikaenda aisee nilichokikuta sitokaa nisahau huwezi amini mwaka mzima form 1 sijawai sogea ata top 50 nakumbuka hapo sijawai shuka no moja nilikotoka nilikuwa na stress balaa nikarudi home mlilia maza balaa akaniamisha akanipeleka private nashukuru mungu piga msuli form four nikafaulu vizuri.

Nikapiga interview marian boys nikapata mcheki mshua analeta story za kusubiria gavoo sijui hana hela nikatulia home piga topic za PCM kama kichaa shule zikatoka nimepata tena ilboru PCM. Nikaenda bila shida walahi nimeingia pale ule msuli sijawai uone popote watu wana bund mpaka asubuhi nakumbuka mimi nilimaliza topic za hesabu form five zote nikiwa likizo na physics form five.

Nimefika pale nakutana na majamaa wawili walipiga pale o level wakaingia top10 ***** maboya walikuwa wamemaliza topic zote mpak form masomo yote wao kila paper za form 6 wanaenda piga darasani kila mtu anajitamba sijui mimi ndo bigwa wa tabora sijui nimeongoza math kilimanjaro sijui mi ndo to wa PCM form four aisee ile experience ilinichanganya piga simu nyumbani omba kubadili combination niingie arts mzee akaniuliza kwa nini nikamwambia PCM ngumu siiwez kaniambia nirudi home akanitaftia prvate nzuri dsm kwa matokeo yangu haikuwa ngumu kuingia nikapiga nao paper la midterm hesabu na chemia nikafaulu wakanikubalia.

Advance ndio ni ngumu na nilisoma sana nikafaulu ila sipati picha ningemaliza pale ilboru ile shule nimeikubali na nimeshaapa ata mwanangu aoneshe vipi kufaulu kamwe siwezi mpeleka shule ya government kule watu wanapiga shule kama vichaa.

Nimekuja chuo nimekutana nao tena coet aisee majamaa wanapiga shule sijawai ona kuna jamaa nakumbuka first year yetu aligomga 4.9 coet ila msuli wake sio wa kitoto. Nashukuru Mungu chuo nilijitambua mapema na kamwe sijawai kujilinganisha na mtu nilisoma kwa uwezo wangu na kumaliza salama.

Ila mpaka kesho nawaheshimu sana vipanga wa hizo special schools hao majamaa ni noma
Kuna watu wanasoma utafikiri wanatafuta kazi kwa Elon musk yule jamaa wa Tesla.
 
Mbaya zaidi pale unapoanza form 5 unakutana na mtu unamuuliza umefikia wapi kusoma anakuambia yote nime_cover mpk form six ninachosubiri necta tu wakati wewe hata topic wala vitabu vya kusoma hauvijui, hapo utajua kuwa dunia haina huruma .
Kawaida Sana A-level science
 
Mm nlkuwa kama wewe...nmeingia o level vipaji maalumu nikitokea shule za kidumu na mfagio,aisee form one watoto karbu wote wametoka English medium,so niliteseka sana,nlkuwa nakuwa wa mwisho ila nilisoma mpk bhc,ikafikia kipindi mm kusoma mpk saa tisa usku kutokea saa mbili n kitu normal,Mungu sio Athman,jitihada zililipa so nikaanza kusogea taratibu,mpk tunamaliza form four niliongoza mm na div 1-9 so nikaenda vipaji maalumu tena ya juu zaidi ambayo n mzumbe....aloooh huko mateso kama ya form one yakaanza upya,naripoti tu form 5 PCB Kuna wadau wa pcm na PCB Tyr washamaliza topic zote za form five,wako wanasoma topic za mwsho za form six...

Wakati mm ndio naanza mechanics,miamba wapo topic za form six,anasovu electromagnetism na anafanya test na form six wanaotegemea kufanya necta inayofuata na wanapiga marks nzuri...I was severely depressed...

But to cut a long story short,mm nliamua kuongeza msuli,nasoma kuanzia saa mbili usku mpk saa tisa au saa kumi throughout...trust me,Ile tunamaliza form six,nikawaongezea mm na div 1-4,na nikaingia top ten kitaifa,hakuna aliyeamini Yale matokeo,hata mm mwenyewe siamini ilkuwaje..

