Wale Tuliosoma sana O-level tukapelekwa shule za Vipaji, Huko Nature ikatuchagua

Nimetoka zangu form IV nimepiga vizuri sanaa,nikachaguliwa shule sana.Picha linaanza kufika tu kule nikakuta jamii ya watoto wa Arusha wanajuana wenyewe mana wametoka mkoa mmoja afu wana ushirikiano kinyama yani."Wame-cover" kila kitu kasoro GS tu,..
hawakua na connection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Primary nimekimbiza balaa sijawai kuwa wa pili nimesoma zangu private huko sina stress nikapata shule private nzuri tu bro mmoja akaniambia subiria uende gavoo shule zimetoka nikapangiwa ilboru nikaenda aisee nilichokikuta sitokaa nisahau huwezi amini mwaka mzima form 1 sijawai sogea ata top 50 nakumbuka hapo sijawai shuka no moja nilikotoka nilikuwa na stress balaa nikarudi home mlilia maza balaa akaniamisha akanipeleka private nashukuru mungu piga msuli form four nikafaulu vizuri.

Nikapiga interview marian boys nikapata mcheki mshua analeta story za kusubiria gavoo sijui hana hela nikatulia home piga topic za PCM kama kichaa shule zikatoka nimepata tena ilboru PCM. Nikaenda bila shida walahi nimeingia pale ule msuli sijawai uone popote watu wana bund mpaka asubuhi nakumbuka mimi nilimaliza topic za hesabu form five zote nikiwa likizo na physics form five.

Nimefika pale nakutana na majamaa wawili walipiga pale o level wakaingia top10 ***** maboya walikuwa wamemaliza topic zote mpak form masomo yote wao kila paper za form 6 wanaenda piga darasani kila mtu anajitamba sijui mimi ndo bigwa wa tabora sijui nimeongoza math kilimanjaro sijui mi ndo to wa PCM form four aisee ile experience ilinichanganya piga simu nyumbani omba kubadili combination niingie arts mzee akaniuliza kwa nini nikamwambia PCM ngumu siiwez kaniambia nirudi home akanitaftia prvate nzuri dsm kwa matokeo yangu haikuwa ngumu kuingia nikapiga nao paper la midterm hesabu na chemia nikafaulu wakanikubalia.

Advance ndio ni ngumu na nilisoma sana nikafaulu ila sipati picha ningemaliza pale ilboru ile shule nimeikubali na nimeshaapa ata mwanangu aoneshe vipi kufaulu kamwe siwezi mpeleka shule ya government kule watu wanapiga shule kama vichaa.

Nimekuja chuo nimekutana nao tena coet aisee majamaa wanapiga shule sijawai ona kuna jamaa nakumbuka first year yetu aligomga 4.9 coet ila msuli wake sio wa kitoto. Nashukuru Mungu chuo nilijitambua mapema na kamwe sijawai kujilinganisha na mtu nilisoma kwa uwezo wangu na kumaliza salama.

Ila mpaka kesho nawaheshimu sana vipanga wa hizo special schools hao majamaa ni noma
 
Mleta mada unanikumbusha mbali sana.
Sikwenda shule ya vipaji maalum ila ni shule flani watu wake na shule yenyewe huji-grade kama vipaji maalum.

Nilipata tabu sana, narudia tena A'level nilipata tabu mnoooo

Wale wenzangu namimi walikuwa wanaji-boost kwa kwenda mchikichini kupiga kitabu kwa akina Mbuga chemistry, sijui Muddy Physics
Sasa mimi kijijin hata nikimwambia mzee nataka hela ya tuition anaona kama utapeli maana huko mwanzo sikuwahi kusoma tuition, akijitahidi sana anatuma 20K kupitia NMB (enzi hizo mpesa wala tigopesa hazijaanza) sasa ukienda kuitoa inatoka 15K hiyo utasoma sub-topic mbili za Physical chemistry hela imekata, bado nauli bado kula mihogo.

