Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

ikhlas

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,038
1,278
Habari wanabodi wenzangu, Katika maisha kuna kuoa na kuolewa, hivyo kuna kutoa talaka na kupewa talaka.

Katika hali zote hizo maisha yanaendelea, kuna ambao hufanikiwa zaidi au kurudi nyuma kimaisha chanzo kikiwa ni talaka. Changamoto na faida pia hujitokeza, wengine hufikia hali kujuta kwanini wametoa talaka au kupewa talaka, lakini pia kuna wengine hufikia mahali husema bora alivyoacha au kuachika.

Wengine wanashindwa kumove on wanabaki na majeraha milele, wengine hupoteza watoto, mali na kazi bada ya talaka.

Karibuni wadau tuliowahi kuingia kwenye ndoa na kukutana na talaka au kuachana na wenza wetu ambao tulidhani tutazikwa nao.

Pia wapo watoto humu ambao walishuhudia wazazi wao wakipeana talaka, je maisha yalikuaje?

1656103201451.png
 
Kutoa talaka sio Jambo la kufurahisha hata kidogo, kwani mwenye anatoa anaumia na anaepokea anaumia vile vile, hakuna mtu ambaye Ni mbaya totally

Kunayo mazuri kadhaa anakua nayo lakini anapokua anakosea mtu unaamua kumhukumu kwa makosa yake ya mwanzo na mnadivorce ,

Soon mnapoachana ndipo utaanza kugundua gap imejitokeza,utaanza kugundua baadhi ya action nzuri alzokua nazo mtalaka wako,utaanza kuumia na wewe japo utajipa matumaini kwa kujikumbusha mabaya yake,
Apo Kama mlikua na watoto hio Ni mada nyingine kabsa na changamoto zake Ni hazielezeki,.

Talaka Ni chungu kwa anaetoa na anaepokea ,tofauti yake Ni mtoaji atakua anafrai wakati wa kutoa while mpokeaji anaumia ila baada ya muda Ni either wote watakua wanaumia au mpokeaji atakua ashapona na alietoa anajutia.
 
Kutoa talaka sio Jambo la kufurahisha hata kidogo, kwani mwenye anatoa anaumia na anaepokea anaumia vile vile,hakuna mtu ambaye Ni mbaya totally

Mkuu unadhani kuna hali inafika ni lazima kutoa talaka?Nauliza hvyo kwa sbb kuna badhi ya dini na mila talaka ni mwiko, naniuliza inapofika kipindi ambacho hakuna anaemtaka mwenzak nini kifanyike?Au talaka ni sehem ya solution
 
Habari wanabodi wenzangu,Katika maisha kuna kuoa na kuolewa, hivyo kuna kutoa talaka na kupewa talaka.

Katika hali zote hizo maisha yanaendelea, kuna ambao hufankiwa zaidi au kurudi nyuma kimaisha chanzo kikiwa ni talaka.Changamoto na Faida pia hujitokeza, wengine hufikia hali kujuta kwann wametoa talaka au lupewa talaka.,lkn pia kuna wengine hufikia mahali husema bora alivyo acha au kuachika.

Wengine wanashindw kumove on wanabaki na majeraha milele, wengine hupoteza watoto, mali na kazi bada ya talaka.

Katibuni wadau tuliowahi kuingia kwenye na kukutana na talaka au kuachana na wenza wetu ambao tulidhani tutazikwa nap.

Pia wapo watoto humu ambao walishuhudia wazazi wao wakipeana talaka ,je maisha yalikuaje??

Wewe mbona hujatoa upande wako ilikuwaje?
 
Talaka isikisge kwa mtu mwingine tena bora mpeane talaka kabla hamjachuma mali nyingi au za gharama kubwa ambapo kiuhalisia mwanaume ndiye huwa amevujisha jasho jingi! Tena itokee mwanamke alikuwa na ajira hata kama ni ps wa mlinzi (salary kima cha chini kabisa) na wewe ofisa wa ngazi flani ya juu!

Sote tunajua wanawake wengi hata awe na ajira mshahara wake ni kwa ajili ya nguo na vipodozi, lakini wakifika mahakamani hao huongea uwongo mkavu anaweza hata kusema ulikuwa ulishamnyanganya kadi ya benk na mshahara wake hakua anagusa hata mia!

Mgao wa mali katika mazingira kama hayo huwa unauma sio mchezo!
 
Mkuu unadhani kuna hali inafika ni lazima kutoa talaka?Nauliza hvyo kwa sbb kuna badhi ya dini na mila talaka ni mwiko, naniuliza inapofika kipindi ambacho hakuna anaemtaka mwenzak nini kifanyike?Au talaka ni sehem ya solution
Mmoja akishashitaki mahakamani na kufungua kesi rasmi tayari mpaka hapo talaka haikwepeki labda tu kabla ya kesi kufika mwisho ninyi wenyewe muamue kuiondoa kesi mahakamani! Hapa ninamaaisha mahakama ndio itakulazimisha kutoa talaka kwa mujibu wa sheria na itazigawa mali zenu hata kama utazuia vipi!
 
Kutoa talaka sio Jambo la kufurahisha hata kidogo, kwani mwenye anatoa anaumia na anaepokea anaumia vile vile,hakuna mtu ambaye Ni mbaya totally
Kunjutia.
Umeeleza vizuri sana mkuu,kiufupi ndoa ni kama vile kazi,unaweza kuiona mbaya wakati unayo lakini ukishaacha ndio unagunduwa uzuri wake.Mara nyingi mpaka mnafikia kutalikiana shetani anakuwa ndani yenu kwa kiwango cha juu sana,na kwakuwa hamkumtanguliza Mungu kwenye maisha yenu inakuwa ni rahisi sana kutoleana talaka,lakini baada ya pale utagundua vizuri vyote vilivyokuwepo kwa mwenzio.
Na mara nyingi move unayokwenda kuifanya ya kuchukua mtu mwingine,ukiifanya kwa papara majuto yake huwa ni mabaya sana,labda tu kama utafanikiwa kumpata mtu sahihi.Ndio maana hata katika Kitabu cha Malaki 2:16 Mwenyezi Mungu anasema nachukia kuachana...
 
Mkuu unadhani kuna hali inafika ni lazima kutoa talaka?Nauliza hvyo kwa sbb kuna badhi ya dini na mila talaka ni mwiko, naniuliza inapofika kipindi ambacho hakuna anaemtaka mwenzak nini kifanyike?Au talaka ni sehem ya solution
Upo wakati talaka inakua ndo solution kwa iliobakia kweli,,mfano ukigundua mwenzi wko Ni mshirikina ,au anaplan za kukuua,lazma ukimbie bill kujiuliza mara mbili
 
Upo wakati talaka inakua ndo solution kwa iliobakia kweli,,mfano ukigundua mwenzi wko Ni mshirikina ,au anaplan za kukuua,lazma ukimbie bill kujiuliza mara mbili
Haya ni mazito mkuu
 
Back
Top Bottom