Wakuu wa Mikoa, Wilaya mshukuruni Mungu kwa kulinda ajira zenu. Mvua bwelele nchi nzima

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Mungu acha tu aitwe Mungu! Mioyo ya watanzania ilishakuwa yenye mfadhaiko, manung'uniko, ghadabu, hasira, hofu nk kuhusu baa la njaa nchini kutokana na kukosekana na mvua maeneo mengi (karibu yote).

Watu walishafikia hatua ya kuilaumu mno serikali ya Mh Rais wetu mpendwa, Dk John Pombe Magufuli. Wanasiasa nao hasa wakuu wa mikoa, Wilaya walishaonywa kwamba wasitangaze njaa katika maeneo yao.

Joto katika maeneo mengi nchini lilishapanda mno kiasi cha kutishia uhai wabinadamu, wanyama na kukauka kwa vyanzo vya maji.

Ajira za wakuu wa mikoa, wilaya zipo salama sasa, mvua imemwagika kote nchini.Wananchi tukalime, tulime kilimo cha kisasa na chenye tija yaani KILIMO BIASHARA.

Asante Mungu kutuletea mvua kote nchini.
 
Katumwa huyo kwani vibarua vinahusiana nini na mvua na wakati aliyewapa ajira ndo kawambia wasitangaze kuna njaa
 
Back
Top Bottom