Wakuu wa mikoa wapanguliwa

Nimewapata:
Wengine ni Luvuvi From Dom to Dar akafukuzane na Machinga. Kandoro From Dar to Mwanza, Nsekela from mwanza to Dom, Babu from Kilimanjaro to Kagera(karudishwa kwao), Mfuru from kagera to Mara. Machibya from Mara to Morogoro na Kalembo ametoka Moro kwenda Tanga. Mbeya hakuna changes. kijana wa zamani anaendelea kutesa. Rukwa na Mikoa mingine ambayo haikutajwa hapa haikuguswa. In fact, hakuna jipya zaidi ya kupeana posho ya uhamisho.
 
Maswali yanayonijia
1. Hivi gharama za kuwahamisha wote hao ni kiasi gani??? (Pesa za mlala hoi)
2. Hivi sababu za kuwabadilisha ni zipi?? (Especially kama hakuana wapya walioteuliwa)
3. Hivi umuhimu wao au kazi ni nini?? (ukichukulia mkoa mmja wakuu wa mikoa 5 in 3 years)
4. Maswali hayaishi................!!!!! Nafikiri hivi vyeo ni vya wana CCM kutesa kwa zamu!!!!!!!!!!
 
Maswali yanayonijia
1. Hivi gharama za kuwahamisha wote hao ni kiasi gani??? (Pesa za mlala hoi)

Huwa wanazificha sana man! Don't try to calculate that at home, you may faint! Huwa wanasafirisha hadi bata na nguruwe
 
Machibya from Mara to Morogoro na Kalembo ametoka Moro kwenda Tanga

Hivi wakuu wa mikoa huwa hawana umri wa kustaafu, huyu mjeshi mstaafu Saidi Kalembo sijui ameishafanya nini pale Morogoro zaidi ya kuwa na vimada kila Wilaya ya Mkoa wake....nadhani undugu wake na mama Salma JK ndo unaomfanya aendelee kutesa ....shame on you! Tanga mnakazi jamaa ni bomu haswa heri muwe hamna mkuu wa the so called mkoa!!
 
Mimi nilidhani wale vilaza wote wanapigwa chini kumbe ni mchezo ule wa ku-recycle!! Yetu macho

..teh teh, jamaa ni environmentalist anajua umhimu wa recycling for environmental conservation. LoL!
 
Uteuzi huo inaelekea kabisa unalenga kutafuta kura mwaka 2010. Waliobadilishwa mikoa wanatakiwa kuwa karibu na majimbo watakayogombea ili waweze kushinda ifikapo 2010. Lakini pia, ili waweze kumsaidia Rais kupata kura za kutosha.

Ukweli unabaki kuwa, Rais anayo mamlaka ya kuteua wakuu wa mikoa kama anavyotaka. Hiyo ndio gharama ya kura alizopewa 2005.
 
Namjua huyo mama in personal ni mchemfu haswa....hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji....

Kampeni za Morogoro zilikuwa ngumu kidogo 2005 Mama alisaidia sana wacha ale matunda si ndio mwendo wenyewe. LoL
 
Uteuzi huo inaelekea kabisa unalenga kutafuta kura mwaka 2010. Waliobadilishwa mikoa wanatakiwa kuwa karibu na majimbo watakayogombea ili waweze kushinda ifikapo 2010. Lakini pia, ili waweze kumsaidia Rais kupata kura za kutosha.

majimbo gani wanaenda kugombea? Wanatarajiwa kumsaidia raisi nini?
 
William Lukuvi karibu Dar es Salaam,Dar si mchezo...Kuna viporo walivyokuachia wenzako Makamba na Kandoro kama Mgogoro wa wamachinga,Mgogoro wa ardhi Kigamboni,Maghorofa yanayoporomoka kila mwaka mara 2,Mgogoro wa upanuzi wa uwanja wa ndege Kipawa bila kusahau kuwapokea na kuwaaga wageni mbalimbali wa nchi yetu!! na kubwa zaidi ni kumsindikiza na kumpokea Vasco Da Gama aka Bartholomew Diaz aka Mh. JK zaidi ya mara 20 kila mwezi Airport...
MUHIMU:
jiandae kukesha wiki hii kwani SIMBA na YANGA wanacheza wiki hii wanaweza kuvuruga mambo...zaidi muulize Kandoro...
 
- Lukuvi, alikosea mahesabu tu na kum-support Sumaye kwa siri kwenye urais, otherwise ni Lowassa to the teeth, na Muungwana hajawahi kumsamehe hii ni njia tu ya kumtolea nje next!

- Na kama unaelewa vizuri huu upanguzi ni kupunguza nguvu za Lowassa tu na 2010, ukiwa Dodoma unakuwa na nguvu ya ajabu sana kuliko Dar as far as uchaguzi is concerned, tuweni makini na uchambuzi wa siasa za taifa letu.

