Rwaz
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 1,969
- 3,320
Hata hivyo tuko katika nyakati za ndoa hatarishi tena za kukusababishia maradhi, msongo au kifo cha mapema kiasi kwamba hata mafanikio mengine kama mali na fedha yasiwe na tija kwako hapa duniani.
Basi kama tunakubaliana asiyeoa/asiyeolewa amejiepusha na mengi imebaki ni miundombinu gani mhusika na jamii tuwekeane ili ukifika hatua ya kuhitaj usaidizi nguvu zimekata bado uzipate. Nashauri tuanze na BIMA ya kutunza wazee. itasaidia sana. ikibidi ukizeeka pesa zako zikuogeshe, zikusafishe, zikulishe bila kulia lia kwa kila mtu awe ndugu au rafiki na jamaaa tena wanaotamani ufe wale vyako.
Tufike mahali jamii iaminishe kizazi cha leo na kesho kuwa ndoa si lazma wala si mafanikio(bali mafanikio ni kuishi vyema katika ndoa hiyo). Kuzaa si lazma hata unyanyasaji wa kijinsia utapungua hata wanaoweka ukosefu wa ndoa kwenye mikosa watapumua. KWA MAANA JAMBO MUHIMU KATIKA MAISHA NI MOJA TU ...KUWA NA FURAHA!
Pia soma:
Kwani lazima kuoana?
Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wa maisha
Nini faida ya kuoa kwa sisi wanaume?
Almost vitu vyote ndani ya nyumba unaweza fanya mwenyewe kama kupika, kufanya isafi nyumbani kwako, kuhudumia mifugo, shambani, ndugu jamii na marafiki zako so unapooa unaongeza faida gani kwenye nyumba yako? Kama ishu ni mwanamke basi unaweza nunua huko utimize haja zako! Kama ni watoto...
www.jamiiforums.com
Je, ni nini hasa faida ya kuoa?
Habari wakuu, Mimi ni kijana niliyefikisha umri wa kuoa nina 27 kwa sasa, ni kwamba familia na jamii inayonizunguka naona wananisisitiza sana nioe eti kwakuwa nina kazi nzuri na ninajimudu kimaisha. Lakini kwa mtazamo wangu sioni ka kuna ulazima katika hili ukizingatia chochote ninachokitaka...
www.jamiiforums.com