tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Wakuu wa vyombo vya habari na wahariri waandamizi nchini Tanzania wamekutana leo oktoba 25, 2025 katika jengo la Millenium Tower Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na watanzania kupitia vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 29, 2025.
Tukio hilo lilikuwa na dhumuni la kuwakabidhi waandishi wa habari azimio lao lililoandaliwa kwa lengo la kuwaasa watanzania kulinda amani, utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kuwaomba kutoshiriki meza moja na wenye kauli zinazochochea kuvunjwa kwa amani
View: https://www.youtube.com/live/sxKRKH-U7MY
Azimio hilo limesomwa na mkuu wa wakuu wa vyombo vya habari TANGE likiwa limebeba mambo 11
===
Pia soma ~ Uchaguzi Mkuu wa 2025 na uadilifu wa Vyombo vya Habari Tanzania
Tukio hilo lilikuwa na dhumuni la kuwakabidhi waandishi wa habari azimio lao lililoandaliwa kwa lengo la kuwaasa watanzania kulinda amani, utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kuwaomba kutoshiriki meza moja na wenye kauli zinazochochea kuvunjwa kwa amani
View: https://www.youtube.com/live/sxKRKH-U7MY
Azimio hilo limesomwa na mkuu wa wakuu wa vyombo vya habari TANGE likiwa limebeba mambo 11
===
- Tanzania ilipata uhuru wake mwaka 1961 kupitia jitihada za majadiliano, mazungumzo na hoja za wanasiasa, wakipingana bila kupigana. Watanzania tuna wajibu wa kuendelea kujenga demokrasia yetu kwa majadiliano na hoja, tukipingana bila kupanga kupigana.
- Demokrasia yetu bado ni changa. (Demokrasia siyo kama mtoto wa nyumbu anayezaliwa sasa na hapo hapo akaanza kukimbia kwa kasi kama wazazi wake). Demokrasia ni mchakato endelevu unaopaswa kujengwa kila siku kwa kuhakikisha kila hatua inalindwa na wadau wote.
- Sisi Wakuu wa Vyombo vya Habari na Wahariri Waandamizi tuliokutana wiki hii, tunaamini katika kushamiri kwa demokrasia ya vyama vingi. Ni dhahiri kuwa vyombo vyetu vimetoa mchango mkubwa katika kuijenga na kuishamirisha demokrasia ya vyama vingi kwa miongo zaidi ya mitatu sasa.
- Tuliripoti na hata kuandika tahariri pale vyama vya siasa viliposuguana hasa nyakati za uchaguzi na kusababisha vurugu, kama ilivyowahi kutokea Zanzibar mwaka 2001 baada ya Uchaguzi Mkuu.
- Aidha, kwa muda mrefu vyombo vyetu vya habari vimeripoti sana matukio ya vurugu, uvunjifu wa amani, vita vya wao kwa wao na hata mauaji ya kimbari, kwenye mataifa mbalimbali ya Afrika, yaliyoathiriwa na siasa chafu na kuingiliwa na maadui wa nje. Kwa maneno mengine, machafuko, mateso na mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia katika nchi hizo, yalisababishwa na ubinafsi wa vikundi vya wanasiasa walioamua kutumia propaganda za kugawa watu, bila kujali maslahi mapana ya mataifa yao. Na ni dhahiri kuwa mataifa makubwa yakiwemo ya wakoloni yamekuwa yakichangia kuvuruga amani kwenye mataifa ya Afrika ili kuendeleza maslahi yao ya kiuchumi.
- Katika siku za karibuni, hapa Tanzania tumesikia kauli zinazochochea chuki na shari, jambo ambalo haliakisi kabisa utamaduni wa Mtanzania. Kauli zinazohamasisha wananchi kufanya vurugu, kuchoma vituo vya mafuta, vituo vya polisi na mali nyingine, siyo tu ni kosa kisheria, bali ni kauli zisizoakisi Utanzania wetu na zinazopaswa kukemewa na kila Mtanzania.
- Mataifa yaliyotumbukia katika machafuko ya kisiasa, vita vya wao kwa wao na mengine kukumbwa na mauaji ya kimbari, yalianza na kauli chochezi za mtu mmoja mmoja, baadaye vikundi na hatimaye zikatengeneza.
- Zipo nchi nyingi, zikiwemo jirani zetu Rwanda na Kongo, kule Sierra Leone, Ivory Coast, Liberia, Somalia, Sudan na nyinginezo, ambazo zimebaki na makovu ya "Uwendawazimu wa Kihaldiki" ambayo, hata pale amani iliporejea (au itakaporejea), bado makovu hayo yataendelea kubaki kama sanamu ya kumbukumbu ya majuto!
- Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa sababu ya misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu na utamaduni wa kukaa katika meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zetu. Na kwa sababu hiyo, kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa ni makazi ya matumaini kwa wakimbizi wanaokimbia machafuko ya kisiasa na vita katika nchi zao.
- Hivyo basi, Watanzania, kwa umoja wetu tukatae kuhudhuria karamu ya uchochezi wenye lengo la kutushawishi kulewa "Uwendawazimu wa Kiholaiki", ambao unaweza kulisambaratisha Taifa letu kama ilivyotokea katika mataifa mengine!
- Sisi Wakuu wa Vyombo vya Habari na Wahariri Waandamizi tunaungana na viongozi wa dini na makundi mengine yaliyojitokeza kusisitiza umuhimu wa kutunza amani tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba.
Pia soma ~ Uchaguzi Mkuu wa 2025 na uadilifu wa Vyombo vya Habari Tanzania