Wakwe wamekataa!

sababu za wao kupinga hasa baba ni kuwa usioe mwanamke wa mbeya atakusumbua sana kama ambavyo yeye amekuwa anapata taabu na mama yetu for the past 40 years za marriage yao..I decided not to buy that advice and i move in a different way..Mama was opposing because i converted form being a muslim to christian so that i marry ze maywaifu
 
Ukiwa na sifa na wazazi wanakuzuia kutokana na umaskini ulio nao kwa mfano binti kwao mambo safi dawa na kupiga vitu binti awe mjamzito kisha unakabidhiwa bureeeeeee.
 
Kuna mambo matatu hapa... jamii, familia na wawili wanaopendana.

Ukioa bila ya ridhaa ya wazazi, familia itawatenga...are you ready for this?

Kwa sababu hali hii ya kutengwa itaadhiri uhusiano wenu msipokuwa makini. Mnahitaji kutafuta njia zote ziwezekanazo ili wazazi wenu wabadilishe maaumizi yao.

Wakikataa, inabidi you do what you have to do ila hakikisha kama ni ndoa iwe halali mbele ya mungu na nchi

Mkishapata watoto, wazazi haswa mama atakuwa na huruma na hamu ya kumwona mjukuu wake.... lakini kuoa bila ridhaa ya wazazi iwe ni the last option
 
ukiwa na sifa na wazazi wanakuzuia kutokana na umaskini ulio nao kwa mfano binti kwao mambo safi dawa na kupiga vitu binti awe mjamzito kisha unakabidhiwa bureeeeeee.

wengine wenye misimamo mikali wako radhi watunze binti na mjukuu ila wewe no!
 
WOS mi nadhani watoto wenyewe ndo wata determine hiyo decency basi...parents cannot do that..Ni mtazamo wangu
 
Mkuu Fidel hiyo nayo imetulia kama wanaleta mlolongo wazazi..Unapiga kitu unatulia kama sio wewe vile wenyewe watakufuata...Hahaaaa you make me laugh today
 
Wenyewe mkipendana, hakuna atakayeweza kuwaachisha, awe mzazi au mkwe. Watagoma mwanzoni lkn wakishaona msimamo wenu wenyewe watakubaliana na nyie.
 
Zamani watu walikuwa wanaoa/olewa kijijini au kijiji cha jirani na wazazi walikuwa katika nafasi kubwa ya kumfahamu mchumba wako na familia/ukoo wake vizuri zaidi kuliko kijana.

Lakini kwa sasa mambo yamebadilika sana. Mara nyingi tunawapelekea wazazi watu (wachumba) wageni kabisa (labda tumekutana shule au kazini nk). Katika situation kama hii, mara nyingi wazazi wanafanya maamuzi/wanatoa ushauri kwa kuzingatia zaidi stereo types za makabila ama koo (mf kabila fulani wachawi, wazinzi, wanamaringo), dini, mwonekano wa nje (labda kijana ni brazameni, bishoo nk), kazi, uwezo wa kifedha nk.

Hata kama hukubaliani na wazazi ni vema ukawasikiliza na utoe sababu ni kwa nini unaona sababu zao za kukataa sio za msingi.
 
Mkuu Fidel hiyo nayo imetulia kama wanaleta mlolongo wazazi..Unapiga kitu unatulia kama sio wewe vile wenyewe watakufuata...Hahaaaa you make me laugh today

Mkuu hii ni bomba sana lakini hakikisha kuwa huyu mchumba ako asiwe mwanafunzi akiwa dent dah utaozea sello mkuu maana pesa itatembea mpaka kwa mgambo.
 
Wenyewe mkipendana, hakuna atakayeweza kuwaachisha, awe mzazi au mkwe. Watagoma mwanzoni lkn wakishaona msimamo wenu wenyewe watakubaliana na nyie.

...yataka moyo, kuna wazee wanagomea na kujiapiza, "kama wewe hujatoka kwenye tundu hii, si mwanangu na ukaolewe/ukamuoe huyo mtu wako!"
 
Tatizo ni kwamba for some parents it's hard to let go. Unakuta mzazi ana tegemea mtoto atam tegemea kwa kila kitu kama alivyo kua mchanga. Ukiwa mdogo kila kitu lazima uombe ruhusa na wazazi ndiyo final say katika everything in your life. Sasa basi for most parents wenye mentality hiyo ikifika kwenye ndoa ndiyo the last time they think they have any control over you kwa hiyo unakuta wana jaribu kuexcercise that control. It's a matter of some parents being controlling na kutegemea milele wao watakua the final say in a child's decisions. Inafika muda mzazi anabidi ajifunze kuwa mtoto nae ana maisha yake na ikifika wakati fulani mzazi anakua in an advisory position tu na si zaidi ya hapo. Wazazi wengine ni ubabe tu kwa sababu wewe ndiyo unam fahamu binti/kijana sasa iweje mzazi awe better judge ya anaye kufaa zaidi ya wewe? Hiyo wazazi kumkataa mchumba na baadae penzi likaingia dosari most of the times ni coincidence unless kama kweli the parents walikua na sababu nzito.Pili kila mtu ana taste tofauti, the kind of man/woman a person wants lazima ita tofautiana na wazazi. Una kuta saa nyingine mzazi kama baba ana taka kijana aoe mwanamke which ni taste yake na hali kadhalika mama kwa binti yake. Only you can make the right choice because you are the one who knows what kind of man/woman you like. Saa nyingine wazazi wana force qualities una kuta wala kijana hana time nazo.
Word of advise to parents, bora mtu afeli mwenyewe ajue amefeli kutokana na mapungufu yake kuliko kufeli akijua ime sababishwa na mwingine. Leo mniforce nioe mwanamke fulani ndoa ikanishinda si nita walaumu nyie? It's better I make my own choice so I have nothing to blame but myself. The parents job is to give life to a child but not live that child's life for them. Nashukuru Mungu mimi nina wazazi ambao wana nipa ushauri kwa mapenzi yote lakini hawa lazimishi chochote. Wazazi wajifunze kulet go mtu afikapo umri fulani.
 