Katika kusoma kwangu sitaisahau A'level japo nilifaulu kwenda kile chuo wanaita cha Taifa lakini A'level sina hamu nayo

Sent using Jamii Forums mobile app

A level in kisanga mkuu
 
Primary nimekimbiza balaa sijawai kuwa wa pili nimesoma zangu private huko sina stress nikapata shule private nzuri tu bro mmoja akaniambia subiria uende gavoo shule zimetoka nikapangiwa ilboru nikaenda aisee nilichokikuta sitokaa nisahau huwezi amini mwaka mzima form 1 sijawai sogea ata top 50 nakumbuka hapo sijawai shuka no moja nilikotoka nilikuwa na stress balaa nikarudi home mlilia maza balaa akaniamisha akanipeleka private nashukuru mungu piga msuli form four nikafaulu vizuri.
Nikapiga interview marian boys nikapata mcheki mshua analeta story za kusubiria gavoo sijui hana hela nikatulia home piga topic za PCM kama kichaa shule zikatoka nimepata tena ilboru PCM. Nikaenda bila shida walahi nimeingia pale ule msuli sijawai uone popote watu wana bund mpaka asubuhi nakumbuka mimi nilimaliza topic za hesabu form five zote nikiwa likizo na physics form five. Nimefika pale nakutana na majamaa wawili walipiga pale o level wakaingia top10 ***** maboya walikuwa wamemaliza topic zote mpak form masomo yote wao kila paper za form 6 wanaenda piga darasani kila mtu anajitamba sijui mimi ndo bigwa wa tabora sijui nimeongoza math kilimanjaro sijui mi ndo to wa PCM form four aisee ile experience ilinichanganya piga simu nyumbani omba kubadili combination niingie arts mzee akaniuliza kwa nini nikamwambia PCM ngumu siiwez kaniambia nirudi home akanitaftia prvate nzuri dsm kwa matokeo yangu haikuwa ngumu kuingia nikapiga nao paper la midterm hesabu na chemia nikafaulu wakanikubalia.
Advance ndio ni ngumu na nilisoma sana nikafaulu ila sipati picha ningemaliza pale ilboru ile shule nimeikubali na nimeshaapa ata mwanangu aoneshe vipi kufaulu kamwe siwezi mpeleka shule ya government kule watu wanapiga shule kama vichaa.
Nimekuja chuo nimekutana nao tena coet aisee majamaa wanapiga shule sijawai ona kuna jamaa nakumbuka first year yetu aligomga 4.9 coet ila msuli wake sio wa kitoto. Nashukuru Mungu chuo nilijitambua mapema na kamwe sijawai kujilinganisha na mtu nilisoma kwa uwezo wangu na kumaliza salama.
Ila mpak kesho nawaheshimu sana vipanga wa hizo special schools hao majamaa ni noma

Hahaha mkuu hao ndio wale wanaotumwa na ukoo.Lazma wakamue tu.
 
Hahaha mkuu hao ndio wale wanaotumwa na ukoo.Lazma wakamue tu.

Mzee acha tu kuna jombaa alikuwa coet kapiga ilboru alituwashia moto first year kagonga 4.9 sijawai ona mimi uwezo wangu darasani haujawai kuwa na mashaka ila huyu jamaa ni noma ogopa mtu mnasoma wote darasani ila yeye ni kama mwalimu wenu anajua kila kitu ni balaa nashukuru tu mungu chuo sijawai kupenda kushindana kama seko dari uko ningekufa kwa presha. Kuna watu wamebarikiwa nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahaha...dah nilikuwa nakimbiza sana primary, nikabahatika kuchaguliwa shule 1 inaitwa ILBORU ipo arusha....shule flani hiv miongoni mwa shule nne bora za serikali , nlokutana nayo kule mungu ndo anajua, kuna watu wanaakili askwambie mtu, sna tofauti saaana na mtoa mada alopitia yeye nahis tunafanana,

Ilifkia kipind mpka nataman kurud shule yang ya kata...bt Alhamdulillah tulvyfika form 3 nkawa naenda nao sambamba tu, chuoni nako hakubagui kule hakuna kilaza bt ukiwa active una enjoy maisha...daah madulu kombe, kulwa mipawa, hillary hiera,hilmi abdallah...jamaa walitutesa sana ilboru,...salute kwao asee...

Sent using [Samsung galaxy s10]
 
Back
Top Bottom