FMES
 
Duh, Mkuu umegonga ilkulu... halafu na macho makavu sana!!!! HAkuna sensor wala filter hapo

Ndinalio
 
Mr. zero
Gharama ni kama ifuatavyo:
Subsistence Allowance Mr & Mrs X 80,000.00 X 14dys= 2,240,000.00
+ watoto 4 X 40,000.00 X 14dys= 2,240,000.00

- Disturbance Allowance 823,000
- Kusafirisha mizigo = 2,000,000/=
- Night Allowance kwenda kuripoti na kurudi kufunga mizigo kwa Mhe. 80,000.00 X 14
Days= 1,120,000.00
Posho ya dereva Dereva 45,000.00 X 14= 630,000.00
Wastani wa Mafuta kwa anayetoka Ruvuma kwenda Kilimanjaro Lita 540 X 1,500.00 kwa lita = 810,000.00
Gharama ya kusafirisha gari binafsi kama unalo 700,000.00
JUMLA KUU= 10,563,000.00 kwa Familia moja. Hapa wamehamishwa 11 zidisha mara 11 utapata 116,193,000.00
Hapo hujaletewa risiti za kuokoteza na gharama za kubadili samani za nguvu na magodoro ya nyumba ya Mhe. maana kila takachokuta atakiita kichafu. Nilisahau gharama za ukarabati wa nyumba hizo. Ni lazima zipakwe rangi au kubomoa kuta ili zifiti mahitaji ya Mkuu. Piga hesabu.Kwa wastani gharama ya ukarabati itakuwa ni Tshs. ngapi. Obviously haipungui 50,000,000.00 ukizidisha mara 11 utapata = 550,000,000.00. Mzee kazi ipo. Kwa mawazo yangu tija haipatikani kwa kuhamisha watu tu. Kama umeshindwa umeshindwa huwezi kuuja na jipya. Nimepata pia kutoka mtonyaji wangu wa unyalu kuwa Kandoro kapigwa Mwanza ili kumzuia kuanza kampeni mapema za kugombea Jimbo la Kalenga.Kama ambavyo mpiga debe wake Bw. Elaston Mbwilo alivohamishiwa Mtwara.
 
Ninavyojua mimi jimbo la Kalenga linaenda CHADEMA wamejipanga vizuri sana kule mgombea wao anauzika kirahisi sana, ndo maana Kandoro alianza kupeleka mabati na kujipendekeza huko....habari ndo hiyo!
 
Hizi gharama itaendelea kuwa butu (sunken costs) mpaka hapo wananchi watakapojua maana yake na umuhimu wa kila senti inayotokana na kodi. Kwa wenzetu ukinunu kitu dukani ukakosa senti moja au penny hupewi. Tanzania hata ukipungukiwa 500 (kama $0.4) bado unapewa kitu na kuchekewa. Tukishajua kuwa kila senti ina maana yake na ni muhimu sana basi tunaweza kuanza mchakato wa kuongelea kodi zetu. Vinginevyo wazee wanavuna na kupata mtaji wa kuanzia kampeni!

Nadhani siyo kweli kwamba hii recycling itawafaidisha wahusika binafsi. Mfano itakuwaje rahisi kwa Dr Ishengoma kuja Moro kupiga kampeni za viti maalumu au Mbega kwenda Iringa. Kuna mchezo fulani wa kijinga hapa. Labda hoja ya FMES inaweza kuwa na mshiko!
 
Samahani wandugu. Aulizaye ataka kujua.

Huyu LUKUVI sio yule KILAZA asiye na degree na alinunua degree PACIFIC au sijui wapi?

Nimeuliza tu!
 
Hapa naona JK kama amepanga kete kwenye draft....lakini kusukuma kete vidole vizito.
Kazi tunayo sijui maisha bora yatatoka wapi hapo....
 
Ninavyojua mimi jimbo la Kalenga linaenda CHADEMA wamejipanga vizuri sana kule mgombea wao anauzika kirahisi sana, ndo maana Kandoro alianza kupeleka mabati na kujipendekeza huko....habari ndo hiyo!

Hayo mabati aliyo peleka kule ni ile michango tuliyo changishwa hapa Dar na mpaka jamaa sasa wamemuamisha hatujasomewa mapato ni kiasi gani wananchi wamechangia shule za kata?
Bongo kweli mfilisi.
 
Mmmhhhh!!! yaani Mwakipesile na kelele zote za Mbeya bado kabakizwa kule kule? Kweli siasa ni ngumu na inakuwa ngumu sana kuelewa maamuzi ya wanasiasa.

Mimi nilifikiri kukiwa na uhamisho wa wakuu wa mikoa basi Mwakipesile angelikuwa wa kwanza kuhamishwa.

Kweli kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji!
 
Back
Top Bottom