...unauchukuliaje msimamo baba mkwe au mama mkwe anapokataa kata kata binti yake asiolewe na fulani, au mwanawe (wa kiume) asimuoe fulani.

...ni sahihi kwa wachumba hao kuoana bila ridhaa ya mzazi/wazazi hao?

...kwa experience yako, nini 'repercussions' za maamuzi hayo?

Mbu, kwa maoni yangu ni msimamo uliopitwa na wakati. Watoto nao waachiwe wafanye maamuzi yao wanapofikia umri wa utu uzima bila ya kuingiliwa na Wazazi. Kwenye maamuzi unaweza ukafanya maamuzi ambayo baadaye ukayafurahia na baadaye ukayajutia, lakini hayo ndiyo maisha kwamba kama binadamu hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ambayo siku zote yatakuwa 100% right.

Kama wana mapenzi ya kweli kati yao basi kwa maoni yangu wanaweza kuoana bila ridhaa za wazzai maana wazazi wengine hutaka kuendelea kuwacontrol watoto wao hata wanapokuwa watu wazima katika maswala mbali mbali likiwemo la kuwachagulia mume/mke

Wakati mwingi wana ndoa hao ambao wameoana bila ridhaa za wazazi wao hujitahidi sana ili kuhakikisha ndoa yao inafanikiwa ili kutowapa opportunity wazazi wao ya kusema "I TOLD YOU SO!" na hukutaka kutusikia.
 
Wazazi wengine wanakuwa hawana sababu za maana basi tu ameamua, Ndo maana wazazi wanatuambia unapoanzisha uhusiano tafuta mtu ambaye style yenu ya maisha inafanana asije akakupeleka kwao wakakukataa, kuna vitu vya muhimu unatakiwa uvizingatie.mara nyingi imetoke wazazi matajiri wanakataa watoto wao wasioe familia duni.
 
...Bonnie1974, picture yourself ukiwa ni mzazi, halafu anamleta mchumba ambaye yeye anaamini anamfaa kuwa wake wa maisha.

...ni vipimo gani utatumia kujua kweli wapo serious kwenye mahusiano yao na kwamba huyo mwenza anafaa kuwa mkweo, atayekujaalia wajukuu?
VIPIMO
1.Huyo kijana alete MKIA WA SIMBA
(kwa msaada wa wanaJF wengine "Mkia wa Simba" ni MZAZI.Hizo ni terms zinazotumika sana unapokwenda kuchumbia kwenye mji wa mtu.Kama ni kijana "wa hovyo" meaning usiyeshirikisha wazazi wako kwenye mambo kama hayo, utabaki unalalama, HOOH AMESEMA NIPELEKE "MKIA WA SIMBA" ,MIMI NITAPATA WAPI!!!!???)

2.Kitendo cha huyo kijana kukutana na mimi USO KWA USO nikiwa kwenye kale "kajumba kangu ka nyasi"(huwa na kuwa na "nguvu za Ajabu" kama Fisad....) ikifuatiwa na Q & A session .Mmhhh ,mtu akipita hapo na akarudi...HUYO MUOAJI.

Akifanya hayo Mkulu ,Ahhhh Mke kachukua.
 
tuacheni utani, sisi tunapenda kujifundisha kwa matatizo lakini hatutaki kuyaepuka matatizo, sidhani kama mtoto wa miaka 15 ana experience ya kutosha akamfundisha kijana mwenye 35yrs, na nina uhakika yale waliyokutana wazazi wetu hatujayafikia hata robo, ndo maana ukiwa mdogo ukisikia kua uyaone unakua uhelewi ukisha fika kwenye majukumu ya lazima ndo unatambua maana ya msemo huo,ila kuna sababu kama sababu lakini kama mzazi,mtu mwenye uzoefu tele wa maisha akikuambia kitu mfuatilize,hakuna mzazi anayemtakia mwanaye mabaya na ingekua kama hivyo wazazi wetu wangetu abort(abortion) kabla tujazaliwa, mimi binafsi kuna mwanamke nilimpenda nikapeleka picha kwa mzee kisha yule binti nikampeleka kwa mama,na ktk mahusiano yetu niligombana mpaka na ndugu zangu na mama kisa sitaki kumuacha,nikakubaliwa nimuoe huwezi amini wakati tunafanya process ya posa binti anakuja kunijulisha ndoa yake na bwana mwingine inafungwa next week, ila nilichojifunza mzazi inakua rahisi kumsoma mtu tabia yake in short period more than us,ambao tukishakua in love masikio na ubongo tunautia ganzi wa kutafakari ulichonacho, ila msimamo wangu utakua palepale mzazi hata akimkataa msichana wangu yoyote i will leave her for the sake of my mummy words.
 
Back
Top Bottom