Nikaingia muhas,alhadulilah nikasoma na kumaliza MD na GPA nzuri kidogo ya 4.1 japo chuo nlipunguza sana kusoma ,saa nne usku mwisho,nalala....

Kusema ukweli safari yangu ya elimu ilkuwa na mambo mengi mpk nikikaa huwa nasema groly to God...

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Naskrini nimuoneshe Binti yangu Yuko shule bweni anapenda udaktari mnooo
Ahsante bro

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yani kuna kitu umeandika hapo umenikumbusha mbali maana mm nimesoma izo vipaji, basi bwana pepar inarudi nina 83 ya chemistry form one nikasema mm si ndo wa kwanza sasa. Sasa mwalimu akabandika matokeo kuja kuchek mm wa 25 huko, wajinga wanasoma waleeeee asikwambie mtu. Nikaona hapa kumbe kukaza nilisomaaaa mpka kichwa kikawa kina mawenge yani nikikaa naona kama kina expand ivi. Nashukuru tulikuwa tunafunga shule midterm so nikapumzika kama wiki ivi ndo nikawa normal
 
Umeisahau Ilboru, nilikiwa na mjuba pale aiseeh ukiacha mistari aliyokiwa ananiimbisha, kipindi hicho yeye alikuwa anacheza na 90 kwenda juu, mwenyewe alikiwa anaita bouncing life yaani ananesanesa kati ya 100 na 90.

Sina hamu na wa kaskazini...

Alikiwa anajua Mahaba hatarii ila hakufanikiwa kuniambukiza ujiniasi wake mie nikaishia kidato cha pili... Poor Kasie.
Kwaiyo saivi upo na shimba sio 😹
 
Primary nimekimbiza balaa sijawai kuwa wa pili nimesoma zangu private huko sina stress nikapata shule private nzuri tu bro mmoja akaniambia subiria uende gavoo shule zimetoka nikapangiwa ilboru nikaenda aisee nilichokikuta sitokaa nisahau huwezi amini mwaka mzima form 1 sijawai sogea ata top 50 nakumbuka hapo sijawai shuka no moja nilikotoka nilikuwa na stress balaa nikarudi home mlilia maza balaa akaniamisha akanipeleka private nashukuru mungu piga msuli form four nikafaulu vizuri.

Nikapiga interview marian boys nikapata mcheki mshua analeta story za kusubiria gavoo sijui hana hela nikatulia home piga topic za PCM kama kichaa shule zikatoka nimepata tena ilboru PCM. Nikaenda bila shida walahi nimeingia pale ule msuli sijawai uone popote watu wana bund mpaka asubuhi nakumbuka mimi nilimaliza topic za hesabu form five zote nikiwa likizo na physics form five.

Nimefika pale nakutana na majamaa wawili walipiga pale o level wakaingia top10 ***** maboya walikuwa wamemaliza topic zote mpak form masomo yote wao kila paper za form 6 wanaenda piga darasani kila mtu anajitamba sijui mimi ndo bigwa wa tabora sijui nimeongoza math kilimanjaro sijui mi ndo to wa PCM form four aisee ile experience ilinichanganya piga simu nyumbani omba kubadili combination niingie arts mzee akaniuliza kwa nini nikamwambia PCM ngumu siiwez kaniambia nirudi home akanitaftia prvate nzuri dsm kwa matokeo yangu haikuwa ngumu kuingia nikapiga nao paper la midterm hesabu na chemia nikafaulu wakanikubalia.

Advance ndio ni ngumu na nilisoma sana nikafaulu ila sipati picha ningemaliza pale ilboru ile shule nimeikubali na nimeshaapa ata mwanangu aoneshe vipi kufaulu kamwe siwezi mpeleka shule ya government kule watu wanapiga shule kama vichaa.

Nimekuja chuo nimekutana nao tena coet aisee majamaa wanapiga shule sijawai ona kuna jamaa nakumbuka first year yetu aligomga 4.9 coet ila msuli wake sio wa kitoto. Nashukuru Mungu chuo nilijitambua mapema na kamwe sijawai kujilinganisha na mtu nilisoma kwa uwezo wangu na kumaliza salama.

Ila mpaka kesho nawaheshimu sana vipanga wa hizo special schools hao majamaa ni noma
Huyo wa coet alikuwa best student sio mkuuu 😂😶
 
Back
Top Bottom